Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Fumbo la Umwilisho

Fumbo la Msalaba ni ufunuo wa huruma, upendo, maisha mapya na wokovu kwa watu wote!

Fumbo la Msalaba ni ufunuo wa huruma, upendo, chemchemi ya maisha mapya na wokovu kwa watu wote!

Fumbo la Msalaba ni kielelezo cha: huruma, upendo na maisha mapya!

19/03/2018 09:54

Baba Mtakatifu Francisko anasema, Fumbo la Msalaba ni ufunuo wa mateso na kifo cha Mwana mpendwa wa Mungu, kielelezo cha hali ya juu kabisa cha upendo, chemchemi ya maisha mapya na wokovu kwa binadamu wa nyakati zote! Kwa njia ya Madonda yake Matakatifu watu wameponywa!

Mwanaume na mwanamke wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu na wanakamilisha katika maisha na wito wao!

Mwanaume na mwanamke wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu na wanakamilishana katika maisha na wito wao kwa kukuza na kudumisha tunu msingi za maisha ya ndoa na familia.

Mwanaume na mwanamke wanakamilishana kama sura na mfano wa Mungu

12/03/2018 12:15

Kardinali Marc Ouellet anasema, mwanaume na mwanamke kadiri ya mpango wa Mungu wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu ili kukamilishana. Kwa pamoja wanawajibika kukuza na kudumisha tunu msingi za maisha ya ndoa na familia ambazo kwa sasa zinakabiliwa na changamoto kubwa duniani!

Unyenyekevu wa wakristo ni fadhila inayowasaidia kukumbatia ukweli ili kujenga na kupyaisha jumuiya na Kanisa katika ujumla wake.

Unyenyekevu ni fadhila inayowawezesha wakristo kukumbatia ukweli unaopyaisha maisha ya jumuiya na Kanisa katika ujumla wake.

Unyenyekevu wa Kikristo unajenga na kupyaisha maisha na jumuiya!

09/03/2018 15:10

Padre Raniero Cantalamessa anasema fadhila ya unyenyekevu wa Kikristo ni gadhila inayofumbatwa katika ukweli na kiasi kama kielelezo cha hekima inayowawezesha wakristo kuanza mchakato wa kumkaribia Mwenyezi Mungu katika maisha yao kwani Mungu ni mwanga na ukweli wa maisha!

Papa: Watoto wanahitaji mashuhuda wa Injili ya matumaini ili kupambana na uharibifu mkubwa kwa mazingira nyumba ya wote!

Watoto wanahitaji mashuhuda wa Injili ya matumaini dhidi ya uharibifu wa mazingira nyumba ya wote!

Papa Francisko: Watoto wanahitaji mashuhuda wa Injili ya matumaini

20/01/2018 11:54

Baba Mtakatifu Francisko anawataka wazazi, walezi na wadau mbali mbali wanaojisadaka kwa ajili ya huduma makini kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na hatarishi kuhakikisha kuwa, wanawezekeza zaidi katika sekta ya elimu itakayowasaidia kuheshimu mazingira, mila na desturi njema.

Kardinali Stella anawataka Wakleri kuwa kukesha katika: Sala, Sakramenti, Tafakari, Toba na Wongofu wa ndani!

Kardinali Stella anawataka wakleri kukesha katika: Sala, Sakramenti, Neno, Toba na Wongofu wa ndani kama ushuhuda wenye mvuto na mashiko katika maisha na utume wa Kipadre!

Kardinali Stella: Wakleri kesheni, msije mkajikuta mnamezwa na giza!

05/01/2018 09:46

Kardinali Stella anawaalika Wakleri kutoa kipaumbele cha kwanza kwa Kristo na Kanisa lake katika maisha na utume wao miongoni mwa familia ya Mungu. Wajitahidi kujenga na kudumisha uhusiano wao na Kristo Yesu kwa njia ya: Sala, Sakramenti, Tafakari, Toba na Wongofu wa ndani, ushuhuda amini!

Mambo makuu ya kuzingatia kwa Mwaka 2018: Matendo ya huruma; huduma kwa familia ya Mungu; haki, amani na maridhiano kati ya watu!

Mambo makuu ya kuzingatia kwa Mwaka 2018: Matendo ya huruma; huduma makini kwa familia ya Mungu pamoja na kudumisha mchakato wa haki, amani na maridhiano kati ya watu!

Kardinali Omella: mambo msingi ya kuzingatia kwa Mwaka 2018

04/01/2018 08:54

Kardinali Juan Josè Omella anasema, Mwaka 2018 unapaswa kupambwa na matendo ya huruma: kiroho na kimwili kama kielelezo cha imani tendaji; Kujenga na kuimarisha huduma na mafungamano ya kijamii pamoja na kujielekeza zaidi katika mchakato wa ujenzi wa haki, amani na maridhiano!

 

Sherehe ya Tokeo la Bwana ni Siku kuu ya Kristo Mwanga unaofunuliwa kwa watu wa Mataifa!

Sherehe ya Tokeo la Bwana ni Siku kuu ya Mwaga, ambao ni Kristo anayejifunua kwa watu wa Mataifa.

Sherehe ya Tokeo la Bwana ni Siku kuu ya ufunuo wa mwanga wa Kristo!

03/01/2018 14:24

Yesu Kristo ni Mwanga wa Mataifa unaofunuliwa kwa watu wa mataifa yote wanaowakilishwa na Mamajusi kutoka Mashariki ya mbali, ni watu wa mazingira na dini ya kipagani, lakini wanaifuata Nyota ya Daudi, Mfalme wa Mataifa, Mwana wa Mungu na Mkombozi wa Ulimwengu. Epifania ni sherehe ya umoja!

 

Vijana wanakumbushwa kwamba, wao ni mahujaji wanaopaswa kuwajibika katika mchakato wa kuleta mageuzi ulimwenguni.

Vijana wanakumbushwa kwamba, wao ni mahujaji hapa duniani wanaopaswa kuwajibika katika mchakato mzima wa mgeuzi hapa duniani, ili ulimwengu uweze kuwa ni mahali pazuri zaidi pa kuishi.

Wakristo ni mahujaji wanaopaswa kuwajibika kikamilifu katika maisha

31/12/2017 14:11

Vijana wanapaswa kuwa makini katika kila hatua ya maisha wanayopiga kama sehemu ya mchakato wa ukuaji na ukomavu katika maisha yao ya kiroho na kimwili, tayari kushiriki kikamilifu  katika mchakato wa maboresho ya ulimwengu huu ili uweze kuwa ni mahali pazuri zaidi pa kuishi!