Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

fursa za ajira

Taarifa zinaonesha kwamba, kuna wakimbizi na wahamiaji ambao kwa sasa wanazamishwa baharini ili kufuta ushahidi dhidi ya wafanya biashara ya binadamu!

Taarifa zinaonesha kwamba, kuna wakimbizi na wahamiaji wanaozamishwa baharini ili kufuta ushahidi dhidi ya wafanyabiashara ya binadamu!

Changamoto mamboleo: fursa za ajira na huduma makini kwa wakimbizi!

11/08/2017 13:45

Baraza la Maaskofu Katoliki Italia linasema, kwa sasa changamoto kubwa inayoikabilia Jumuiya ya Kimataifa ni fursa za ajira kwa wafanyakazi, ili waweze kutekeleza dhamana na wajibu wao barabara sanjari na huduma makini kwa wakimbizi na wahamiaji wanaotafuta: usalama, hifadhi na maisha bora zaidi.

Utalii endelevu ni chombo cha maendeleo!

Utalii endelevu ni chombo cha maendeleo!

Siku ya Utalii Duniani 2017: Utalii endelevu ni chombo cha maendeleo

02/08/2017 14:55

Kardinali Peter Turkson anasema, sekta ya utalii ina umuhimu mkubwa sana katika ustawi na maendeleo ya watu. Ni sekta inayochangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi; utamaduni na maisha ya kijamii; utalii endelevu ni kikolezo kikubwa cha maendeleo endelevu ya binadamu!

Papa Francisko asema, vyama vya wafanyakazi vinapaswa kulinda na kutetea haki msingi za wafanyakazi na kuwa ni sauti ya wanyonge.

Papa Francisko asema, vyama vya wafanyakazi vinapaswa kusimama kidete kulinda, kutetea na kudumisha haki msingi za wafanyakazi na kuendelea kuwa ni sauti ya wanyonge ndani ya jamii.

Vyama vya wafanyakazi visimame kidete kutetea haki za wafanyakazi!

30/06/2017 07:43

Baba Mtakatifu Francisko anasema vyama vya wafanyakazi vina wito na dhamana muhimu sana kwani vinapaswa kusimama kidete kulinda, kutetea na kudumisha haki msingi za wafanyakazi! Vinapaswa kuwa ni sauti ya wanyonge, lakini vikiendekeza rushwa na ufisadi, vitakuwa ni kikwazo cha haki!

Ukosefu wa fursa za ajira unapelekea vijana wengi kuzikimbia nchi zao ili kutafuta maisha bora zaidi!

Ukosefu wa fursa za ajira unapelekea vijana wengi kuzikimbia nchi zao ili kutafuta fursa bora zaidi za maisha.

Ajira bado ni kizungumkuti duniani, waathirika zaidi ni vijana!

14/06/2017 07:47

Askofu mkuu Ivan Jurkovic, Mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizoko mjini Geneva anasema, ukosefu wa fursa za ajira unapelekea vijana wa kizazi kipya kukata tamaa ya maisha kiasi cha kujikuta wanajiingiza kwenye mchakato wa kutafuta fursa bora zaidi za maisha!

Papa Francisko asema, Kanisa litaendelea kushirikiana na Serikali ya Italia kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi!

Papa Francisko asema, Kanisa litaendelea kushirikiana na kushikamana na Serikali ya Italia kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi.

Vatican kuendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali ya Italia!

10/06/2017 15:46

Baba Mtakatifu Francisko anasema, changamoto zinazoikabili Italia kwa sasa zinapaswa kushughulikiwa kwa njia ya ushirikiano na mshikamano na wote, ili kuwajengea vijana matumaini ya leo na kesho iliyo bora zaidi; kwa kujikita katika utajiri na amana za maisha ya kiroho na kiutu nchini Italia.

Utu, heshima, haki msingi za binadamu na uchumi shirikishi ni mambo msingi katika mafundisho jamii ya Kanisa.

Utu, heshima, haki msingi za binadamu ni kati ya mambo msingi yanayopewa kipaumbele cha pekee katika Mafundisho Jamii ya Kanisa.

Papa: ajira, utu na heshima ya binadamu ni muhimu katika uchumi

28/05/2017 14:47

Baba Mtakatifu Francisko anasema, mafundisho Jamii ya Kanisa yamekuwa yakitoa kipaumbele cha pekee kwa utu, heshima ya binadamu pamoja na haki zake msingi kama vigemo muhimu sana katika sera na mikakati ya uchumi shirikishi ili kutengeneza fursa za ajira, kielelezo cha utimilifu wa utu wa mtu!

Papa Francisko tarehe 10 Juni 2017 anatembelea Ikulu ya Italia ili kukutana na kuzungumza na Rais Mattarella wa Italia.

Papa Francisko tarehe 10 Juni 2017 anatarajia kukutana na kuzungumza na Rais Sergio Mattarella wa Italia.

Papa Francisko kutembelea Ikulu ya Italia tarehe 10 Juni 2017

16/05/2017 09:29

Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa hapo tarehe 10 Juni 2017 kutembelea rasmi Ikulu ya Italia ili kukutana na kuzungumza na Rais Sergio Mattarella wa Italia kama njia ya kukuza na kudumisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Italia na Vatican na kuendeleza ushirikiano wa kitaifa na kimataifa.

Askofu A.Gabuza Rais wa Tume ya Haki na Amani Afrika ya Kusini anasema ukosefu wa ajira kwa vijana ni hatari

vijana wengi wasio kuwa na ajira wako hatarini: waathirika wa madawa ya kulevya, biashara ya binadamu, kujiingiza katika vitendo vya kialifu, vilevile kudanganywa na baadhi ya wanasiasa wasio kuwa na huruma

A.Kusini: Inahitajika mabadiliko ya uchumi kwa ajili ya vijana

09/05/2017 13:48

 Askofu A.Gabuza wa Afrika ya Kusini anasema; ni mabadiliko makubwa ya kiuchumi yanayoweza kutatua janga la ukosefu wa ajira kwa vijana, lakini  kwa bahati mbaya,utamaduni wa sasa wa uongozi umetanda mizizi  katika ufisadi na hauna uwezo kimaadili katika ukufanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi