Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Injili ya Huruma ya Mungu

Caritas Internationalis inawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kushiriki katika safari ya matumaini ya wakimbizi na wahamiaji.

Caritas Internationalis inawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kushiriki katika safari ya matumaini ya wakimbizi, wahamiaji na watu wanaotafuta hifadhi ya kisiasa.

Caritas Internationalis: 17-24 Juni 2018 Juma la Upendo kwa vitendo

14/05/2018 12:05

Baba Mtakatifuf Francisko mwezi Septemba 2017 alizundua rasmi kampeni ya kimataifa ya ukarimu kwa wakimbizi, wahamiaji na watu wanaotafuta hifadhi ya kisiasa inayoongozwa na kauli mbiu "Share the journey" yaani "Shiriki safari" kama kielelezo cha kumwilisha fadhila ya upendo katika maisha!

Kanisa linapaswa kusikiliza kilio cha maskini na kukata kiu yao kwa njia ya huduma ya maendeleo endelevu kiroho na kimwili.

Kanisa linapaswa kusikiliza kilio cha maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii kutokana na umaskini, ujinga na maradhi na kukata kiu yao kwa kuwa na sera na mikakati makini ya maendeleo endelevu ya binadamu yanayogusa mahitaji yao msingi: kiroho na kimwili.

Kanisa lisikilize kilio na kukata kiu ya maskini wanaoteseka duniani

23/02/2018 07:13

Kanisa halina budi kuendelea kuwa ni sauti ya kinabii kwa kusoma alama za nyakati ili kuweza kusikiliza kilio cha maskini wanaoteseka kutokana na umaskini, ujinga, maradhi pamoja na ukosefu wa haki msingi za binadamu; mambo yanayodhalilisha utu na heshima yao kama binadamu! Vinginevyo Kanisa....!

 

Waamini jifunezni tena Injili ya Huruma ya Mungu, ufuno wa Uso na haki ya Mungu kwa binadamu!

Waamini jifunzeni tena Injili ya Huruma ya Mungu ambayo ni Ufunuo wa Uso na haki ya Mungu kwa binadamu!

Jifunzeni kumwilisha Injili ya Huruma ya Mungu katika maisha!

22/02/2018 10:43

Injili ya huruma ya Mungu ni chanda na pete na Furaha ya Injili inayokita mizizi yake katika toba na wongofu wa ndani; upendo na mshikamano wa dhati kama ulivyoshuhudiwa na Baba mwenye huruma. Injili ya huruma ni ufunuo wa Uso na Haki ya Mungu; ni divai ya upendo na uhuru kamili katika ukweli!

Siku ya IX ya Familia Duniani inapania kukazia sera na mikakati ya kutangaza na kushuhudia Injili ya familia duniani.

Siku ya IX ya Familia Duniani inapania kukuza na kudumisha sera na mikakati ya Injili ya familia duniani inayofumbatwa katika Injili ya uhai na huruma ya Mungu!

Siku ya Familia Duniani kwa Mwaka 2018, Jimbo kuu la Dublin, Ireland

09/02/2018 07:10

Ni matumaini ya Baba Mtakatifu Francisko kwamba, baada ya maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya Huruma ya Mungu, Siku ya IX ya Familia Duniani huko Jimbo kuu la Dublin, Ireland itakuwa ni fursa makini ya kumwilisha Injili ya huruma ya Mungu katika maisha na utume wa familia duniani.

Nabii wa kweli anatangaza Neno; Yesu ni Ufunuo wa huruma na upendo wa Mungu kwa watu wake.

Nabii wa kweli anatangaza Neno! Yesu Kristo ni ufunuo wa huruma na upendo wa Mungu kwa watu wake.

Wandugu zalisheni mazao yenye viwango na tija! Vinginevyo...!

06/10/2017 07:53

Tafakari ya Neno la Mungu, Jumapili ya XXVII ya Kipindi cha Mwaka wa Kanisa ni mwaliko wa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu yenye: viwango, tija na mashiko! Nabii wa kweli ni yule anayesadaka maisha yake kwa ajili ya Mungu! Yesu ni ufunuo wa huruma na upendo wa Mungu!

 

Wema, huruma, ukuu na utakatifu wa Mungu hauna mipaka kwa watu wote!

Wema, huruma, ukuu na utakatifu wa Mungu hauna mipaka kwa waja wake wote.

Wema na huruma ya Mungu inawagusa hata wale walioko kijiweni!

23/09/2017 09:54

Kristo Yesu anatumia mfano wa maisha ya mwanadamu kufafanua kuhusu: wema, huruma, ukuu na utakatifu wa Mungu na kwamba, mawazo na njia zake ni tofauti kabisa na mawazo na njia za mwanadamu, kwani Mungu anawalipa wote kadiri ya huruma na mapenzi yake. Mungu ni mwema kwa wote!

Papa Francisko asema: huruma, msamaha na upatanisho ni kati ya mafundisho makuu ya Kristo Yesu kwa wafuasi wake.

Papa Francisko asema: huruma, msamaha na upatanisho ni kati ya mafundisho makuu ya Kristo Yesu kwa wafuasi wake.

Papa Francisko: huruma na msamaha ni mafundisho makuu ya Yesu

18/09/2017 10:09

Baba Mtakatifu Francisko anasema, huruma, msamaha na upatanisho ni kati ya mafundisho makuu ya Yesu yanayopatika kwa muhtasari katika Sala kuu ya Baba Yetu! Huu ni mwaliko kwa wale wote walionja huruma na upendo wa Mungu kuwa ni mashuhuda na vyombo vya huruma ya Mungu kwa jirani zao!