Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

DR. Olav F. Tveit

Jubilei ya Miaka 70 ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni: Ushuhuda wa toba, wongofu na upatanisho!

Jubilei ya Miaka 70 ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni, WCC. Ushuhuda wa toba, wongofu na upatanisho kama alama na kielelezo makini cha uinjilishaji.

WCC: Ulimwengu uliomeguka unahitaji alama na ushuhuda wa nguvu!

21/06/2018 17:20

Walimwengu waliogawanyika na kusambaratika juu ya uso wa dunia, wanahitaji alama na ushuhuda wenye mvuto na mashiko, changamoto na mwaliko kwa Wakristo kujipatanisha, kudumisha umoja, kulinda maisha na kutunza mazingira nyumba ya wote, daima haki msingi za binadamu zikipewa kipaumbele!

Papa Francisko: Wakristo wanahamasishwa kuenenda katika Roho!

Papa Francisko: Wakristo wanahamasishwa kuenenda katika Roho!

Papa Francisko asema, Wakristo wanahimizwa kuenenda katika Roho!

21/06/2018 16:56

Baba Mtakatifu Francisko katika Ibada ya sala ya toba, upatanisho na umoja wa Makanisa amewataka Wakristo kuenenda katika Roho kwa kutambua kwamba, binadamu hapa duniani ni hujaji na kwamba, kuenenda katika Roho ni kiini cha wito na maisha ya Kikristo; ni kujikita katika msamaha na huduma!

Baraza la Makanisa Ulimwenguni limetuma salam na matashi mema kwa waamini wa dini ya Kiislam baada ya kuhitimisha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Baraza la Makanisa Ulimwenguni limetuma salam na matashi mema kwa waamini wa dini ya Kiislam baada ya kuhitimisha mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Baraza la Makanisa Ulimwenguni: Salam za Id Al Fitri kwa Waislam

15/06/2018 11:36

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa waamini wa dini ya Kiislam kimekuwa ni kipindi cha kufunga na kuswali; toba na kutoa sadaka kama njia ya kumwilisha huruma na ukarimu wa Mwenyezi Mungu katika uhalisia wa maisha yao. Kimekuwa ni kipindi cha kujichotea amana na utajiri kutoka kwenye Quran Tukufu.

 

Waraka wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni uko tayari kuwakilishwa katika Mkutano Kuu utakao fanyika mjini Geneva 21 Juni 2018

Waraka wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni uko tayari kuwakilishwa katika Mkutano Kuu utakao fanyika mjini Geneva 21 Juni 2018

Waraka wa Baraza la Makanisa duniani uitwao,tunaitwa kubadili matendo!

04/06/2018 13:08

Shirikisho la Kiluteri duniani na Shirikisho la mshikamano wa matendo na Baraza la Kiekumene la Makanisa watia saini kwa Waraka  uitwao:Tunaitwa kubadili matendo. Ushemasi wa kiekumeni. ni Waraka ambao utawakilishwa katika kamati kuu ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni mjini Geneva. 

 

 

Uwepo na ushiriki wa Baba Mtakatifu Francisko katika Jubilei ya miaka 70 ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni ni zawadi kwa Makanisa!

Uwepo na ushiriki wa Baba Mtakatifu Francisko kwenye Jubilei ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Makanisa Ulimwenguni ni zawadi kubwa kwa Makanisa!

Papa Francisko ni zawadi kwa Makanisa katika majadiliano ya kiekumene

16/05/2018 08:40

Nembo na kauli mbiu inayoongoza hija ya kiekumene ya Baba Mtakatifu Francisko mjini Geneva nchini Uswiss, tarehe 21 Juni 2018 inakazia umuhimu wa Makanisa: Kutembea, Kusali na Kushirikiana kama muhtasari wa dhamana na malengo makuu ya majadiliano ya kiekumene miongoni mwa Makanisa!

Ufuasi wa kweli kwa Kristo Yesu unafumbatwa katika: ari ya kimisionari, sadaka na ushuhuda wa imani katika matendo!

Ufuasi wa kweli kwa Kristo Yesu unafumbatwa katika ari ya kimisionari, sadaka na ushuhuda wa maisha ya kila siku!

Baraza la Makanisa Ulimwenguni: Utume unafumbata sadaka na ushuhuda

14/03/2018 09:45

Baraza la Makanisa Ulimwenguni katika mkutano wake mkuu wa uinjilishaji ulimwenguni, limefafanua kwamba, utume na ufuasi kwa Kristo Yesu na Kanisa lake kwa namna ya pekee kabisa, unafumbatwa katika:ari na nia thabiti ya kumfuasa Kristo pamoja na ushuhuda wenye mvuto na mashiko, kila siku!

Makanisa ulimwenguni yanapaswa kuwa ni vyombo na mashuhuda wa: uinjilishaji, utamadunisho na haki msingi za binadamu.

Makanisa ulimwenguni yanapaswa kuwa ni vyombo na mashuhuda wa uinjilishaji na utamadunisho; haki, amani na maridhiano kati ya watu wa Mataifa.

Makanisa Ulimwenguni yawe ni: vyombo vya haki, amani na upendo!

13/03/2018 08:10

Mkutano mkuu wa uinjilishaji ulimwenguni uliokuwa unatimua vumbi kwenye kilima cha Ngurdoto, Jijini, Arusha Tanzania kuanzia tarehe 8 -13 Machi 2018 imekuwa ni nafasi murua kwa Makanisa kusali, kutafakari na kushirikishana changamoto na vipaumbele katika mchakato wa uinjilishaji kwa nyakati hizi!

Papa Francisko ni shuhuda wa majadiliano ya kiekumene yanayowawezesha Wakristo kutembea, kusali na kufanya kazi kwa umoja kwa ajili ya huduma!

Papa Francisko ni shuhuda na chombo cha majadiliano ya kiekumene kinachowawezesha Wakristo kutembea, kusali na kufanya kazi katika umoja kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu sehemu mbali mbali za dunia.

Papa Francisko ni shuhuda wa majadiliano ya kiekumene katika huduma

13/03/2018 07:47

Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 13 Machi 2018 anaadhimisha kumbu kumbu ya miaka 5 tangu alipochaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki kwa kulitaka Kanisa kujielekeza zaidi katika: huduma kwa maskini kama amana na utajiri wa Kanisa; Amani na Utunzaji Bora wa Mazingira bila kusahau Uekumene!