Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya

Maaskofu Katoliki Kenya: Jengeni utamaduni wa kuheshimu utawala wa sheria!

Maaskofu Katoliki Kenya: Jengeni utamaduni wa kutekeleza kwa dhati na kwa hiyari utawala was sheria.

Familia ya Mungu nchini Kenya jengeni utamaduni wa utawala wa sheria

07/09/2017 16:33

Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya linawaalika wadau mbali mbali nchini Kenya kuhakikisha kwamba, wanatekeleza uamuzi wa Mahakama kuu ili kufanikisha uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 17 Oktoba 2017! Wazingatie sheria, kanuni na taratibu ili uchaguzi mkuu uwe ni huru na wa haki.

Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya linawataka wanasiasa kuganga na kutibu magonjwa ya utengano na mipasuko ya kisiasa na kkijamii.

Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya linawataka wananchi wa Kenya kuganga na kuponya madonda ya athari za uchaguzi mkuu maka 2017.

Uchaguzi Mkuu Nchini Kenya: Ponyeni makovu ya utengano, jengeni umoja

16/08/2017 14:20

Mchakato mzima wa uchaguzi mkuu nchini Kenya umesababisha mpasuko mkubwa miongoni mwa familia ya Mungu nchini Kenya kwa misingi ya ushabiki wa kisiasa, ukabila na umajimbo; mambo ambayo hayana tija wala mashiko kwa ustawi na maendeleo ya wananchi wengi wa Kenya.

 

Mauaji ya Christopher Msando mtaalam wa teknolojia ya mawasiliano, Tume ya Uchaguzi Kenya yameacha pengo kubwa!

Mauaji ya Christopher Msando aliyepotea kwenye mazingira ya kutatanisha tangu tarehe 28 Julai na hatimaye, kupatikana tarehe 1 Agosti 2017 amekufa, kumeacha doa katika mchakato mzima wa uchaguzi mkuu nchini Kenya.

Uchaguzi mkuu Kenya kwa Mwaka 2017: Ombeeni amani na maendeleo!

01/08/2017 15:00

Bwana Wafula Chebukati, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Kenya anasema, mauaji ya Bwana Christopher Msando, Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Kenya aliyekuwa anashughulikia masuala ya teknolojia ya habari yamewasikitisha sana wapenda amani na demokrasia nchini Kenya!

Familia ya Mungu nchini Kenya inafanya uchaguzi mkuu hapo tarehe 8 Agosti 2017

Familia ya Mungu nchini Kenya inafanya uchaguzi mkuu tarehe 8 Agosti 2017.

Uchaguzi mkuu nchini Kenya 2017: Sifa kuu za viongozi wanaotakiwa!

29/07/2017 10:03

Familia ya Mungu nchini Kenya inaendelea kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na viongozi wa Serikali za mitaa, hapo tarehe 8 Agosti 2017. Hii ni fursa makini kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya kiraia, kwa kuzingatia sifa kuu za viongozi wanaopaswa kuchaguliwa!

Uchaguzi Kenya uwe wa amani na watafutwe viongozi waadilifu

Uchaguzi Kenya uwe wa amani na watafutwe viongozi waadilifu

Raia Kenya wachague viongozi waadilifu

24/06/2017 13:41

Taifa la Kenya linapoelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 8 2017, Baraza la Maaskofu Katoliki nchini humo, limeandika Barua ya kichungaji likialika kusimamia uchaguzi huru na wa amani, na raia wajichunguze vema dhamiri ili kuchagua viongozi waadilifu

Utamaduni wa uchoyo na ubaguzi unazidisha hali ya sasa kuwa ngumu na ndiyo maana wakenya sasa wana msukumo wa mawazo ya kukata tamaa

Utamaduni wa uchoyo na ubaguzi unazidisha hali ya sasa kuwa ngumu na ndiyo maana wakenya sasa wana msukumo wa mawazo ya kukata tamaa.

Maaskofu wa Kenya wanashutumu uchoyo na ubaguzi wa wanasiasa!

08/05/2017 11:38

Maaskofu wa Kenya wanasema,Bara la Afrika linakabiliana na mgogoro mbaya zaidi wa chakula kwa mihongo pia dharura kutokana na ukame.Lakini janga hilo ni pamoja na viongozi wenyewe kwasababu wanapoteza rasilimali chache zilizopo kununua kura.Utamaduni wa uchoyo na ubaguzi unakithiri Kenya

 

Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya katika kampeni yake ya Kwaresima linawataka wananchi  kufanya uchaguzi wa amani na unaoaminika.

Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya katika kampeni yake ya Kipindi cha Kwaresima linawataka waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kufanya uchaguzi wa amani na unaoaminika kama kielelezo cha ukomavu wa demokrasia.

Kampeni ya Kwaresima nchini Kenya kwa Mwaka 2017: Uchaguzi mkuu!

20/03/2017 10:29

Uchaguzi wa amani na unaominika ndiyo kauli mbiu iliyotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya katika kampeni ya Kwaresima mwa Mwaka 2017. Itakumbukwa kwamba, chaguzi nchini Kenya zimekuwa ni chanzo cha mipasuko ya kijamii na kisiasa nchini Kenya, kumbe, kuna haja ya kubadilika!

Maaskofu Katoliki Kenya wasema, wananchi wanakabiliwa na maafa ya njaa kutokana na ukame wa kutisha!

Maaskofu Katoliki Kenya wasema, wananchi wanakabiliwa na baa la njaa kutokana na ukame wa kutisha, kumbe, kuna haja kwa Serikali kutangaza kwamba, Kenya inakabiliwa na maafa ya njaa ili iweze kupatiwa msaada na Jumuiya ya Kimataifa.

Maaskofu Kenya: Watu wanakufa kwa baa la njaa!

09/02/2017 13:24

Taarifa kutoka majimbo mbali mbali ya Kanisa Katoliki nchini Kenya inaonesha kwamba, kuna idadi kubwa ya familia ya Mungu nchini Kenya inayoteseka kwa baa la njaa kutokana na ukame wa kutisha, mwaliko kwa Kenya kutangaza Kenya kuwa inakabiliwa na maafa ya njaa ili iweze kupata msaada!