Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Injili ya Amani

Papa Francisko wakati akirejea kutoka Colombia amepata nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari waliokuwa kwenye msafara wake.

Papa Francisko wakati akirejea mjini Vatican kutoka kwenye hija yake ya kitume nchini Colombia amepata nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari waliokuwa kwenye msafara wake.

Papa Francisko achonga na waandishi wa habari wakati akirejea Vatican

12/09/2017 09:49

Baba Mtakatifu Francisko wakati akirejea mjini Vatican amepata bahari ya kuzungumza na waandishi wa habari kwa kukazia umuhimu wa kuwapokea na kuwatunza wakibizi na wahamiaji; athari za mabadiliko ya tabianchi za wajibu wa kimaadili; misingi ya haki, amani na upatanisho na utume kwa vijana!

Waamini wanahamasishwa na Mama Kanisa kujikosoa, kukosoana na hatimaye kujipatanisha na Mungu ili kuonja ukuu wa huruma yake!

Waamini wanahamasishwa na Mama Kanisa kujikosoa, kukosoana katika upendo na udugu, ili hatimaye, kujipatanisha na Mwenyezi Mungu ili kuonja ukuu wa huruma na upendo wake usiokuwa na kifani!

Umuhimu wa kukosoana kidugu!

06/09/2017 15:44

Kukosa na kukoseana ni jambo la kawaida katika maisha ya mwanadamu, lakini kusamehe na kupatana ni njia inayomwelekeza mwamini katika utimilifu wa maisha! Baba Mtakatifu Francisko anakazia umuhimu wa Sakramenti ya Upatanisho inayomwezesha mwamini kugusa ukubwa wa huruma ya Mungu!

 

Baba Mtakatifu katika ujumbe wake wa video kwa watu wa Colombia anasema, Ninakuja kama muhujaji wa matumaini na amani kuadhimisha na ninyi imani

Baba Mtakatifu katika ujumbe wake wa video kwa watu wa Colombia anasema, Ninakuja kama muhujaji wa matumaini na amani kuadhimisha na ninyi imani katika Bwana

Papa Francisko: Ninakuja kwenu kama mjumbe wa amani na matumaini!

05/09/2017 15:21

Baba Mtakatifu Francisko kuanzia tare 6 hadi tarehe 11 Septemba 2017 anafanya hija ya kitume nchini Colombia inayoongozwa na kauli mbiu "Tupige hatua ya kwanza" inayowahimiza wananchi wa Colombia kujenga madaraja ya majadiliano, haki, amani, udugu na umoja wa kitaifa kwa ajili ya mafao ya wengi!

 

Upatanisho: Mapadre 40 waliuwawa kati ya mwaka 1987 hadi mwaka 2003; Makanisa 63 kuchomwa moto katika kipindi hiki.

Upatanisho: Mapadre 40 waliuwawa nchini Colombia kati ya Mwaka 1987 hadi mwaka 2004; Makanisa 63 kuchomwa moto.

Mada zinazoongoza hija ya kitume ya Papa Francisko nchini Colombia!

05/09/2017 12:26

Baraza la Maaskofu Katoliki Colombia linasema, hija ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Colombia inaongozwa na mada zifuatazo: Upatanisho, haki na amani; Injili ya uhai na familia; Ufuasi, Umisionari na utume unaowasukuma Wakristo kuwa ni vyombo na mashuhuda wa uinjilishaji wa kina!

Waamini wana hamasishwa na Mama Kanisa kushikamana na Kristo Yesu katika maisha yao, kamwe wasijitafute wenyewe na kusahau uwepo wa Kristo!

Waamini wana hamasishwa na Mama Kanisa kujishakamanisha na Kristo Yesu katika hija ya maisha yao na kamwe wasijitafute wenyewe watazama ndani ya tumbo la maji kama risasi.

Usiposhikamana na Kristo Yesu, utazama kama jiwe majini!

09/08/2017 13:23

Tafakari ya Neno la Mungu, Jumapili ya XIX ya Mwaka A wa Kanisa ni mwaliko kwa waamini kujishikamanisha na Kristo Yesu, aliye njia, ukweli na uzima! Pale wanaposhindwa kumwambata Kristo, watazama majini na kutoweka kama ndoto ya mchana! Kwa kushikamana na Yesu, amani inapatikana!

Watu wana kiu ya haki, amani na upatanisho na wala si vita!

Watu wana kiu ya haki, amani na upatanisho na wala si vita!

Watu wana kiu ya amani duniani!

05/08/2017 17:36

Baraza la Maaskofu Katoliki Japan linasema, familia ya Mungu duniani ina kiu ya amani ya kweli na endelevu  na wala si vita, ghasia na mipasuko ya kijamii. Kumbe, waamini wanahamasishwa kuwa kweli ni mashuhuda na vyombo vya Injili ya amani duniani, kwani vita ni chanzo cha maafa ya binadamu!

Papa Francisko anawataka wadau wa tasnia ya mawasiliano ya jamii kuwa ni vyombo vya amani duniani.

Papa Francisko anawataka wadau wa tasnia ya habari duniani kuwa ni vyombo vya amani kwa kujikita katika ukweli na kuondokana na "fake news" yaani habari zilizochakachuliwa!

Wanahabari iweni vyombo na mashuhuda wa Injili ya amani duniani!

19/06/2017 14:05

Baba Mtakatifu Francisko anawaalika wadau wa tasnia ya habari ulimwengu kuwa kweli ni vyombo na mashuhuda wa Injili ya haki, amani, upendo na maridhiano kati ya watu kwa kuhakikisha kwamba, wanasimamia na kutangaza ukweli badala ya kukazia "habari zilizochakachuliwa" hatari kwa amani.

Pentekoste ni siku ya kuzaliwa kwa Kanisa, siku ambayo mitume walitoka kimasomaso kutangaza na kushuhudia kuhusu: mateso, kifo na ufufuko wa Yesu.

Pentekoste ni siku ya kuzaliwa kwa Kanisa, siku ambayo Mitume walishukiwa na Roho Mtakatifu, wakatoka kimasomaso kutangaza na kushuhudia kwamba, Kristo Yesu aliyeteswa, akafa amefufuka kwa wafu! Hiki ni kiini cha imani na matumaini ya Kanisa.

Siku kuu ya Pentekoste, Siku ya kuzaliwa kwa Kanisa!

01/06/2017 14:40

Pentekoste ni Siku ambayo Kanisa linaadhimishwa kuzaliwa kwake kwa njia ya Roho Mtakatifu kuwashukia Mitume na hivyo kuwapatia nguvu, ujasiri, ari na moyo mkuu wa kuweza kutoka kifua mbele kutangaza na kushuhudia kwamba, Yesu aliyeteswa, akafa, akafufuka amepaa mbinguni! Kiini cha imani yetu!