Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Biashara ya ngono

Kuwashughulikia wafanyabiashara ya binadamu na utumwa mamboleo ni tendo la haki, lakini tiba muafaka ni toba na wongofu wa ndani dhidi ya kifo!

Kuwashughulikia wafanyabiashara wa binadamu na utumwa mamboleo ni tendo la haki kabisa lakini tiba muafaka ni toba na wongofu wa ndani ili kuachana kabisa na utamaduni wa kifo unaodhalilisha utu na heshima ya binadamu!

Biashara ya binadamu na utumwa mamboleo: tiba ni toba na wongofu!

20/02/2018 06:43

Baba Mtakatifu Francisko anasema biashara haramu ya binadamu na utumwa mamboleo ni uhalifu dhidi ya binadamu, pamoja na mambo yote yanayoweza kutekelezwa kwa njia ya ushirikiano wa kitaifa, kikanda na kimataifa, lakini tiba muafaka ni toba na wongofu wa ndani ili kuachana na utamaduni wa kifo!

Papa Francisko akisalimiana na vijana walioudhuria Siku ya sala na uhamasishaji kimataifa kuhusu biashara haramu ya watumwa

Papa Francisko akisalimiana na vijana walioudhuria Siku ya sala na uhamasishaji kimataifa kuhusu biashara haramu ya watumwa

Papa Francisko:inahitaji ujasiri kufichua wanafiki wa biashara ya watumwa!

13/02/2018 15:44

Papa Francisko amebadilishana mawazo na baadhi ya washiriki wa Mkutano ya Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Biashara haramu ya binadamu na utumwa mamboleo. Amejibu maswali mengi kuhusu: unyanyasaji kijinsia, uonevu, shule za picha za ngono katika mitandao,kifolaini na sintofahamu!

 

Biashara haramu ya binadamu na utumwa mamboleo una madhara makubwa katika utu, heshima na haki msingi za binadamu!

Biashara haramu ya binadamu na utumwa mamboleo vina madhara makubwa katika utu, heshima na haki msingi za binadamu.

Mt. Bakhita ni kielelezo cha mapambano dhidi ya utumwa mamboleo!

12/02/2018 09:36

Maadhimisho ya kumbu kumbu ya Mtakatifu Josefine Bakhita ni changamoto endelevu kwa Jumuiya ya Kimataifa kuhakikisha kwamba, inasimama kidete ili kupmbana kufa na kupona na biashara haramu ya binadamu na utumwa mamboleo, madonda makubwa katika utu, maisha na haki msingi za binadamu!

Utumwa mamboleo ni uhalifu dhidi ya utu, heshima na haki msingi za binadamu!

Utumwa mamboleo ni uhalifu dhidi ya utu, heshima na haki msingi za binadamu

Biashara ya binadamu na utumwa mamboleo ni uhalifu dhidi ya ubinadamu

10/02/2018 17:44

Biashara haramu ya binadamu na utumwa mambo leo ni uhalifu mkubwa dhidi ya utu, heshima na haki msingi za binadamu; mambo ambayo wakati mwingine yanafumbiwa na jamii, lakini umefika wakati kwa Jumuiya ya Kimataifa kuhakikisha kwamba, inatokomeza kabisa biashara ya binadamu na athari zake.

Papa Francisko: Uongozi bora na makini katika vikosi vya ulinzi na usalama, wanasiasa na mihimili ya uinjilishaji ni muhimu katika kupambana na utumwa

Papa Francisko: uongozi bora na makini katika vikosi vya ulinzi na usalama, miongoni mwa wanasiasa na mihimili ya uinjilishaji ni muhimu sana katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya binadamu na utumwa mamboleo.

Papa Francisko: Uongozi bora ni dawa ya mchunguti dhidi ya utumwa!

09/02/2018 15:44

Baba Mtakatifu Francisko anasema, uongozi bora na makini katika vikosi vya ulinzi na usalama; miongoni mwa wanasiasa pamoja na mihimili ya uinjilishaji ni muhimu sana katika kupambana na janga la biashara ya binadamu na utumwa mamboleo unaofumbatwa katika biashara ya ngono na kazi za suluba!