Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

fursa za kazi

Papa Francisko asema, vyama vya wafanyakazi vinapaswa kulinda na kutetea haki msingi za wafanyakazi na kuwa ni sauti ya wanyonge.

Papa Francisko asema, vyama vya wafanyakazi vinapaswa kusimama kidete kulinda, kutetea na kudumisha haki msingi za wafanyakazi na kuendelea kuwa ni sauti ya wanyonge ndani ya jamii.

Vyama vya wafanyakazi visimame kidete kutetea haki za wafanyakazi!

30/06/2017 07:43

Baba Mtakatifu Francisko anasema vyama vya wafanyakazi vina wito na dhamana muhimu sana kwani vinapaswa kusimama kidete kulinda, kutetea na kudumisha haki msingi za wafanyakazi! Vinapaswa kuwa ni sauti ya wanyonge, lakini vikiendekeza rushwa na ufisadi, vitakuwa ni kikwazo cha haki!

Ukosefu wa fursa za ajira unapelekea vijana wengi kuzikimbia nchi zao ili kutafuta maisha bora zaidi!

Ukosefu wa fursa za ajira unapelekea vijana wengi kuzikimbia nchi zao ili kutafuta fursa bora zaidi za maisha.

Ajira bado ni kizungumkuti duniani, waathirika zaidi ni vijana!

14/06/2017 07:47

Askofu mkuu Ivan Jurkovic, Mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizoko mjini Geneva anasema, ukosefu wa fursa za ajira unapelekea vijana wa kizazi kipya kukata tamaa ya maisha kiasi cha kujikuta wanajiingiza kwenye mchakato wa kutafuta fursa bora zaidi za maisha!

Papa Francisko asema, Kanisa litaendelea kushirikiana na Serikali ya Italia kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi!

Papa Francisko asema, Kanisa litaendelea kushirikiana na kushikamana na Serikali ya Italia kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi.

Vatican kuendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali ya Italia!

10/06/2017 15:46

Baba Mtakatifu Francisko anasema, changamoto zinazoikabili Italia kwa sasa zinapaswa kushughulikiwa kwa njia ya ushirikiano na mshikamano na wote, ili kuwajengea vijana matumaini ya leo na kesho iliyo bora zaidi; kwa kujikita katika utajiri na amana za maisha ya kiroho na kiutu nchini Italia.

Utu, heshima, haki msingi za binadamu na uchumi shirikishi ni mambo msingi katika mafundisho jamii ya Kanisa.

Utu, heshima, haki msingi za binadamu ni kati ya mambo msingi yanayopewa kipaumbele cha pekee katika Mafundisho Jamii ya Kanisa.

Papa: ajira, utu na heshima ya binadamu ni muhimu katika uchumi

28/05/2017 14:47

Baba Mtakatifu Francisko anasema, mafundisho Jamii ya Kanisa yamekuwa yakitoa kipaumbele cha pekee kwa utu, heshima ya binadamu pamoja na haki zake msingi kama vigemo muhimu sana katika sera na mikakati ya uchumi shirikishi ili kutengeneza fursa za ajira, kielelezo cha utimilifu wa utu wa mtu!

Hija ya kitume ya Papa Francisko nchini Misri imewasha moto wa mapambazuko ya ubinadamu mpya unaojikita katika majadiliano ya kidini na kiekumene.

Hija ya kitume ya Papa Francisko nchini Misri imewasha moto wa mapambazuko ya ubinadamu mpya unaojikita katika mchakato wa majadiliano ya kidini na kiekumene ili kudumisha: utu, heshima, ustawi na maendeleo ya wengi.

Cheche za Mapambazuko Mapya ya Ubinadamu zawashwa nchini Misri!

08/05/2017 07:20

Hija ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Misri hivi karibuni, imewasha moto wa mapambazuko ya ubinadamu mpya unaosimikwa katika majadiliano ya kidini na kiekumene ili kujenga na kudumisha: utu, heshima, ustawi na maendeleo ya wengi huko Mashariki ya kati! Hii ni changamoto kubwa.

CEI: Kazi tunayohitaji izingatie: uhuru, ubinifu, ushirikiano na mshikamano

CEI: Kazi tunayohitaji izingatie: uhuru, ubunifu, ushirikiano na mshikamano!

Juma la Kijamii nchini Italia: Uhuru, Ubunifu, Umoja na Mshikamano

01/05/2017 13:30

Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, kuanzia tarehe 26 - 29 Oktoba 2017 linaadhimisha Juma la Kijamii nchini Italia kwa kuongozwa na kauli mbiu: "Kazi tunayohitaji: ni ile inayofanywa kwa uhuru, kwa ubunifu kwa kushirikiana pamoja na kushikamana na wengine". Kazi ni sehemu ya maandalizi haya!

RECOWA-CERAO: changamoto kubwa: hali tete ya kisiasa; misimamo mikali ya kidini na majanga asilia.

RECOWA-CERAO: changamoto kubwa: hali tete ya kisiasa, kiuchumi na kijamii; misimamo mikali ya kidini na kiimani pamoja na athari za majanga asilia.

RECOWA-CERAO na changamoto zake Afrika Magharibi!

19/04/2017 11:12

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Magharibi linasema, linapenda kushirikiana kwa dhati na Jumuiya ya Uchumi Afrika Magharibi,ECOWAS ili kukabiliana na changamoto zinazoendelea kujitokeza katika Nchi wanachama wa RECOWA-CERAO hasa: vitendo ya kigaidi na misimamo mikali ya kidini

Askofu Mkuu Auza anasema ni jambo linalopaswa kuwa muhimu hasa la kazi ya mwanamke katika  kutunza familia,ni zawadi,ni asili yake kusaidia wengine

Askofu Mkuu Auza anasema,ni jambo linalopaswa kuwa muhimu hasa la kazi ya mwanamke katika kutunza familia,ni zawadi,ni asili ya mwanamke kuwasaidia wengine

Nafasi ya mwanamke katika ulimwengu wa kazi ni nguzo isiyoonekana!

18/03/2017 14:57

Wanawake wengi ni kama sanaa nzuri ya mawe yaliyojipanga,katika ulimwengu unao badilika.kwa upande wa ajira ya hakuna mfumo wa kijamii wa kuwalinda wanawake,hata kuhamasisha kwasababu wengi ni waathirika wa kukosa usawa na wanaume hata kama wote wanafanya kazi katika sehemu moja