Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Furaha ya Injili

Furaha ni pumzi ya kikristo ni furaha ambayo inatokana na amani ya moyo na siyo unafiki kama vile utolewavyo  na utamaduni wa kisasa kwa kuunda anasa

Furaha ni pumzi ya kikristo ni furaha ambayo inatokana na amani ya moyo na siyo unafiki kama vile utolewavyo na utamaduni wa kisasa kwa kuunda mambo mengi ya kujifurahisha na anasa

Pumzi ya Kikristo ni furaha itokanayo na tunda la Roho Mtakatifu!

28/05/2018 14:13

Kwa mujbu wa Papa Francisko,furaha ya kikristo ni pumzi ya mkristo.Mkristo hasiye kuwa na furaha katika moyo wake siyo mkristo.Pumzi ya mkristo inajionesha katika furaha,maana siyo jambo linalonunuliwa au kufanya nguvu yoyote, bali ni tunda la Roho Mtakatifu anayefanya moyo uwe na furaha.

 

Patriaki Bartolomeo wa kwanza anasema, mafao ya wengi ni ajenda na kiekumene!

Patriaki Bartolomeo wa kwanza anasema, mafao ya wengi ni ajenda ya kiekumene.

Patriaki Bartolomeo wa kwanza: Mafao ya wengi ni ajenda ya kiekumene

26/05/2018 14:55

Patriaki Bartolomeo wa kwanza anasema, mafao ya wengi ni ajenda ya pamoja kwa wakristo wote ili kusaidia maboresho katika sekta ya uchumi na ekolojia; sayansi na teknolojia; jamii na siasa; kwa kusimama kidete: kulinda na kutetea utu, heshima, ustawi, maendeleo na mafao ya wengi!

Baba Mtakatifu Francisko katika Wosia wake wa kitume, Furaha ya Injili anapembua magonjwa ya maisha ya kiroho.

Baba Mtakatifu Francisko katika Wosia wake wa kitume Furaha ya Injili anapembua kwa kina na mapana magonjwa ya maisha ya kiroho yanayoweza kukwamisha maisha na utume wa Kanisa.

Papa Francisko anadadavua magonjwa ya maisha ya kiroho!

12/05/2018 07:34

Baba Mtakatifu Francisko katika Wosia wake wa kitume "Evangelium gaudium" yaani "Furaha ya Injili" anachambua kwa kina na mapana magonjwa ya maisha ya kiroho yanayoweza kumdumaza mwamini kiasi cha kushindwa kuzaa matunda yanayokusudiwa na hivyo kukwamisha maisha na utume wa Kanisa.

Kristo Yesu ni chemchemi ya furaha ya kweli inayobubujika kutoka katika Amri za Mungu na upendo kwa jirani!

Kristo Yesu ni chemchemi ya furaha ya kweli inayobubujika kutoka katika Amri za Mungu na upendo wa dhati kwa jirani!

Yesu ni chemchemi ya furaha ya kweli inayofumbatwa katika upendo!

03/05/2018 07:00

Kristo Yesu ni chemchemi ya furaha ya kweli inayofumbatwa katika amri ya upendo unaomwilishwa kwa Mungu na jirani. Furaha hii inaendelea kukua na kuchipuka, ikiwa kama mwamini anajikita katika kutekeleza Amri za Mungu katika maisha yake kama dira na mwongozo wa maisha adili na matakatifu.

Papa Francisko amekutana katika ukumbi wa Papa Paulo VI, karibia vijana elfu tatu kutoka jimbo la Brescia nchini Italia

Papa Francisko amekutana katika ukumbi wa Papa Paulo VI, karibia vijana elfu tatu kutoka jimbo la Brescia nchini Italia

Papa na Vijana wa Brescia Italia:Jikane binafsi na kuvua utu wa zamani!

07/04/2018 16:00

 Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi  tarehe 7 Aprili 2018 amekutana na vijana kutoka Jimbo Katoliki  la Brescia nchini Italia  kwenye  Ukumbi wa Mwenyeheri Paulo VI.Amewaalika wamfuase Mungu wa upendo kwa kujikana binafsi na hasa kuvua kile kiitwacho katika Biblia,utu wa zamani. 

 

Papa amewatakia matashi mema ya Jumatatu ya Malaika mahujaji wote na kuwaomba wamkumbuke katika sala zao

Papa amewatakia matashi mema ya Jumatatu ya Malaika mahujaji wote na kuwaomba wamkumbuke katika sala zao.

Papa Francisko anawaombea wote hasa waliotekwa nyara ili warudi makwao!

02/04/2018 15:33

Ili kutosahau yale ambayo walikuwa wakisema wakristo wa kwanza:Bwana amefufuka kweli kweli.Nasi tutamke mara moja zaidi:Bwana amefufuka Kweli Kweli.Ni maneno ya Papa Francisko mara baada ya sala ya Malkia wa Mbingu,Jumatatu ya Pasaka, tarehe 2 Aprili 2018,akitoa  salamu zake

 

Papa Francisko anawataka Maaskofu wa Vietnam kuwa kati pamoja na watu wao, kwa kuinjilisha kwa furaha!

Papa Francisko anawataka Maaskofu wa Vietnam kuwa kati pamoja na watu wao ili kuinjilisha kwa njia ya furaha ya Injili.

Papa Francisko kwa Maaskofu wa Vietnam: Injilisheni kwa furaha!

06/03/2018 14:30

Baba Mtakatifu Francisko anawataka Maaskofu Katoliki kutoka Vietnam kuhakikisha kwamba, wanakuwa kati pamoja na watu wao kama kielelezo cha uinjilishaji mpya unaofumbatwa kwenye ushuhuda wa furaha ya Injili kama njia ya kukabiliana na changamoto mbali mbali wanazokumbana nazo!

Miujiza iliyotendwa na Kristo Yesu anasema Papa Francisko ilipania kuamsha imani, toba na wongofu wa ndani, kielelezo cha uwepo wa Ufalme wa Mungu!

Miujiza iliyotendwa na Kristo Yesu, ilipania kuamsha imani, toba na wongofu wa ndani, kielelezo makini cha uwepo wa Ufalme wa Mungu.

Papa asema, miujiza ya Yesu ilipania kuamsha imani, toba na wongofu

05/02/2018 08:14

Baba Mtakatifu Francisko anasema, kuna uhusiano mkubwa kati ya miujiza iliyotendwa na Kristo Yesu kwa watu walioteseka kwa magonjwa, udhaifu wa mwili na dhambi ili kuamsha tena ndani mwao imani, toba na wongofu wa ndani, kielelezo cha uwepo endelevu wa Ufalme wa Mungu kati ya watu wake!