Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Fumbo la Mateso na Mahangaiko ya Binadamu

Injili ya ufufuko wa Kristo Yesu inaendelea kutangazwa na kushuhudiwa kwenye ulimwengu unaosheheni ukosefu wa haki jamii!

Injili ya ufufuko wa Kristo Yesu inaendelea kutangazwa na kushuhudiwa kwenye ulimwengu ambamo kuna ukosefu mkubwa wa haki jamii.

Injili ya Ufufuko inatangazwa katika Golgota ya ukosefu wa haki jamii

09/04/2018 08:36

Patriaki Bartholomeo wa kwanza anasema hata leo hii, Injili ya Ufufuko wa Kristo Yesu kutoka kwa wafu inaendelea kutangazwa na kushuhudiwa kwenye Ulimwengu wa Golgotha unaofumbatwa katika ukosefu wa haki jamii; dhuluma na nyanyaso kwa wakimbizi na wahamiaji pamoja na uharibifu wa mazingira.

Fumbo la Mateso, Kifo na Ufufuko wa Kristo Yesu ni kiini cha Habari Njema inayotangazwa na kushuhudiwa na Mama Kanisa!

Fumbo la Mateso, Kifo na Ufufuko wa Kristo Yesu ni kiini cha Habari Njema inayotangazwa na kushuhudiwa na Mama Kanisa.

Tafakari ya Mateso ya Kristo Yesu kwa jicho la wanawake!

26/03/2018 07:19

Fumbo la Pasaka ni kiini cha Habari Njema ambayo inatangazwa na kushuhudiwa na Kanisa. Imani inaweza kujaribu kutafuta mazingira ya mateso na kifo cha Yesu yaliyotajwa kiaminifu na Injili na kuangazwa na chemchemi nyingine za historia ili kujua maana ya ukombozi katika maisha ya binadamu!

Jumapili ya Matawi ni mwanzo wa maadhimisho ya Juma kuu! Tafakari kuhusu nafasi na dhamana yako katika mateso ya Yesu kwa wakati huu!

Jumapili ya Matawi ni mwanzo wa maadhimisho ya Juma kuu mwaliko wa kutafakari nafasi na dhamana yako katika Mateso ya Kristo Yesu kwa wakati huu!

Je, wewe unachukua nafasi na dhamana gani katika Mateso ya Yesu?

24/03/2018 08:47

Jumapili ya Matawi inaliingiza Kanisa katika maadhimisho ya Juma kuu, yaani: Siku kuu tatu: Alhamisi kuu Kanisa linapokumbuka kuwekwa kwa Sakramenti ya Ekaristi Takatifu, Daraja na Huduma ya upendo; Ijumaa kuu: Mateso na Kifo cha Kristo Yesu, Jumamosi kuu, kimya kikuu na hatimaye Pasaka!

Fumbo la mateso, kifo na ufufuko wa Kristo Yesu ni ufunuo wa huruma, upendo na msamaha wa Mungu kwa binadamu!

Fumbo la mateso, kifo na ufufuko wa Kristo Yesu ni ufunuo wa huruma, upendo, na msamaha wa Mungu kwa binadamu!

Fumbo la Mateso ya Kristo Yesu katika maisha ya mwanadamu!

23/03/2018 15:38

Wenye dhambi wote, walikuwa ni chanzo cha Mateso ya Kristo Yesu. Yesu alitolewa ili atese na hatimaye kufa Msalabani kadiri ya Mpango wa Mungu uliokusudiwa tangu milele yote. Alikufa kwa ajili ya dhambi za binadamu kadiri ya Maandiko Matakatifu na alifanywa kuwa dhambi kwa ajili ya watu!

 

Kwaresima iwe ni fursa ya kutafakari mateso na kifo cha Kristo! Msalabani, ili kuonesha toba na wongofu wa ndani!

Kwaresima iwe ni fursa ya kutafakari mateso, kifo na ufufuko ili kuonesha toba na wongofu wa ndani, tayari kusimama kidete kulinda, kutetea na kudumisha: haki, amani na maridhiano kati ya watu.

Wakristo fungeni na kusali katika roho na kweli!

24/02/2018 09:25

Kwaresima ni kipindi cha kusali, kufunga, kutafakari na kutenda matendo ya huruma kwa maskini na wahitaji zaidi. Hiki ni kipindi muafaka kwa ajili ya maandalizi ya adhimisho la Fumbo la Pasaka, yaani: mateso, kifo na ufufuko wa Kristo kutoka kwa wafu. Hata leo hii kuna bado watu wanateseka!