Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Injili ya Furaha

Sinodi ya Maaskofu Ukanda wa Amazonia kwa mwaka 2019 itaongozwa na kauli mbiu "Amazonia: Njia Mpya ya Kanisa na kwa ajili ya Ekolojia Endelevu".

Sinodi ya Maaskofu Ukanda wa Amazonia itaongozwa na kauli mbiu "Amazonia: Njia Mpya ya Kanisa na kwa ajili ya Ekolojia Endelevu".

Sinodi ya Amazonia: Njia mpya ya Kanisa kwa ajili ya ekolojia endelevu

09/04/2018 14:50

Baba Mtakatifu Francisko analitaka Kanisa kujikita katika masuala ya haki, amani na mshikamano; utume na huduma ya upendo, ili kuhakikisha kwamba, Injili ya Kristo inatamadunishwa katika uhalisia wa maisha ya wananchi wa Amazonia, ili Kanisa liweze kupaya sura mpya ya watu wa Amazonia!

Papa Francisko asema, vijana wasipopiga kelele, mawe yatapiga kelele badala yao!

Papa Francisko asema, vijana wasipoiga kelele kupaaza sauti zao ili Kanisa na Jamii iweze kuwasikiliza, kuwapatia nafasi ya kushirikisha karama na mapaji yao, mawe yatapiga kelele badala yao!

Papa Francisko: Vijana msipopiga kelele, mawe yatapiga badala yenu!

26/03/2018 07:49

Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya Jumapili ya Matawi, sanjari na Siku ya XXXIII ya Vijana Duniani ambayo imeadhimishwa katika ngazi ya Kijimbo, amewataka vijana kutoa mawazo, kushirikisha karama na mapaji yao kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi, vinginevyo....!

Papa Francisko analitaka Shirika la Madonda Matakatifu kuwasha moto wa upendo na imani kwa njia ya huduma makini kwa maskini.

Papa Francisko analitaka Shirika la Madonda Matakatifu kuwasha moto wa imani na upendo kwa njia ya huduma makini kwa maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii.

Wamissionari washeni moto wa imani na huduma kwa maskini duniani

10/02/2018 16:23

Baba Mtakatifu Francisko anawataka wamissionari wa Shirika la Madonda Matakatifu kuwasha moto wa imani na huduma kwa watu wanaowainjilisha kwa njia ya ushuhuda unaofumbatwa katika furaha ya Injili wanayoitangaza na kuishuhudia katika upendo wa kidugu katika maisha ya kijumuiya!

 

Papa Francisko anawataka waamini kujenga utamaduni wa mshikamano na upendo kwa kusikiliza na kujibu kilio cha jirani zao.

Papa Francisko anawataka waamini kujenga na kudumisha utamaduni wa upendo kwa kusikiliza na kujibu kilio cha jirani zao

Papa: Tangazeni Injili ya furaha kwa kudumisha haki msingi za binadamu

18/01/2018 15:15

Baba Mtakatifu Francisko anasema, hata leo hii kuna watu "hawana divai" kwa kukosa fursa za ajira ili kuhudumia familia zao; kuna ukosefu mkubwa wa haki msingi za binadamu na utumwa mamboleo unaonyanyasa utu na heshima ya binadamu; haki za wahamiaji ziko rehani; waamini wasimame kidete kuwatetea!

Baraza la Kipapa la Makleri kwa ushirikiano na Sekretarieti ya mawasiliano wameunda Clerus App, inayohusu mahubiri ya kila Jumapili

Baraza la Kipapa la Makleri kwa ushirikiano na Sekretarieti ya mawasiliano wameunda Clerus App, inayohusu mahubiri ya kila Jumapili

Baraza la Kipapa la Makleri wameunda Clerus App, je ni kitu gani?

03/01/2018 16:00

Clerus App ni nyezo msingi ya kuweza kuwa karibu na maparoko kusaidiana katika maandaliza ya tafakari ya kila Jumapili. Hayo ni maelezo ya Mosinyo Andrea Ripa Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makleri kwa ushirikiano na Sekretarieti ya Mawasiliano,ambao wameunda  hiyo App

 

 

Jumapili 19 Novemba ni siku ya Maskini duniani. Tunaalikwa na Kanisa kutazama matendo yetu na hasa tunapopewa talanta je tunazitumia namna gani?

Jumapili 19 Novemba ni siku ya Maskini duniani. Tunaalikwa na Kanisa kutazama matendo yetu na hasa tunapopewa talanta je tunazitumia namna gani?

Tuipande ardhini tunu ya imani ili ichipue,ikue na kuzaa matunda mema

17/11/2017 16:58

Mpendwa msikilizaji wa Radio Vatican! Leo Mama Kanisa anaadhimisha Siku ya kwanza ya maskini duniani.Hili ni zao la Jubilei ya Huruma ya Mungu ambalo linabeba ujumbe mahususi wenye kichwa cha habari:“Tupende si kwa maneno bali kwa matendo”.Huu ni Ujumbe kutekeleza kwa matendo mema. 

 

Watu wa Norcia wakiwa wanasikiliza Misa mbele ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Benedikto. Misa iliyo ongozwa na Kard Parolin

Watu wa Norcia wakiwa wanasikiliza Misa mbele ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Benedikto. Misa iliyo ongozwa na Kard Parolin

Kard Parolin awatia Moyo watu wa Norcia baada ya mwaka 1 wa Tetemeko la ardhi

30/10/2017 10:31

Baba Mtakatifu anawatia moyo ili kuanza safari kwa upya,wasiache kamwe kuelemewa na kushindwa na matatizo,badala yake watazame mbele kwa matumaini ya wakati ujao.Ni maneno ya Kardinali Pietro Parolin wakati wa maadhimisho mbele ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Benedikto 

 

Furaha ya vijana Barani Asia ni kuishi Injili katika wingi wa makabila ya Bara la Asia.

Furaha ya vijana Barani Asia ni kuishi wingi wa Makabila ya Bara la Asia.

Vijana wawasha moto wa Injili Barani Asia!

03/08/2017 16:21

Vijana ni jeuri na matumaini ya Kanisa na Jamii katika ujumla wake. Wanapaswa kusindikizwa katika hija ya maisha yako ili kujengewa utamaduni unaoheshimu na kudumisha Injili ya uhadi dhidi ya utamaduni wa kifo; kwa kujikita katika Injili ya imani, matumaini na mapendo kwa Mungu na jirani.