Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Jubilei ya miaka 100 ya Bikira Maria wa Fatima

Dhamana na wajibu wa wanadiplomasia ni kukuza na kudumisha majadiliano katika ukweli na uwazi kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi.

Dhamana na wajibu wa wanadiplomasia ni kuhakikisha kwamba wanakuza na kudumisha majadiliano katika ukweli na uwazi kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi.

Dhamana ya wanadiplomasia ni kukoleza majadiliano, haki na amani!

09/01/2018 07:08

Dhamana na wajibu mkubwa wa wanadiplomasia ni kuhakikisha kwamba, wanajitahidi kujenga na kudumisha utamaduni wa majadiliano katika ukweli na uwazi ili kukuza na kuendeleza misingi ya haki, amani, upendo na mshikamano wa kimataifa, mwanadamu akipewa kipaumbele cha kwanza!

Jubilei ya Miaka 100 ya Bikira Maria wa Fatima imekuwa ni musa wa sala, toba na wongofu wa ndani!

Jubilei ya Miaka 100 ya Bikira Maria wa Fatima umekuwa ni muda wa sala, toba na wongofu wa ndani!

Kanisa lahitimisha Jubilei ya Miaka 100 ya B. Maria wa Fatima

14/10/2017 13:34

Jubilei ya Miaka 100 tangu Bikira Maria alipowatokea Watoto wa Fatima, imekuwa ni fursa kwa familia ya Mungu sehemu mbali mbali za dunia kujikita katika sala kwa ajili ya kuombea haki, amani na maridhiano kati ya watu;  kutubu na kumwongokea Mwenyezi Mungu pamoja na kushuhudia imani kwa dhati!

Papa Francisko anasema, madhabahu ni mahali pa uinjilishaji unaofumbatwa katika ushuhuda wa imani na matendo ya huruma!

Papa Francisko anasema, madhabahu ni mahali pa uinjilishaji unaofumbatwa katika ushuhuda wa imani na matendo ya huruma: kiroho na kimwili.

Madhabahu ni mahali muafaka pa uinjilishaji na ushuhuda wa imani

14/10/2017 10:33

Baba Mtakatifu Francisko katika barua yake binafsi "Madhabahu ndani ya Kanisa" anakiri umuhimu wa madhabahu haya kuwa ni sehemu muafaka pa uinjilishaji unaojikita katika ushuhuda wa imani kwa Kristo na Kanisa lake! Hapa ni mahali ambapo huduma ya upendo na mshikamano vinashuhudiwa!

Maaskofu wa Jimbo Kuu la Owerri Nigeria wanasema hiki ni kipindi cha toba na wongofu wa ndani; amani, msamaha na upatanisho.

Maaskofu wa Jimbo kuu la Owerri, Nigeria wanasema hiki ni kipindi cha toba na wongofu wa ndani; msamaha, haki, amani na upatanisho wa kweli!

Nigeria ni wakati wa toba na wongofu wa ndani; msamaha na upatanisho

28/08/2017 09:19

Maaskofu wa kutoka Jimbo kuu la Owerri, Nigeria wanasema, sasa ni wakati wa toba na wongofu wa ndani; msamaha na upatanisho ilikujenga amani, ustawi na maendeleo ya wengi: kiroho na kimwili. Ni wakati wa kuganga na kuponya madhara ya vita, ghasia, chuki na uhasama kwa kukumbatia amani na utulivu.

Mapadre wanahamasishwa kupyaisha maisha na utume wao kwenye shule ya Bikira Maria.

Mapadre wanahamasishwa kupyaisha maisha na utume wao kwenye shule ya Bikira Maria.

Mapadre endelezeni maisha na utume wenu katika shule ya Bikira Maria

17/08/2017 13:36

Bikira Maria ni mfano na kielelezo cha imani, matumaini na mapendo, kwani amediriki kuwa ni mfuasi amini wa Kristo Yesu na chombo cha huduma makini kwa jirani zake; mtindo na mfumo wa maisha unaopaswa kutekelezwa na Mapadre kama sehemu ya majiundo yao ya awali na endelevu katika Kanisa.

Kardinali Leonardo Sandri amehitimisha ziara yake ya kikazi nchini Australia kwa kuhimiza: umoja na mshikamano; ushuhuda, upendo, mshikamano na huduma

Kardinali Leonardo Sandri amehitimisha ziara yake ya kikazi nchini Australia kama sehemu ya maadhimisho ya Jubilei ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki, amekazia umoja, upendo, mshikamano na huduma kwa maskini, wakimbizi na wahamiaji.

Kardinali Sandri mkazo: Umoja wa Kanisa na ukarimu kwa maskini!

18/05/2017 07:30

Kardinali Leonardo Sandri amehitimisha safari yake ya kikazi nchini Australia kama sehemu ya maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 100 tangu Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki lilipoanzishwa. Amekazia umuhimu wa kujenga na kudumisha umoja na mshikamano na huduma kwa maskini zaidi!

Vita, mifumo ya biashara na utumwa mamboleo na biashara ya silaha ni hatari kwa amani, utu na heshima ya binadamu.

Vita, mifumo ya biashara na utumwa mamboleo ni hatari kwa amani, utu na heshima ya binadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano ya Mungu.

Bado kuna vitendo vinavyotishia amani, utu na heshima ya binadamu!

17/05/2017 14:17

Askofu mkuu Bernardito Auza, Mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Umoja wa Mataifa anasema kuna vitendo ambavyo bado vinatishia, amani, usalama, utu, heshima na haki msingi za binadamu! Vitendo hivi ni vita, biashara haramu ya binadamu na mifumo yake pamoja na biashara ya silaha.

Madhabahu ya Bikira Maria ni mahali maalum pa uinjilishaji mpya, toba na wongofu wa ndani!

Madhabahu ya Bikira Maria ni mahali pa uinjilishaji makini; shule ya: Imani, Sakramenti, Amri za Mungu na Maisha ya Sala.

Madhabahu ni mahali pa uinjilishaji wa kina, toba na wongofu wa ndani

17/05/2017 13:49

Baba Mtakatifu Francisko anasema, madhabahu au vituo vya hija ni mahali muafaka pa uinjilishaji wa kina unaogusa undani wa maisha ya mtu; toba na wongofu wa ndani. Hapa ni mahali pa katekesi makini kuhusu: Imani, Sakramenti za Kanisa, Amri za Mungu na Maisha ya sala na tafakari makini!