Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Dhambi ya asili

Mateso na kifo ni kati ya changamoto zinazomkabili mwanadamu, mwaliko wa kuliangalia Fumbo la Pasaka!

Mateso na kifo ni ya changamoto zinazomwandama mwanadamu, changamoto ni kuangalia Fumbo la Pasaka kwa imani na matumaini.

Tafakari ya Neno la Mungu: Fumbo la mateso na kifo katika maisha!

30/06/2018 07:16

Tafakari ya Neno la Mungu, Jumapili ya XIII ya Kipindi cha Mwaka B wa Kanisa ni mwaliko wa kutafakari kwa kina na mapana mambo makuu katika maisha ya mwanadamu: magonjwa na hatimaye kifo; kwamba, haya ni matokeo ya dhambi ya asili, lakini Kristo Yesu ameibuka kidedea kwa Fumbo la Pasaka!

Mwanadamu ana lazima ya kufuataq sheria maadili inayomsukuma kutenda jema na kuepuka ovu. Sheria hii inaongea ndani kabisa ya dhamiri ya mtu!

Mwanadamu ana lazima ya kufuata sheria ya maadili inayomsukuma kutenda jema na kuepuka ovu. Sheria hii yaongea ndani kabisa ya dhamiri ya mwanadamu!

Dhambi na matokeo ya ufunuo wa mpango wa ukombozi wa mwanadamu

09/06/2018 16:39

Mwenyezi Mungu ni mwingi wa huruma na mapendo, mambo yanayojionesha tangu pale Adamu na Eva walipoanguka dhambini na kujikuta wako watupu, kwa kupoteza: urafiki na Mwenyezi Mungu; Uhuru wa kweli; Wema na utakatifu wa maisha! Lakini Mungu anawaahidia ukombozi!

Maisha yote ya Kristo Yesu ni Fumbo linalomrejeshea mwanadamu wito wake wa asili, yaani ile sura na mfano wa Mungu.

Maisha yote ya Kristo Yesu ni fumbo linalomrejeshea tena mwanadamu ule wito wake wa asili, yaani sura na mfano wa Mungu

Maisha yote ya Kristo Yesu ni Fumbo kuu!

06/06/2018 15:09

Mama Kanisa anafundisha kwamba, maisha yote ya Kristo Yesu ni fumbo linalojumlisha yote. Yote Yesu aliyofanya, kutenda na kuteseka yalikuwa na lengo la kumrudisha mtu aliyeanguka katika wito wake wa awali; yaani kwa kuwa ni sura na mfano wa Mungu pamoja na kuwarejeshea tena ushirika na Mungu!

Papa Francisko anasema, ukatili, nyanyaso na dhuluma dhidi ya jirani ni matokeo ya dhambi ya asili!

Papa Francisko anasema dhuluma, nyanyaso na ukatili dhidi ya jirani ni matokeo ya dhambi ya asili.

Papa Francisko: Ukatili na unyanyasaji ni madhara ya dhambi ya asili

09/01/2018 10:30

Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri yake anasema, wataalamu mbali mbali wanaweza kuwa na upembuzi yakinifu kuhusu sababu zinazopelekea baadhi ya watu kujikuta wakifanya ukatili, nyanyaso na udhalimu dhidi ya jirani zao, kadiri ya imani, haya ni madhara ya dhambi ya asili!