Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Dawa za kulevya

Papa Francisko anawaalika vijana kujitahidi kukutana na Kristo Yesu katika maisha yao ili awagange na kuwaponya katika mahangaiko yao.

Papa Francisko anawaalika vijana wa kizazi kipya kujitahidi kukutana na Kristo Yesu katika hija ya maisha yao ili aweze kuwaganga na kuwaponya katika shida na mahangaiko yao.

Wosia wa Baba Mtakatifu Francisko kwa vijana wa kizazi kipya!

28/05/2017 13:44

Baba Mtakatifu Francisko anawataka vijana wa kizazi kipya kujenga na kudumishaz utamaduni wa sala, tafakari na matendo ya huruma kwa jirani zao! Ikiwa kama kweli wanataka kuwa ni wamissionari wanapaswa kuwapenda, kuwathamini na kujisadaka kwa ajili ya vijana wenzao wenye shida na mateso!

RECOWA-CERAO: changamoto kubwa: hali tete ya kisiasa; misimamo mikali ya kidini na majanga asilia.

RECOWA-CERAO: changamoto kubwa: hali tete ya kisiasa, kiuchumi na kijamii; misimamo mikali ya kidini na kiimani pamoja na athari za majanga asilia.

RECOWA-CERAO na changamoto zake Afrika Magharibi!

19/04/2017 11:12

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Magharibi linasema, linapenda kushirikiana kwa dhati na Jumuiya ya Uchumi Afrika Magharibi,ECOWAS ili kukabiliana na changamoto zinazoendelea kujitokeza katika Nchi wanachama wa RECOWA-CERAO hasa: vitendo ya kigaidi na misimamo mikali ya kidini

Mkesha wa Pasaka ni mama wa mikesha yote ambao umesheheni utajiri wa mafumbao, maisha na utume wa Kanisa!

Mkesha wa Pasaka ni mama wa mikesha yote unaofumbata: mafumbo, maisha na utume wa Kanisa!

Papa Francisko: Kristo Mfufuka ni chemchemi ya matumaini mapya!

16/04/2017 15:03

Baba Mtakatifu Francisko ameongoza Mkesha wa Pasaka unaofumbata utajiri mkubwa wa maisha na utume wa Kanisa kwa njia ya alama mbali mbali! Amewabatiza wakatekumeni kumi na mmoja na kuwaimarisha kwa Sakramenti ya Kipaimara! Yesu Mfufuka ni chemchemi ya matumaini mapya kwa watu!

Yesu Kristo Mfufuka bado anaendelea kujitaabisha kuwatafuta waja wake ili kuwarejeshea utu na heshima yao!

Yesu Kristo Mfufuka bado anaendelea kujitaabisha ili kuwatafuta waja wake ili aweze kuwarejeshea tena utu na heshima yao kama binadamu!

Papa Francisko: Urbi et Orbi: Mchungaji mwema bado anawatafuta watu wake!

16/04/2017 14:37

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa mji wa Roma na Dunia katika ujumla wake, amewakumbusha walimwengu kwamba, Yesu Kristo Mchungaji mwema aliyeteswa, akafa na kufufuka kwa watu bado anaendelea kujitaabisha kuwatafuta wake wake ili kuwarudishia hadhi na utu wao!

Askofu Mapunda anawataka Mapadre kushuhudia wito na maisha ya Kipadre; kuwekeza kwa vijana na kujisadaka kwa ajili ya huduma kwa wagonjwa.

Askofu Edward Mapunda wa Jimbo Katoliki Singida anawataka Mapadre kushuhudia maisha na wito wao wa Kipadre; kuwekeza kwa utume wa vijana wa kizazi kipya pamoja na kujisadaka kwa ajili ya huduma kwa wagonjwa na wazee.

Askofu Mapunda: Shuhudieni Upadre; wekezeni kwa vijana na wagonjwa!

13/04/2017 15:18

Askofu Edward Mapunda wa Jimbo Katoliki Singida, Tanzania anawataka Mapadre kushuhudia utakatifu na ukuu wa maisha na wito wao wa Kipadre sanjari na kuwekeza katika maisha na utume wa vijana wa kizazi kipya kwa kujisadaka kwa ajili ya wagonjwa wanaohitaji faraja, upendo, imani na matumaini!

Waziri mkuu wa Tanzania asema: watanzania msijiingize kwenye biashara ya dawa za kulevya!

Waziri mkuu wa Tanzania amewataka watanzania kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi na kamwe wasikubali kujitumbukiza au kutumbukizwa kwenye biashara na matumizi haramu ya dawa za kulevya.

Msithubutu kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya!

22/03/2017 15:47

Waziri mkuu wa Tanzania Kassim M. Majaliwa amewataka watanzania kujenga nidhamu, utii wa sheria, taratibu na kanuni za nchi husika na kamwe wasithubutu kujihusisha na biashara, usambazaji na matumizi haramu ya dawa za kulevya kwani ni hatari kwa maisha yao na usalama wa nchi!

 

Kuna mamilioni ya wanawake, wasichana na watoto wanaotumbukizwa katika biashara haramu ya binadamu na viungo vyake.

Kuna mamilioni ya wanawake, wasichana na watoto wanaotumbukizwa katika biashara haramu ya binadamu na viungo vyake; utumwa mamboleo na mifumo yake yote! Vatican inaendelea kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya mifumo yote hii kwa maneno na vitendo.

Vatican na mapambano dhidi ya biashara haramu ya binadamu!

20/03/2017 10:00

Kuna mamilioni ya watu wanaotumbukizwa katrika biashara haramu ya binadamu na viungo vyake; utumwa mamboleo na mifumo yake yote inayoendelea kudhalilisha utu na heshima ya binadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Vatican iko mstari wa mbele kutetea utu na heshima ya binadamu!

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania linamshukuru Mungu kwa kuadhimisha Jubilei ya Miaka 150 ya Ukristo, Tanzania Bara.

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania lina mshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuadhimisha Jubilei ya miaka 150 ya Ukristo, Tanzania Bara.

Sala ya Jubilei ya Miaka 150 ya Ukristo, Tanzania Bara

10/03/2017 11:13

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania linamshukuru na kumwimbia Mwenyezi Mungu utenzi wa sifa na shukrani kwa kuadhimisha Jubilei ya Miaka 150 ya Ukristo, Tanzania Bara. Maaskofu wanalishukuru Shirika la Roho Mtakatifu; wanagusia kukua na kukomaa kwa Kanisa na changamoto za Tanzania.