Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Injili ya Matumaini

Kanisa linapaswa kusikiliza kilio cha maskini na kukata kiu yao kwa njia ya huduma ya maendeleo endelevu kiroho na kimwili.

Kanisa linapaswa kusikiliza kilio cha maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii kutokana na umaskini, ujinga na maradhi na kukata kiu yao kwa kuwa na sera na mikakati makini ya maendeleo endelevu ya binadamu yanayogusa mahitaji yao msingi: kiroho na kimwili.

Kanisa lisikilize kilio na kukata kiu ya maskini wanaoteseka duniani

23/02/2018 07:13

Kanisa halina budi kuendelea kuwa ni sauti ya kinabii kwa kusoma alama za nyakati ili kuweza kusikiliza kilio cha maskini wanaoteseka kutokana na umaskini, ujinga, maradhi pamoja na ukosefu wa haki msingi za binadamu; mambo yanayodhalilisha utu na heshima yao kama binadamu! Vinginevyo Kanisa....!

 

Papa Francisko anaitaka Kamati ya Ushauri Kitaifa Italia dhidi ya michezo ya kamari na upatu kutoa kipaumbele kwa waathirika!

Papa Francisko anaitaka Kamati ya Ushauri Kitaifa nchini Italia dhidi ya michezo ya Kamari na Upatu ya Yohane Paulo II kutoa kipaumbele cha kwanza kwa waathirika wa michezo hii ili kuwaonjesha Injili ya matumaini.

Papa Francisko: Waathirika wa Kamari na Upatu wapewe kipaumbele!

22/02/2018 11:52

Baba Mtakatifu Francisko hata baada ya kukutana na kuzungumza na Kamati ya Ushauri Kitaifa nchini Italia dhidi ya michezo ya kamari na upatu hapo tarehe 3 Februari 2018 amemwandikia barua Rais wa Kamati hii kumtaka kutoa kipaumbele cha kwanza kwa waathirika wa michezo ya kamari na upatu!

Siku ya IX ya Familia Duniani inapania kukazia sera na mikakati ya kutangaza na kushuhudia Injili ya familia duniani.

Siku ya IX ya Familia Duniani inapania kukuza na kudumisha sera na mikakati ya Injili ya familia duniani inayofumbatwa katika Injili ya uhai na huruma ya Mungu!

Siku ya Familia Duniani kwa Mwaka 2018, Jimbo kuu la Dublin, Ireland

09/02/2018 07:10

Ni matumaini ya Baba Mtakatifu Francisko kwamba, baada ya maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya Huruma ya Mungu, Siku ya IX ya Familia Duniani huko Jimbo kuu la Dublin, Ireland itakuwa ni fursa makini ya kumwilisha Injili ya huruma ya Mungu katika maisha na utume wa familia duniani.

Michezo ya kamari na upatu ni hatari sana kwa maisha ya watu wengi nchini Italia!

Michezo ya kamari na upatu ni hatari sana kwa wananchi wengi nchini Italia.

Mchezo wa kamari na upatu ni hatari sana kwa maisha ya watu!

03/02/2018 15:44

Kamati ya Ushauri Kitaifa nchini Italia dhidi ya mchezo wa kamari na upatu, Jumamosi, tarehe 3 Februari 2018 imepata nafasi ya kukutana na kusali kwenye kaburi la Mtakatifu Yohane Paulo II ili kuomba ulinzi na tunza yake katika mapambano dhidi ya athari za michezo ya kamari na upatu kwa watu.

Papa Francisko anaishukuru familia ya Mungu nchini Perù kwa wema na ukarimu waliomwonjesha wakati wa hija yake ya kitume nchini humo.

Papa Francisko anaishukuru familia ya Mungu nchini Perù kwa wema, ukarimu na mapokezi makubwa waliyomwonesha wakati wa hija yake ya kitume nchini humo.

Papa Francisko anaishukuru familia ya Mungu nchini Perù kwa ukarimu

22/01/2018 15:51

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu, amewashukuru wale wote waliojisadaka ili kufanikisha hija yake ya kitume nchini Perù na kwamba, anaporejea tena mjini Vatican anapenda kuwabeba na kuwahifadhi katika sakafu ya moyo wake kwa matumaini makubwa!

 

Huruma na upendo ni chachu ya mchakato wa ujenzi mpya wa matumaini yanayofariji, kuganga na kuponya!

Huruma na upendo ni chachu ya mchakato wa ujenzi mpya wa matumaini yanayofariki, yanayoganga na kuponya madonda ya mwanadamu!

Papa Francisko asema, mshikamano wa upendo ni ushuhuda wa matumaini

21/01/2018 14:50

Moyo wa mshikamano na upendo katika kupambana na matatizo na changamoto za maisha ni kielelezo cha hali ya juu kabisa cha ushuhuda wa Injili ya matumaini inayomwilishwa katika uhalisia wa maisha ya watu wa Mungu na kwa njia hii, wakristo wanaweza kutambulikana kuwa kweli ni wafuasi wa Yesu.

Papa Francisko asema, vijana ni chachu ya mageuzi ya kijamii, upyaisho wa Kanisa na kiini cha maisha na utume wa Kanisa.

Papa Francisko anasema vijana ni chachu ya mageuzi na upyaisho wa KanisA; Niini cha maisha na utume wa Kanisa.

Vijana ni chachu ya mageuzi na kiini cha maisha na utume wa Kanisa!

18/01/2018 08:15

Baba Mtakatifu Francisko anapenda kuwahakikishia vijana kwamba, wao ni sehemu muhimu sana ya mageuzi ya kijamii na chachu inayolipyaisha Kanisa! wao ni kiini cha maisha na utume wa Kanisa, ndiyo maana ameitisha Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana ili Kanisa liweze kujifunza kutoka kwa vijana!

Papa Francisko anawataka wananchi wa Chile kujenga utamaduni wa umoja, mshikamano, maridhiano na kusikilizana.

Papa Francisko anawataka wananchi wa Chile kujenga utamaduni wa umoja, mshikamano na maridhiano kwa kuheshimiana, kuthaminiana na kukamilisha katika maisha.

Papa Francisko: Jengeni utamaduni wa umoja, upatanisho na kusikilizana

17/01/2018 14:48

Baba Mtakatifu Francisko anawataka wananchi wa Chile kujenga utamaduni wa umoja unaofumbatwa katika zawadi ya amani unaowawezesha watu kusikilizana, kushikamana, kutegemeana na kukamilishana ili kuimarisha upatanisho dhidi ya nguvu zinazotishia Injili ya matumaini!