Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Hazina: uvumba, Manemane na Dhahabu

Kardinali Polycarp Pengo anawataka waamini lakini zaidi wakleri kutekeleza mapenzi ya Mungu katika maisha na utume wao.

Kardinali Polycarp Pengo anawataka waamini, lakini zaidi wakleri kutekeleza mapenzi ya Mungu katika maisha yao.

Kardinali Pengo: Jitahidini kutekeleza mapenzi ya Mungu katika maisha

11/01/2018 16:35

Kardinali Polycarp Pengo, Askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam anawataka waamini, lakini kwa namna ya pekee kabisa Wakleri kuhakikisha kwamba, wanajitahidi kutekeleza mapenzi ya Mungu katika maisha na utume wao, vinginevyo wanaweza kujikuta wakiogelea kwenye dimbwi la maafa!

 

Papa Francisko: Sherehe ya Tokeo la Bwana iwe ni fursa ya kutembea, kuinua macho juu angani na kumtolea Mungu hazina kwa njia ya matendo ya huruma.

Papa Francisko: Sherehe ya Tokeo la Bwana ni fursa kwa waamini kutembea, kuinua macho yao angani na kumtolea Mungu hazina ya maisha yao kwa njia ya matendo ya huruma.

Papa: Sherehe ya Tokeo la Bwana: Kuona nyota, kutembea na kutoa hazina

06/01/2018 12:00

Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri yake wakati wa maadhimisho ya Sherehe ya Tokeo la Bwana, maarufu kama Epifania, amewataka waamini kujitahidi kuina nyota ya Mtoto Yesu katika maisha yao, kuifuata kwa kuthubutu kutembea na kumtolea hazina inayofumbatwa katika matendo ya huruma.

Sherehe ya Tokeo la Bwana, maarufu kama Epifania ni ufunuo wa Kristo Yesu: Mwanga wa Mataifa, Mfalme na Mkombozi wa ulimwengu.

Sherehe ya Tokeo la Bwana, maarufu kama Epifania ni ufunuo wa Kristo Yesu kama Mwanga wa Mataifa, Mfalme na Mkombozi wa Ulimwengu.

Kristo Yesu ni Mwanga wa Mataifa, Mfalme na Mkombozi wa Ulimwengu

05/01/2018 06:45

Maadhimisho ya Liturujia ya Sherehe ya Tokeo la Bwana ni ufunuo wa Kristo Yesu, Mwanga wa Mataifa, Mfalme na Mkombozi wa ulimwengu; dhamana na utume wake unaojionesha hasa kwenye hazina ambayo Mamajusi kutoka Mashariki ya mbali walimtolea Mtoto Yesu: Dhahabu, Uvumba na Manemane!

Sherehe ya Tokeo la Bwana ni Siku kuu ya Kristo Mwanga unaofunuliwa kwa watu wa Mataifa!

Sherehe ya Tokeo la Bwana ni Siku kuu ya Mwaga, ambao ni Kristo anayejifunua kwa watu wa Mataifa.

Sherehe ya Tokeo la Bwana ni Siku kuu ya ufunuo wa mwanga wa Kristo!

03/01/2018 14:24

Yesu Kristo ni Mwanga wa Mataifa unaofunuliwa kwa watu wa mataifa yote wanaowakilishwa na Mamajusi kutoka Mashariki ya mbali, ni watu wa mazingira na dini ya kipagani, lakini wanaifuata Nyota ya Daudi, Mfalme wa Mataifa, Mwana wa Mungu na Mkombozi wa Ulimwengu. Epifania ni sherehe ya umoja!

 

Sherehe ya Tokeo la Bwana: Zawadi: Ubani, dhahabu na manemane yaani: Umungu, Ufalme na Ubinadamu wa Kristo Yesu.

Sherehe ya Tokeo la Bwana: Zawadi: Ubani, Dhahabu na Manemane maana yake ni: Umungu, Ufalme na Ubinadamu wa Kristo Yesu, Mwanga wa Mataifa.

Sherehe ya Tokeo la Bwana! Kristo Yesu ni Mwanga wa Mataifa!

02/01/2018 13:49

Mamajusi kutoka Mashariki ya mbali huku wakiongozwa na nyota walifika mjini Bethlehemu, wakamsujudu Bwana na kumtolea zawadi kuu tatu zinazofafanua maana na utume wa Kristo Yesu: Ubani ni Umungu wa Kristo; Dhahabu: Ufalme wa Kristo na Manemane ni Ubinadamu wa Kristo utakaopambana na kifo!

Imani ya Kanisa kuhusu Yesu Mwana wa Mungu aliye hai imesimikwa katika Mwamba thabiti wa ushuhuda wa Mitume wa Yesu.

Imani ya Kanisa kuhusu Yesu Mwana wa Mungu aliye hai imesimikwa katika mwamba thabiti wa ushuhuda na mafundisho ya Mitume wa Yesu.

Imani ya Kanisa inasimikwa katika ushuhuda makini wa Mitume wa Yesu

26/08/2017 07:00

Kanuni ya Imani ni muhtasari wa Mafundisho makuu ya Mama Kanisa kwa watoto wake kuhusu: Fumbo la Utatu Mtakatifu; Kanisa na Mambo ya Nyakati. Hii ni imani ambayo imesimikwa katika ushuhuda na mafundisho ya Mitume wa Yesu, changamoto kwa Wakristo kuwa kweli ni mashuhuda amini!

Kristo Yesu na Ufalme wa Mungu ndizo hazina zilizofichika zinazohitaji uwekezaji na wa hali ya juu, hekima na busara kuweza kuzipata.

Kristo Yesu na Ufalme wa Mungu ndizo hazina zilizofichika zinazohitaji uwekezaji wa hali ya juu kuweza kuzipata kwa kutumia hekima na busara kufanya maamuzi mazito.

Hazina iliyofichika ni: Ufalme wa Mungu na Kristo Yesu!

29/07/2017 09:36

Liturujia ya Neno la Mungu, Jumapili ya XVII ya Kipindi cha Mwaka A wa Kanisa kwa ufupi inatujuza kwamba, hazina iliyofichika inayopaswa kutolewa maamuzi mazito, makini na yenye busara kiasi cha kujisadaka ni Ufalme wa Mungu na Kristo Yesu aliyeufunua kwa njia ya ushuhuda wa maisha!

Kristo Yesu ni hekima na hazina iliyofika, dira na mwongozo wa maisha katika kufikiri na kutenda

Kristo Yesu ni hekima ya Mungu iliyomwilishwa na hazina iliyofichika, dira na mwongozo katika kufikiri na kutenda!

Hekima ya Mungu ni dira na mwongozo katika kufikiri na kutenda mema!

26/07/2017 16:03

Liturujia ya Neno la Mungu, Jumapili ya XVII ya Mwaka A wa Kanisa inatoa mwaliko kwa waamini kuitafuta na kuiambata hekima ya Mungu ili iweze kuwasaidia kufikiri na kutenda vyema. Hekima iliyofichika inayopaswa kutafutwa kwa udi na uvumba ni Kristo Yesu, Mwana wa Mungu aliye hai!