Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Heri za Mlimani

Papa Francisko anawataka wakleri kuachana na tabia ya kupinga kila jambo; kujenga mahusiano mema na watu na kumwilisha huduma katika uhalisia wa watu.

Papa Francisko anawataka wakleri kuachana na tabia ya kupinga kila jambo, kujenga mahusiano mema na watu wanaowahudumia pamoja na kuhakikisha kwamba, huduma za kiroho zinamwilishwa katika uhalisia wa maisha ya watu.

Padre Primo Mazzolari, alikuwa ni Baba wa maskini na waliotelekezwa!

20/06/2017 16:48

Baba Mtakatifu Francisko anapenda kuwaonya Mapadre kuachana na tabia ya kupinga kila jambo linalojitokeza mbele yao! Kuepuka tabia ya kufanya kazi nyingi bila kujenga mahusiano mema na watu wanaowahudumia; tatu washughulikie mambo ya kiroho kwa kushuka katika uhalisia wa maisha ya watu!

 

Siku ya Maskini Duniani Kwa Mwaka 2017: " Kauli mbiu: Tusipende kwa neno bali kwa tende"

Siku ya Maskini Duniani Kwa Mwaka 2017: Kauli mbiu " Tusipende kwa neno bali kwa tendo".

Ujumbe wa Papa Francisko kwa Siku ya Kwanza ya Maskini Duniani 2017

13/06/2017 15:34

Siku ya kwanza ya Maskini Duniani iliyoanzishwa na Baba Mtakatifu Francisko kama sehemu ya mwendelezo wa maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu itaadhimishwa hapo tarehe 19 Novemba 2017. Kauli mbiu "Tusipende kwa neno bali kwa tendo".

Papa Francisko anawaalika waamini kuwa ni mashuhuda na vyombo vya faraja na huduma ya Mungu kwa jirani zao!

Papa Francisko anawaalika waamini kuwa ni mashuhuda na vyombo vya faraja na huduma ya Mungu kwa jirani zao!

Waamini wanahamasishwa kuwa ni vyombo vya faraja na huduma kwa jirani

12/06/2017 15:55

Baba Mtakatifu Francisko anawataka waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kuwa ni vyombo na mashuhuda wa faraja na huduma kwa maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii kwa kujikita katika Heri za Mlimani, muhtasari wa Mafundisho Makuu ya Yesu!

Mapadre onesheni na kushuhudia utakatifu wa maisha kwa njia ya huduma makini kwa watu!

Mapadre onesheni na kushuhudia utakatifu wa maisha kwa njia ya huduma makini, maisha ya sala, na maadhimisho ya mambo matakatifu.

Kardinali Stella, toeni harufu nzuri ya utakatifu wa maisha kila siku!

21/04/2017 13:16

Mama Kanisa anapenda kuwahamasisha waamini wote, lakini zaidi wakleri kuhakikisha kwamba, kila siku ya maisha yao inapaswa kwa ushuhuda wa utakatifu wa maisha unaojikita katika sala, tafakari ya kina ya Neno la Mungu, huduma na uwajibikaji makini pamoja na maadhimisho ya Sakramenti!

 

Hata katika shida na changamoto za maisha, Wakristo wanahamasishwa kuwa waamini kwa Kristo na Kanisa!

Hata katika shida na mahangaiko, dhuluma na nyanyaso, wakristo wanahamasishwa kusimama kidete kulinda, kutetea na kushuhudia imani yao.

Hata katika madhulumu, Wakristo wanaitwa kuwa waaminifu kwa Kristo!

14/04/2017 17:06

Mashambulizi ya kigaidi, misimamo mikali ya kiimani, dhuluma na nyanyaso dhidi ya Wakristo ni kati ya changamoto pevu katika ulimwengu mamboleo! Wakristo pia wanahamasishwa kuendelea kuwa waamini kwa Kristo na Kanisa lake hata wanapokumbana na changamoto za maisha kama ilivyo kwa sasa.

 

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana ametafakari kuhusu Heri za Mlimani muhtasari wa mafundisho makuu ya Kristo.

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana ametafakari kuhusu Heri za Mlimani, muhtasari wa Mafundisho makuu ya Yesu kwenye Agano Jipya.

Heri za Mlimani ni dira na mwongozo wa maisha ya Kikristo!

29/01/2017 14:09

Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana amefafanua kwa kina na mapana maana ya Heri za Mlimani ambazo ni muhtasari wa Mafundisho Makuu ya Yesu katika Agano Jipya na kuwataka waamini kuzimwilisha katika uhalisia wa maisha yao kama sehemu ya safari ya maisha!

Waamini wanahamasishwa na Mama Kanisa kuzitafakari na hatimaye kuzimwilisha heri za mlimani katika maisha yao kwani ni dira na mwongozo wa Kikristo!

Waamini wanahamasishwa na Mama Kanisa kuhakikisha kwamba, wanazitafakari na hatimaye, kuzimwilisha Heri za Mlimani katika maisha yao kwani huu ni muhtasari wa Mafundisho Makuu ya Kristo Yesu.

Heri za Mlimani zinavyochambuliwa kama karanga!

28/01/2017 14:29

Waswahili wanasema, eti kufa kunoga! Leo, Padre Alcuin Nyirenda, OSB anachambua kwa kina na mapana maana ya Heri za Mlimani, ambazo kimsingi ni muhtasari wa mafundisho makuu ya Yesu yanayoweza kuwasaidia katika mchakato wa kufikia furaha ya uzima wa milele! Jitaabishe kuzitafakari zaidi!

 

Waamini wanahitaji kujivika paji la unyenyekevu kutambua ukuu wa Mungu, ili kuumwilisha katika upendo kwa jirani!

Waamini wanahitaji kujivika paji la unyenyekevu ili kutambua ukuu wa Mungu unaomwilishwa katika upendo kwa jirani!

Hofu ya Mungu ni ufupisho makini wa heri za mlimani!

26/01/2017 11:56

Heri za Mlimani ambacho ni kiini cha Liturujia ya Neno la Mungu, Jumapili IV ya Kipindi cha Mwaka A wa Kanisa ni zinaweza kufupishwa kwa kushuhudia hofu ya Mungu na upendo kwa jirani kama kielelezo makini cha dira na mwongozo wa maisha ya Kikristo hapa duniani! Haya ni madundisho makuu ya Yesu.