Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Jubilei ya miaka 150 ya Uinjilishaji Tanzania

Askofu Flavian Matindi Kassala wa Jimbo Katoliki Geita anasema, familia ni kitovu cha malezi ya kiutu, kijamii na maisha ya kiroho.

Askofu Flavian Matindi Kassala wa Jimbo Katoliki Geita anasema, familia ni kitovu cha malezi na majiundo ya kiutu, maisha ya kiroho na kitamaduni.

Askofu Kassala: familia ni chemchemi ya malezi na majiundo ya kiutu

19/05/2018 14:10

Familia ni Kanisa dogo la nyumbani, shule ya utakatifu, haki, amani, upendo na maridhiano. Ni mahali pa kwanza kabisa pa kukuza na kudumisha tunu msingi za maisha ya kiutu, maisha ya kiroho, kijamii na kitamaduni. Familia ni mahali pa kutakatifuzana katika ndoa! Ni shule ya huruma na upendo.

 

Viongozi wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania wanatambua changamoto, fursa na matatizo katika malezi na majiundo ya kipadre: Yanashughulikiwa!

Viongozi wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania wanatambua matatizo, changamoto na fursa za malezi ya wuto wa kipadre, na kwamba, wameanza kuzivalia njuga ili kuandaa mwongozo wa malezi ya kipadre kitaifa.

Changamoto za malezi na majiundo ya kikasisi nchini Tanzania!

23/04/2018 14:51

Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 150 ya Uinjilishaji Tanzania Bara sanjari na Mwaka wa Padre Tanzania ulioadhimishwa mwaka 2017 kama kumbu kumbu ya Jubilei ya Miaka 100 tangu Mapadre wa kwanza wazalendo kuwekwa wakfu. Hii ni nafasi ya kutafakari kuhusu; wito, utume na maisha ya kipadre!

Askofu Mkude: Waamini wajitahidi kumfahamu na kuwambata Kristo Yesu pamoja na kudhibiti vilema vya maisha yao!

Askofu Mkude: Anawataka waamini wajitahidi kumfahamu, kumwambata na kumshuhudia Kristo katika uhalisia wa maisha ya pamoja na kujitahidi kudhibiti vilema vya maisha yao!

Ujumbe wa Pasaka 2018 kutoka kwa Askofu Mkude, Jimbo la Morogoro

31/03/2018 16:48

Askofu Telesphor Mkude wa Jimbo Katoliki Morogoro nchini Tanzania katika maadhimisho ya Fumbo la Pasaka kwa Mwaka 2018 sanjari na Jubilei ya Miaka 150 ya Ukatoliki Tanzania Bara anawaalika waamini kujibidisha kumfahamu na kumshuhudia Kristo sanjari na kujizatiti katika kushinda vilema vyao!

Kanisa Katoliki Tanzania linaadhimisha Pasaka ya 150 tangu wainjilishwe! Matendo makuu ya Mungu!

Kanisa Katoliki Tanzania linaadhimisha Pasaka ya 150 tangu wainjilishwe!

Askofu mkuu Ruwaichi: Ujumbe wa Pasaka na Miaka 150 ya Ukatoliki

31/03/2018 12:02

Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi wa Jimbo Kuu la Mwanza katika uujumbe wake wa Pasaka kwa mwaka 2018 anamwomba Mwenyezi Mungu awapatie Wakristo wote nchini Tanzania nguvu, uthubutu na furaha ya kumshangilia Kristo Mfufuka bila woga, kigugumizi na wala bila ubaridi wowote ule!

TEC: Kwaresima 2018: Jubilei Miaka 50 ya Ukatoliki na Uinjilishaji; Miaka 50 ya Hatima ya Tanzania & Haki Msingi za Binadamu.

TEC: Kwaresima 2018: Jubilei ya Miaka 150 ya Ukatoliki na Uinjilishaji Tanzania Bara; Miaka 50 tangu Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania litoe Waraka kuhusu Hatima ya Tanzania na Maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, 2019.

TEC: Kwaresima 2018: Jubilei ya Miaka 150, Maendeleo & Haki msingi!

27/03/2018 13:56

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania katika ujumbe wake wa Kwaresima kwa mwaka 2018, limetoa dira na mwelekeo wa tafakari kuhusu maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 150 ya Ukatoliki na Uinjilishaji Tanzania Bara; Miaka 50 ya Waraka wa Hatima ya Tanzania pamoja na Haki msingi za binadamu!

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania katika ujumbe wake wa Kwaresima linaitaka familia ya Mungu kujiuliza swali la msingi Je, ndugu yako yuko wapi?

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania linaialika familia ya Mungu kujiuliza swali la msingi, Je, ndugu yako yuko wapi?

Maaskofu Katoliki Tanzania: Kwani mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?

22/03/2018 15:05

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania katika ujumbe wake wa Kwaresima kwa mwaka 2018 linaitaka familia ya Mungu kujiuliza swali msingi "Ndugu yako yuko wapi? Huu ni mwaliko wa kutafakari mahusiano na mafungamano yao kama watanzania katika masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii!

Ufuasi wa kweli kwa Kristo Yesu unafumbatwa katika: ari ya kimisionari, sadaka na ushuhuda wa imani katika matendo!

Ufuasi wa kweli kwa Kristo Yesu unafumbatwa katika ari ya kimisionari, sadaka na ushuhuda wa maisha ya kila siku!

Baraza la Makanisa Ulimwenguni: Utume unafumbata sadaka na ushuhuda

14/03/2018 09:45

Baraza la Makanisa Ulimwenguni katika mkutano wake mkuu wa uinjilishaji ulimwenguni, limefafanua kwamba, utume na ufuasi kwa Kristo Yesu na Kanisa lake kwa namna ya pekee kabisa, unafumbatwa katika:ari na nia thabiti ya kumfuasa Kristo pamoja na ushuhuda wenye mvuto na mashiko, kila siku!

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania: Kilele cha Jubilei, tarehe 7 Oktoba 2018: Kauli mbiu: Miaka 150 ya Uinjilishaji, Furaha ya Injili.

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania: Kilele cha Jubilei Jumapili tarehe 7 Oktoba, 2018. Kauli mbiu: Miaka 150 ya Uinjilishaji, Furaha ya Injili.

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania: Maelekezo muhimu!

09/03/2018 15:30

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania linatangaza kwamba, kilele cha Jubilei ya Miaka 150 ya Ukatoliki Tanzania Bara ni Jumapili tarehe 7 Oktoba 2018 huko Bagamoyo kwa kuongozwa na kauli mbiu: Miaka 150 ya Uinjilishaji, Furaha ya Injili. Jumapili tarehe 10 Machi 2018 waamini wanaalikwa kuchangia.