Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Biashara ya binadamu

Jumuiya ya Kimataifa haina budi kulinda haki msingi za watoto hasa wale wanaoishi katika mazingira ya vita na machafuko ya kisiasa.

Jumuiya ya Kimataifa haina budi kulinda haki msingi za watoto wanaoishi katika mazingira ya vita na machafuko ya kisiasa.

Mbinu mkakati wa kuwalinda watoto kwenye maeneo ya vita na kinzani

10/07/2018 15:09

Askofu mkuu Bernardito Auza anasema, Jumuiya ya Kimataifa haina budi kulinda haki msingi za watoto wanaoishi katika maeneo ya vita kwa kuwawajibisha kisheria wale wote wanaowapeleka mstari wa mbele na kwenye mifumo ya utumwa mamboleo, kwa kuwaingiza katika jamii na kuwapatia elimu makini.

Shirika la Save the Children linaitaka Jumuiya ya Ulaya kuwa sera na mbinu mkakati wa kulinda, kuwaendeleza wato wakimbizi na wahamiaji.

Shirika la Save the Children linaitaka Jumuiya ya Kimataifa kulinda na kuwaendeleza watoto wakimbizi na wahamiaji.

Ulinzi, usalama na maendeleo ya watoto yapewe kipaumbele cha kwanza

26/06/2018 14:30

Shirika la Kimataifa la "Save the Children" linasema, Jumuiya ya Ulaya haiba budi kuhakikisha kwamba, inatoa kipaumbele kwa ulinzi na usalama wa watoto wakimbizi wanaotafuta: usalama, hifadhi na maisha bora zaidi. Watoto walindwe, waendelezwe na kushirikishwa katika maisha ya jamii inayowatunza. 

Papa Francisko: Simameni kidete kupambana na utamaduni wa kifo, utumwa mamboleo na biashara haramu ya binadamu.

Papa Francisko: Simaneni imara kupambana na utamaduni wa kifo, biashara haramu aya binadamu na utumwa mamboleo.

Papa Francisko shikamaneni kupambana na utumwa mamboleo!

15/06/2018 07:28

Baba Mtakatifu Francisko anawataka waamini kusimama kidete kulinda, kutetea na kudumisha Injili ya uhai dhidi ya utamaduni wa kifo, biashara haramu ya binadamu na utumwa mamboleo; mambo yanayoendelea kunyanyasa utu, heshima na haki msingi ya binadamu sehemu mbali mbali za dunia.

Tarehe 11 Juni 2018 Malta na Italia, zimewatakaa wakimbizi na wahamiaji 620 waliopewa hifadhi baadaye nchini Hispania.

Tarehe 11 Juni 2018 Malta na Italia ziliwakataa wakimbizi na wahamiaji 620 waliokuwa wanahofiwa kufa maji na baadaye Hispania imetoa hifadhi kwa wakimbizi na wahamiaji hawa.

Caritas Internationalis: Shiriki safari na wakimbizi kwa ukarimu!

12/06/2018 11:00

Shirikisho la Mashirika ya Misaada ya Kanisa Katoliki Kimataifa, Caritas Internationalis linasema, changamoto, fursa na matatizo yaliyoibuliwa na wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji linapaswa kushughulikiwa kwa moyo ya upendo na ukarimu ili kuondokana na ubinafsi pamoja na maamuzi mbele!

Baraza la Usalama la Umoja wa Mtaifa limepitisha Azimio dhidi ya walanguzi na wafanyabiashara haramu ya binadamu.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, hivi karibuni limepitisha Azimio dhidi ya walanguzi na wafanyabiashara ya binadamu.

Baraza la Usalama la UN na mapambano dhidi ya biashara ya binadamu

12/06/2018 09:57

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hivi karibuni limepitisha azimio la kutaifisha akaunti za walanguzi na wafanyabiashara haramu ya binadamu pamoja na kuwapiga marufuku kusafiri nje ya nchi zao kama mbinu mkakati wa Jumuiya ya Kimataifa wa kutaka kupambana na biashara hharamu ya binadamu.

 

Papa Francisko: Biashara ya binadamu na utumwa mamboleo ni uhalifu dhidi ya ubinadamu!

Papa Francisko: Biashara ya binadamu na utumwa mamboleo ni uhalifu dhidi ya utu, heshima na haki msingi za binadamu.

Mapambano dhidi ya utumwa mamboleo yanahitaji ushirikiano wa dhati!

05/06/2018 10:10

Toba na wongofu wa ndani, umoja na mshikamano; sera na mikakati inayoweza kutekelezeka ni mambo msingi katika mapambano dhidi ya biashara ya binadamu na viungo vyake pamoja na utumwa mamboleo unaodhalilisha utu, heshima pamoja na haki zake msingi! Huu ni uhalifu dhidi ya ubinadamu!

Jumuiya ya Yohane XXIII mwaka 2018 inaadhiisha Jubilei ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.

Jumuiya ya Yohane XXIII mwaka 2018 inaadhimisha Jubilei ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwake na Don Oreste Benzi kunako mwaka 1968.

Jumuiya ya Papa Yohane XXIII inaadhimisha Jubilei ya Miaka 50

24/05/2018 15:47

Jumuiya ya Papa Yohane XXIII iliyoanzishwa kunako mwaka 1968 na Don Oreste Benzi kama kielelezo cha umoja, upendo, udugu na mshikamano wa Kiinjili kwa maskini na watu wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii inaadhimisha Jubilei ya Miaka 50  ya uwepo na utume wake katika nchi 42 duniani! Si haba!

Utumwa mamboleo ni uhalifu dhidi ya utu, heshima na haki msingi za binadamu!

Utumwa mamboleo ni uhalifu dhidi ya utu na heshima ya binadamu.

Papa Francisko: Tushikamane kupambana na utumwa mamboleo duniani!

08/05/2018 13:26

Baba Mtakatifu Francisko anapenda kuihamasisha Jumuiya ya Kimataifa kushikamana katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya binadamu na utumwa mamboleo kwa kuvunjilia mbali ukimya, kwa kuwasaidia waathirika kwa kukuza na kudumisha haki msingi za binadamu, utawala wa sheria na maendeleo.