Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu
Lugha:
Jimbo kuu la Dublin, Ireland
Jubilei ya Miaka 50 ya Waraka wa Paulo VI "Humanae vitae", mwaliko kwa waamini na watu wote wenye mapenzi mema kusimamakidete kulinda, kutetea na kudumisha Injili ya maisha.
Mama Kanisa tarehe 25 Julai 2018 anaadhimisha kumbu kumbu ya Jubilei ya Miaka 50 tangu Mwenyeheri Paulo VI alipochapisha Waraka wake wa Kitume "Humane vitae" yaani "Maisha ya mwanadamu" kwa kuonesha dhamana na wajibu wa kurithisha zawadi ya uhai; kwa uhuru na waujibaki mkubwa!
Baraza la Maaskofu Katoliki Ireland linawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kujiunga nao ili kusherehekea Injili ya familia kwa mwaka 2018.
Baraza la Maaskofu Katoliki Ireland linawalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kushiriki kikamilifu katika maandalizi na hatimaye, maadhimisho ya Siku ya IX ya Familia Duniani huko Dublin, nchini Ireland kwa kutafakari: ukuu, utakatifu na changamoto za Injili ya familia!
Papa Francisko ametangaza nia ya kushiriki katika maadhimisho ya Siku ya IX ya Familia Duniani, Dublin, Ireland kuanzia tarehe 25-26 Agosti, 2018.
Baba Mtakatifu Francisko ameonesha nia ya kushiriki katika maadhimisho ya Siku ya IX ya Familia Duniani inayoadhimishwa Jimbo kuu la Dublin nchini Ireland kuanzia tarehe 21 hadi 26 Agosti 2018 ili kutangaza na kushuhudia Injili ya furaha, chemchemi ya furaha kwa ulimwengu!
Maaskofu Barani Ulaya wanataka kuwekeza zaidi katika utume kwa vijana na kwenye tunu msingi za maisha ya ndoa na familia.
Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Barani Ulaya, Ccee, linataka kuwekeza zaidi katika majiundo makini kwa vijana wa kizazi kipya ili kuwajengea uwezo wa kupambana na changamoto za maisha kwa njia ya imani makini sanjari na kujikita katika tunu msingi za Injili ya familia!
Baba Mtakatifu Francisko anawaalika wanandoa kuwa ni mashuhuda na vyombo vya Injili ya familia: furaha ya ulimwengu.
Maadhimisho ya Siku ya 9 ya Familia Kimataifa kwa mwaka 2018 huko Jimbo kuu la Dublin, nchini Ireland ni wakati muafaka wa kutafakari kuhusu tunu msingi za maisha na utume wa ndoa na familia, ili kujizatiti kuwa tayari kutangaza na kushuhudia Injili ya familia chemchemi ya habari njema kwa watu!
Mitandao ya kijamii: