Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Fadhila ya Matumaini

Kila siku katika maisha yetu , turudie kuomba kama wafuasi wake wa  kwanza kwa lugha ya kiaramaiko walisema  ”Maranatha"

Kila siku katika maisha yetu , turudie kuomba kama wafuasi wake wa kwanza kwa lugha ya kiaramaiko walisema ”Maranatha"

Papa:Kila siku ni ukurasa mweupe wa kuandika matendo mema ya Mungu

11/10/2017 16:08

Papa katika Katekesi yake tarehe 11 Oktoba katika Viwanja vya Mtakatifu Petro anasema,Yesu anataka maisha yetu yawe ya kuwajibika bila kuchoka,kutoa shukrani kwa maajabu yake tunayo pokea kila siku.Kila asubuhi ni ukurasa mpya mweupe ambao mkristo analazimika kuandika matendo mema.

 

Katika katekesi ya baba Mtakatifu Jumatano 27 Septemba 2017, anasema matumaini ni kama wema wa aina yoyote amabao daima unakumbana na maadui

Katika katekesi ya baba Mtakatifu Jumatano 27 Septemba 2017, anasema matumaini ni kama wema wa aina yoyote amabao daima unakumbana na maadui

Papa: Matumaini kama aina ya wema mwingine duniani ina maadui wake

27/09/2017 15:49

Papa anasema:Matumaini ni msukumu wa moyo kwa yule nayesafiri kuacha nyumba,ardhi,wakati mwingine familia na ndugu kwa ajili ya kutafuta maisha bora na yenye hadhi kwa ajili yake na ndugu zake.Vile matumaini yanatoa msukumo katika moyo ya yule anayepokea kwa shahuku ya kukutana

 

Papa Francisko anawaalika waamini kujikita katika malezi na majiundo ya matumaini ya Kikristo!

Papa Francisko anawaalika waamini kujikita katika malezi na majiundo ya matumaini ya Kikristo!

Papa Francisko: Jikiteni katika malezi ya matumaini ya Kikristo!

20/09/2017 14:46

Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kujikita katika malezi ya matumaini ya kikristo yanayowawezesha kusonga mbele katika maisha, licha ya shida, magumu na changamoto wanazoweza kukumbana nazo katika hija ya maisha yao hapa duniani!

Papa Francisko anawaalika waamini kuiga mfano bora wa Ibrahimu baba wa imani na matumaini katika maisha yao!

papa Francisko anawaalika waamini kuiga mfano bora wa Ibrahimu baba wa imani na matumaini katika maisha yao!

Ibrahimu ni baba wa imani na matumaini, mfano bora wa kuigwa!

29/03/2017 13:42

Ibrahimu ni baba wa imani na matumaini kwani alimiani kwa kutarajia yasiowezekana, hali inayojonesha kwa namna ya pekee katika maisha yake kwa kukiona kifo kinamkodolea macho sanjari na maisha ya Sarak aliyekuwa mgumba, kiasi cha kutotarajia kupata mtoto, lakini akajiaminisha kwa Mungu!

Mtakatifu Paulo anatukumbusha ya kwamba saburi na faraja vinaoneshwa na kwa namna ya pekee katika neno yaani yaliyoandikwa yameandikwa

Mtakatifu Paulo anatukumbusha ya kwamba saburi na faraja vinaoneshwa na kwa namna ya pekee katika neno yaani yaliyoandikwa yameandikwa

Mkristo huongozwa na saburi na faraja ili awe mfereji wa tumaini

22/03/2017 16:37

Anaye fanya uzoefu binafsi wa maisha yake ya upendo mwaminifu katika Mungu anauwezo na zaidi analazimika kukaa karibu na ndugu wadhaifu kubeba mizigo yao.Anaweza kufanya hivyo bila kujipendelea binafsi kijisikia kama vile mfereji unao toa zawadi za Bwana, na kama mpanzi wa matumaini

 

Kwaresima ni kipindi cha matumaini, imani, toba na wongofu wa ndani!

Kwaresima ni hija ya matumaini, imani, mapendo, toba na wongofu wa ndani!

Kwaresima ni kipindi cha matumaini, imani, toba na wongofu wa ndani

01/03/2017 11:56

Kwaresima ni safari ya matumaini ya siku 40 kutoka katika jangwa la maisha ya dhambi na mauti kuelekea katika maadhimisho ya Fumbo la Pasaka, yaani mateso, kifo na ufufuko wa Kristo Yesu kwa njia ya: toba, wongofu wa ndani; maadhimisho ya Sakramenti za Kanisa, tafakari na matendo ya huruma.

Tafuteni kwanza ufalme wa Mungu, mengine yote mtapewa kwa ziada!

Tafuteni kwanza ufalme wa Mungu, mengine yote mtapewa kwa ziada.

Msiwe na hofu, wekezeni kwenye Injili ya Kristo!

25/02/2017 12:50

Watumishi wa Kristo wanakumbushwa kwamba, wao ni walinzi wa Mafumbo Matakatifu ya Mungu, dhamana wanayopaswa kuitekeleza kwa unyenyekevu, utii na unyofu wa moyo! Waamini waendelee kumtumainia na kumtegemea Mwenyezi Mungu, kwani ndiye asili ya wema na utakatifu wote!

 

Hamwezi kumtumikia Mungu na mali!

Hamwezi kumtumikia Mungu na mali!

Mtumainieni Mungu katika maisha yenu!

24/02/2017 14:04

Liturujia ya Neno la Mungu, Jumapili VIII ya Kipindi cha Mwaka A wa Kanisa inajikita zaidi katika fadhila ya matumaini kwa Mwenyezi Mungu aliyeasili ya wema wote! Waamini wanaonywa kwamba, kamwe hawawezi kumtumikia Mungu na mali! Mali iwasaidie waamini kuwaendea jirani zao kwa njia ya huduma!