Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Injili ya familia

Mama Kanisa kwa Mwaka 2018-2019 anakazia: Utume wa Vijana na Maisha ya Ndoa na Familia.

Mama Kanisa kwa Mwaka 2018-2019 anakazia utume wa vijana na maisha ya ndoa na familia.

Vipaumbele vya Kanisa kwa Mwaka 2018-2019: Vijana na familia

21/07/2018 08:41

Mama Kanisa kanisa katika mwaka 2018-2019 anapenda kujielekeza zaidi katika utume kwa vijana, ili kujenga sanaa na utamaduni wa kuwasikiliza, kuwasindikiza na kuwaongoza vijana kufanya maamuzi mazito katika maisha. Pili ni utume wa maisha ya ndoa na familia, ili kutangaza Injili ya familia. 

Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu inaadhimisha Jubilei ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwake kunako mwaka 1968 kwa kukazia: Injili ya familia & ushuhuda

Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, Jimbo kuu la Mombasa, Kenya inaadhimisha Jubilei ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwake kwa kukazia: Injili ya familia; Sakramenti za Kanisa na Jumuiya ndogo ndogo za Kikristo!

Jubilei ya Miaka 50 ya Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, Mombasa!

16/07/2018 10:33

Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, Jimbo kuu la Mombasa, Kenya imekuwa ni fursa ya kuimarisha utume wa maisha ya ndoa na familia; Jumuiya ndogo ndogo za Kikristo na ushuhuda wa imani kwa Kristo na Kanisa lake!

Papa Francisko anawataka vijana kuwa ni mashuhuda na vyombo vya Injili ya familia.

Papa Francisko anawataka vijana kuwa ni vyombo na mashuhuda wa Injili ya familia.

Papa Francisko asema, vijana ni chachu ya mageuzi ya familia!

16/07/2018 07:00

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa washiriki wa kongamano la la Vijana Kitaifa huko kwenye Visiwa vya Caribbean anasema, vijana ni chachu ya mageuzi katika maisha ya ndoa na familia, ili kufanikisha dhamana hii, wanapaswa kuwa ni vyombo na mashuhuda wa Injili ya familia!

Jubilei ya Miaka 50 ya Waraka wa "Humanae vitae", 25 Julai 1968: Changamoto Injili ya uhai dhidi ya utamaduni wa kifo.

Jubilei ya Miaka 50 ya Waraka wa Paulo VI "Humanae vitae", mwaliko kwa waamini na watu wote wenye mapenzi mema kusimamakidete kulinda, kutetea na kudumisha Injili ya maisha.

Kanisa litaendelea kujizatiti kutetea Injili ya uhai!

29/05/2018 13:30

Mama Kanisa tarehe 25 Julai 2018 anaadhimisha kumbu kumbu ya Jubilei ya Miaka 50 tangu Mwenyeheri Paulo VI alipochapisha Waraka wake wa Kitume "Humane vitae" yaani "Maisha ya mwanadamu" kwa kuonesha dhamana na wajibu wa kurithisha zawadi ya uhai; kwa uhuru na waujibaki mkubwa!

Rehema kamili kutolewa na Mama Kanisa kwa waamini watakaotimiza masharti wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani 2018.

Rehema kamili kutolewa na Mama Kanisa kwa waamini watakaotimiza masharti yanayotolewa na Mama Kanisa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani kwa Mwaka 2018.

Papa Francisko: Siku ya Familia Duniani, 2018: Rehema kamili kutolewa

23/05/2018 15:44

Baba Mtakatifu Francisko anasema, rehema kamili itatolewa kwa waamini watakaojiandaa barabara kuadhimisha Siku ya IX ya Familia Duniani huko Jimbo kuu la Dublin, kuanzia tarehe 22 - 26 Agosti 2018. Waamini wanaalikwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na Mama Kanisa ili kupata rehema kamili!

Mfuko wa "Centesimus Annus" unasema changamoto kuu kwa sasa ni: Ukosefu wa ajira, familia na wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji.

Mfuko wa "Centesimus Annus" unasema, changamoto mamboleo ni: ukosefu wa fursa za ajira, kuporomoka kwa tunu msingi za maisha ya ndoa na familia pamoja na wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji duniani.

Changamoto mamboleo: Ukosefu wa ajira, Familia na Wakimbizi!

22/05/2018 07:04

Mfuko wa "Centesimus Annus" kwa ajili ya Khalifa wa Mtakatifu Petro unaadhimisha Jubilei ya Miaka 25 tangu ulipoanzishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kunako mwaka 1993. Changamoto mamboleo ni: ukosefu wa fursa za ajira, kuporomoka kwa tunu msingi za familia na wimbi kubwa la wakimbizi!

Askofu Flavian Matindi Kassala wa Jimbo Katoliki Geita anasema, familia ni kitovu cha malezi ya kiutu, kijamii na maisha ya kiroho.

Askofu Flavian Matindi Kassala wa Jimbo Katoliki Geita anasema, familia ni kitovu cha malezi na majiundo ya kiutu, maisha ya kiroho na kitamaduni.

Askofu Kassala: familia ni chemchemi ya malezi na majiundo ya kiutu

19/05/2018 14:10

Familia ni Kanisa dogo la nyumbani, shule ya utakatifu, haki, amani, upendo na maridhiano. Ni mahali pa kwanza kabisa pa kukuza na kudumisha tunu msingi za maisha ya kiutu, maisha ya kiroho, kijamii na kitamaduni. Familia ni mahali pa kutakatifuzana katika ndoa! Ni shule ya huruma na upendo.

 

Baba Mtakatifu Francisko katika Wosia wake wa kitume, Furaha ya Injili anapembua magonjwa ya maisha ya kiroho.

Baba Mtakatifu Francisko katika Wosia wake wa kitume Furaha ya Injili anapembua kwa kina na mapana magonjwa ya maisha ya kiroho yanayoweza kukwamisha maisha na utume wa Kanisa.

Papa Francisko anadadavua magonjwa ya maisha ya kiroho!

12/05/2018 07:34

Baba Mtakatifu Francisko katika Wosia wake wa kitume "Evangelium gaudium" yaani "Furaha ya Injili" anachambua kwa kina na mapana magonjwa ya maisha ya kiroho yanayoweza kumdumaza mwamini kiasi cha kushindwa kuzaa matunda yanayokusudiwa na hivyo kukwamisha maisha na utume wa Kanisa.