Mitandao ya kijamii:

RSS:

App:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Dr. Gregory Joseph Burke

Baraza la Makardinali Washauri limejadili kuhusu Mabaraza ya Uinjilishaji, Majadiliano pamoja na Sheria na Mahakama za Kanisa

Baraza la Makardinali Washauri limejadili kuhusu Mabaraza ya Kipapa kuhusu Uinjilishaji, Majadiliano, Sheria na Mahakama za Kanisa.

Yaliyojiri mkutano wa Baraza la Makardinali washauri!

27/04/2017 10:06

Mkutano wa Baraza la Makardinali washauri chini ya uongozi wa Baba Mtakatifu Francisko umejadili pamoja na mambo mengine: mabaraza kadhaa ya Kipapa hususan mintarafu Uinjilishaji, Haki na Sheria! Makardinali wameangalia kuhusu uteuzi na majiundo makini kwa wakleri na walei mjini Vatican!

 

Papa Francisko mjumbe na shuhuda wa amani anatembelea nchini Misri kuanzia tarehe 28 - 29 Aprili 2017

Papa Francisko mjumbe na shahidi wa amani anatembelea nchini Misri kuanzia tarehe 28- 29 Aprili 2017 ili kuwaimarisha ndugu zake katika imani, kukuza na kudumisha majadiliano ya kidini pamoja na kuendeleza majadiliano ya kiekumene.

Papa Francisko mjumbe wa amani nchini Misri

25/04/2017 15:00

Hija ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Misri inalenga kwanza kabisa kuwaimarisha ndugu zake katika imani, mapendo na matumaini tayari kumshuhudia Kristo na Kanisa lake. Pili ni kukuza na majadiliano ya kidini na Waislam na tatu na kuendeleza uekumene wa damu na Wakristo!

Familia ya Mungu nchini Brazil inaadhimisha kumbu kumbu ya miaka 300 tangu Bikira Maria wa Aparecida alipotokea na kuwa ni chemchemi ya ibada kubwa.

Familia ya Mungu nchini Brazil kwa mwaka 2017 inaadhimisha kumbu kumbu ya miaka 300 tangu Bikira Maria wa Aparecida alipotokea na hivyo kuwa ni chemchemi ya ibada kuu kwa Bikira Maria, Mama wa Mungu na Kanisa.

Jubilei ya miaka 300 tangu Bikira Maria alipotokea Aparecida!

19/04/2017 11:00

Familia ya Mungu nchini Brazil kwa mwaka 2017 inaadhimisha Jubilei ya miaka 300 tangu Bikira Maria alipotokea kule Aparacida na kuwa ni chemchemi ya Ibada ya nguvu kwa wananchi wengi huko Amerika ya Kusini! Rais wa Brazil amemwalika Papa Francisko katika tukio hili, lakini imeshindikana kwa sasa!

Papa Francisko tarehe 22 Aprili 2017 atasali Lituruji ya Neno la Mungu kwa ajili yua mashuhuda wa imani kwa karne ya XX & XXI

Papa Francisko tarehe 22 Aprili 2017 ataadhimisha Liturujia ya Neno la Mungu kama sehemu ya kumbu kumbu ya mashuhuda wa imani wa karne ya XX na karne ya XXI.

Papa Francisko kuadhimisha kumbu kumbu ya mashuhuda wapya wa imani!

12/04/2017 13:44

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 22 Aprili 2017 majira ya saa 11: 00 jioni kwa saa za Ulaya ataadhimisha Ibada ya Liturujia ya Neno la Mungu kwa kushirikiana na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio kwa ajili ya kuwakumbuka mashuhuda wa imani waliojisadaka kwa ajili ya Kristo katika karne ya XX & XXI.

Papa Francisko kufanya hija ya kitume nchini Misri kuanzia tarehe 28-29 Aprili 2017.

Papa Francisko kufanya hija ya kitume nchini Misri kuanzia tarehe 28-29 Aprili 2017.

Papa Francisko shuhuda wa amani nchini Misri: Ratiba elekezi

03/04/2017 14:00

Hija ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Misri kuanzia tarehe 28- 29 Aprili 2017 inaongozwa na kauli mbiu "Papa wa amani nchini Misri". Baba Mtakatifu anapenda kutembelea nchini Misri ili kukuza na kudumisha mchakato wa majadiliano ya kidini na kiekumene ili kuimarisha amani na upendo.

 

Papa Francisko amekubali mwaliko wa kutembelea Misri kuanzia tarehe 28- 29 Aprili 2017

Papa Francisko amekubali mwaliko wa kutembelea Misri kuanzia tarehe 28- 29 Aprili 2017.

Ziara ya Papa Francisko Barani Afrika, 28 - 29 Aprili 2017

18/03/2017 15:47

Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kutembelea Barani Afrika, hususan nchini Misri kuanzia tarehe 28- 29 Aprili 2017 ziara ambayo inapania pamoja na mabo mengine kuendelea kuimarisha majadiliano ya kidini na kiekumene, ili kudumisha umoja, upendo na mshikamano kati ya watu wa mataifa!

Jumuiya ya Umoja wa Ulaya inaadhimisha kumbu kumbu ya miaka 60 kwa kukutana pia na Papa Francisko

Jumuiya ya Ulaya inaadhimisha Miaka 60 tangu kuanzishwa kwake kwa kukutana pia na Papa Francisko.

Papa Francisko kukutana na kuzungumza na "vigogo" wa Umoja wa Ulaya

04/03/2017 15:10

Umoja wa Ulaya unaadhimisha kumbu kumbu ya miaka 60 tangu ulipoanzishwa kwa wakuu wa nchi kwa wakati huo walipotia mkwaju katika Mkataba wa Roma. Kilele cha maadhimisho haya ni hapo tarehe 25 Machi 2017. Hii itakuwa ni nafasi kwa wakuu wa Umoja wa Ulaya kukutana na Papa Francisko.

 

Tarehe 26 Februari 2017 Papa Francisko anatembelea Kanisa Anglikani mjini Roma.

Tarehe 26 Februari 2017 Papa Francisko anatembelea Kanisa Anglikani mjini Roma.

Papa Francisko kutembelea Kanisa Anglikani Roma, 26 Februari 2017

20/02/2017 12:00

Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kuchochea mchakato wa majadiliano ya kiekumene yanayofumbatwa katika: damu, sala, maisha ya kiroho na huduma makini kwa maskini na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii kama kielelezo cha imani tendaji. Tarehe 26 Fe. 2017 anawatembelea Waanglikani.