Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Fumbo la Msalaba

Waamini wanaitwa na kutumwa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu inayofumbatwa katika toba, wongofu na utakatifu wa maisha.

Waamini wanaitwa na kutumwa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu inayosimikwa katika ushuhuda wa maisha, toba, wongofu wa ndani na utakatifu wa maisha!

Mnatumwa kuwa mashuhuda wa furaha ya Injili ya Kristo kwa Mataifa!

14/07/2018 06:58

Mababa wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican wanasema, ushuhuda wa Kikristo unafumbatwa katika uhalisia wa maisha na majadiliano katika nyanja mbali mbali za maisha ya mwanadamu. Ni ushuhuda wa upendo unaojikita katika toba na wongofu wa ndani kama chachu ya kuyatakatifuza malimwengu!

 

Utukufu wa Kanisa unafumbatwa katika Fumbo la Msalaba!

Utukufu wa Kanisa unafumbatwa katika Fumbo la Msalaba.

Papa Francisko: Utukufu wa Kanisa unafumbatwa katika Fumbo la Msalaba

29/06/2018 13:29

Baba Mtakatifu Francisko anasema, Kristo Yesu aliunganisha utukufu wa Kanisa na Fumbo la Msalaba kwa kuwataka wafuasi wake na Kanisa katika ujumla wake kujikita katika huduma makini inayofumbatwa katika huruma na mapendo; kwa kujisadaka bila ya kujibakiza pamoja na kuzamisha huduma kwa watu!

Papa Francisko anawataka Makardinali kuwa waaminifu kwa Kristo na Kanisa lake na hivyo kuwajibika kwa ajili ya utume wa Kanisa.

Papa Francisko anawataka Makardinali kuwajibika na kuendelea kuwa waaminifu kwa Kristo na Kanisa lake, ili kushiriki kikamilifu katika utume wa kutangaza Habari Njema ya Wokovu!

Makardinali dhamana yenu ni: Uaminifu, uwajibikaji na utume kwa Kanisa

29/06/2018 08:00

Toba na wongofu wa ndani, uwasaidie waamini kuondokana na dhambi pamoja na ubinafsi, ili kujikita katika uaminifu na uwajibikaji kwa kujisadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu kwa watu wa Mataifa! Makardinali wanao wajibu mkubwa zaidi!

Wakristo wanayo dhamana na utume wa kumwilisha Ari ya upendo kwa adui kwa njia ya sala, msamaha na upendo.

Wakristo wanayo dhamana na utume wa kumwilisha Amri mpya ya upendo kwa kuwapenda adui zao, kuwaombea na hatimaye kuwasamehe.

Papa Francisko asema: Msamaha, Sala na Upendo ni silaha dhidi ya adui

19/06/2018 14:17

Baba Mtakatifu Francisko anasema, Amri mpya iliyotangazwa na kushuhudiwa na Kristo Yesu ni Upendo kwa adui; mageuzi makubwa katika mtazamo wa maisha ya kikristo yanayofumbatwa katika msamaha wa kweli, sala na upendo wa dhati kama nyenzo msingi za kupambana na adui! Yesu ni mfano!

Kwa njia ya Fumbo la Msalaba, Kristo Yesu ameanzisha Ufalme wa Mungu hapa duniani.

Kwa njia ya Fumbo la Msalaba, Kristo Yesu ameanzisha Ufalme wa Mungu hapa duniani na wote wanaalikwa kushiriki kikamilifu.

Ufalme wa Mungu unapata utimilifu wake katika Fumbo la Pasaka!

16/06/2018 06:30

Kristo Yesu kwa kutimiza mapenzi ya Baba yake wa mbinguni, ameanzisha duniani ufalme wa mbinguni. Sasa mapenzi ya Baba, ni kuinua watu wamzunguke, Mwanawe, Kristo Yesu. Kusanyiko hilo ni Kanisahapa duniani, mbegu na mwanzo wa Ufalme wa Mungu. Wote wanaitwa kuingia katika ufalme wa Mungu.

Ekaristi Takatifu ni Sadaka ya Kristo Msalabani na Agano la Upendo.

Ekaristi Takatifu ni Sadaka ya Kristo Msalabani na Agano la Upendo.

Papa Francisko: Fumbo la Ekaristi Takatifu livunjilie mbali ubinafsi!

04/06/2018 08:37

Baba Mtakatifu Francisko anasema, kila wakati waamini wanapoadhimisha Fumbo la Ekaristi Takatifu, wanavutwa na uwepo wake katika maumbo ya Mkate na Divai; wanaalikwa kumwabudu na kumtafakari kwa jicho la imani, tayari kujimega na kujisadaka kwa ajili ya huduma makini kwa jirani zao!

Ekaristi Takatifu ni Sakramenti ya upendo, haki, amani na mshikamano!

Ekaristi Takatifu ni Sakramenti ya upendo, haki, amani na mshikamano.

Papa Francisko: Ekaristi Takatifu ni kifungo cha upendo!

04/06/2018 08:15

Baba Mtakatifu Francisko anasema, watu wanaoteseka kutokana na sababu mbali mbali; wanaotelekezwa na kujikuta wametumbukia katika upweke hasi; wote hawa ni sawa na Tabernakulo iliyotelekezwa; waamini wanaoshiriki Fumbo la Ekaristi takatifu wanapaswa kujimega na kujitoa kwa ajili ya wengine!

Papa Francisko: Zingatieni: Fumbo la Msalaba, Ekaristi Takatifu na Ibada kwa Bikira Maria, Mama wa Mungu na Kanisa.

Papa Francisko: Zingatieni: Fumbo la Msalaba, Adhimimisho la Ekaristi Takatifu na Ibada kwa Bikira Maria, Mama wa Mungu na Kanisa.

Siku kuu ya Bikira Maria Mama wa Kanisa

21/05/2018 08:37

Baba Mtakatifu Francisko anasema, ikiwa kweli waamini wanataka kuwa wafuasi amini wa Kristo Yesu na Kanisa lake; ili kuguswa na kuponywa na huruma pamoja na upendo wa Mungu, wanapaswa kuzingatia: Fumbo la Msalaba, Ekaristi Takatifu na Ibada ya Bikira Maria, Mama wa Mungu na Kanisa.