Tasaufi ya Damu Azizi ya Kristo Yesu ni dira na mwongozo wa maisha ya Kikristo yanayojikita katika uhusiano na mafungamano kati ya Mwenyezi Mungu na jirani. Tasaufi hii inajengwa katika misingi ya Neno la Mungu, Mapokeo ya Kanisa, Ushuhuda na Mafundisho ya Watakatifu, Liturujia na Sakramenti.
Damu Azizi ya Kristo Yesu ni mto wa rehema, shule ya huruma, msamaha, upatanisho, upendo na utakatifu wa maisha!
Tasaufi ya Damu Azizi ya Yesu ni shule ya huruma ya Mungu kwa binadamu; msamaha ulioletwa na Kristo Yesu kwa kumwaga damu yake Azizi Msalabani na hivyo ikawa ni sadaka ya upatanisho kati ya Mungu na binadamu! Damu Azizi ya Kristo ni mto wa rehema na upendo wa Mungu kwa binadamu!
Damu Azizi ya Yesu ni utimilifu wa maisha ndiyo kauli mbiu iliyooongoza hija ya kukutana na Papa Francisko tarehe 30 Juni 2018.
Damu Azizi ya Yesu ni utimilifu wa maisha ndiyo kauli mbiu ambayo imeongoza hija ya familia ya Damu Azizi ya Yesu inayoundwa na wamisionari, watawa na waamini walei ambao wako chini ya Ushirika wa Damu ya Kristo, "Unione Sanguis Christi" wakati wa kukutana na Papa Francisko mjini Vatican!
Wosia wa Papa Francisko kwa familia ya Damu Azizi ya Yesu: Ujasiri wa ukweli, upendeleo kwa maskini, ushuhuda wenye mvuto na mashiko sanjari na uwezo wa kuwasiliana na wengine.
Baba Mtakatifu Francisko ameitaka Familia ya Damu Azizi ya Yesu kujikita zaidi katika ujasiri wa ukweli; kwa kuwa na jicho la upendeleo kwa maskini; kwa kutoa ushuhuda wenye mvuto na mashiko pamoja na uwezo wa kuwasiliana na wengine kama njia ya kushirikishana kweli za Kiinjili!
Mitandao ya kijamii: