Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baraza la Maaskofu Katoliki DRC

Vatican inaendelea kufuatilia kwa karibu sana hali ya kisiasa na kijamii nchini DRC!

Vatican inaendelea kufuatilia kwa karibu sana hali tete ya kisiasa na kijamii nchini DRC.

Papa Francisko anaendelea kufuatilia kwa karibu hali tete nchini DRC

14/04/2018 16:31

Baba Mtakatifu Francisko kwa nyakati mbali mbali ameonesha masikitiko makubwa pamoja na kuguswa na hali tete ya wananchi wa DRC wanaoendelea kuteseka kutokana na vita pamoja na mpasuko wa kisiasa na kijamii. Vatican inaiomba Jumuiya ya Kimataifa kusimamia mchakato wa uchaguzi DRC.

Caritas Internationalis inasema, hali ni tete sana nchini DRC, kunahitajika msaada wa dharura ili kuokoa maisha ya watu wanaoendelea kuteseka.

Caritas Internationalis insema, hali ni tete sana nchini DRC kuna watu wanauwawa kila siku na watoto wengi wanaishi katika mazingira hatarishi.

Caritas Internationalis: DRC. Hali ni tete sana!

01/03/2018 10:23

Shirikisho la Mashirika ya Misaada ya Kanisa Katoliki Kimataifa, Caritas Internationalis linasema kwa sasa hali ni tete sana nchini DRC kutokana na vita, ghasia, kinzani na mipasuko ya kijamii kiasi kwamba, kuna maelfu ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na watu wanaendelea kuuwawa!

Baraza la Maaskofu Katoliki DRC linataka: uhuru, usalama na demokrasia ya kweli!

Baraza la Maaskofu Katoliki DRC linaitaka Serikali iliyoko madarakani kuhakikisha kwamba, watu wanakuwa na uhuru wa kujieleza, wanapatiwa ulinzi na usalama wa maisha na mali zao pamoja na kuwa na demokrasia inayozingatia utawala wa sheria.

Tamko la Baraza la Maaskofu Katoliki DRC: Uhuru, Usalama & Demokrasia

21/02/2018 07:20

Baraza la Maaskofu Katoliki DRC katika tamko lake kuhusu hali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi nchini mwao, linapenda kukazia kwa namna ya pekee kabisa uhuru wa watu kujieleza kama sehemu ya haki zao msingi; ulinzi na usalama wa raia na mali zao pamoja na demokrasia inayoheshimu utawala wa sheria.

Askofu mkuu Fridolin Ambongo Besungu ateuliwa kuwa Askofu mwandamizi Jimbo kuu la Kinshasa, DRC.

Askofu mkuu Fridolin Ambongo Besungu ateuliwa na Papa Francisko kuwa Askofu mwandamizi mrithi wa Jimbo kuu la KInshasa, DRC.

Askofu mkuu Fridolin Ambongo Besungu ateuliwa kuwa Askofu mwandamizi

06/02/2018 16:21

Askofu mkuu Fridolin Ambongo Besungu ameteuliwa kuwa Askofu mwandamizi mrithi wa Jimbo kuu la Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo. Huyu anatarajiwa kumrithi Kardinali Laurenti Monswengo Pasinya, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Kinshasa nchini DRC.

Papa Francisko: Kanisa nchini DRC linaunga mkono mchakato wa haki, amani na upatanisho wa kitaifa

Papa Francisko: Kanisa nchini DRC linaunga mkono mchakato wa haki, amani na maridhiano kati ya watu.

Papa Francisko: DRC jengeni msingi wa haki, amani na maridhiano!

24/01/2018 12:59

Baba Mtakatifu Francisko anaitaka familia ya Mungu nchini DRC kuhakikisha kwamba, inajenga na kudumisha utamaduni wa watu kukutana ili kuimarisha misingi ya haki, amani, upendo na maridhiano kati ya watu. Kanisa Katoliki linapania ustawi, maendeleo na mafao ya wananchi wote wa DRC.

Baraza la Maaskofu Katoliki DRC lina laani vikaliukatili na kufuru zilizofanywa na Serikali ya Rais Josefu Kabila dhidi ya wananchi wake!

Baraza la Maaskofu Katoliki DRC lina laani vikali ukatili na kufuru iliyofanywa na Serikali ya Rais Josefu Kabila dhidi ya watu wake.

Kardinali Monsengwo Pasinya alaani ukatili wa Serikali ya Rais Kabila

03/01/2018 10:54

Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo, DRC limelaani ukatili uliofanywa na vikosi vya ulinzi na usalama dhidi ya waandamanaji waliokuwa wana dai haki zao msingi pamoja na kufuru iliyofanywa na wanajeshi kwenye nyumba za Ibada wakati wa kupambana na wananchi.

Kanisa nchini DRC litaendelea kutangaza Injili ya haki, amani, utawala wa sheria mintarafu mwanga wa Injili na Mafundisho Jamii ya Kanisa.

Kanisa nchini DRC litaendelea kutangaza na kushuhudia: Injili ya haki, amani na utawala wa sheria mintarafu mwanga wa Injili na Mafundisho Jamii ya Kanisa.

Maaskofu Katoliki DRC: Utekaji nyara na mauaji ya viongozi wa Kanisa

29/09/2017 10:32

Machafuko ya kisiasa nchini DRC yamepelekea baadhi ya viongozi wa Kanisa kutekwa nyara, kuuwawa na hata wakati mwingine mali ya Kanisa kuharibiwa vibaya kwa misingi ya kisiasa. Lakini, Kanisa litaendelea kutangaza na kushuhudia: haki, amani, utawala wa sheria mintarafu mwanga wa Injili ya Kristo!

Ni matumaini ya Baraza la Maskofu Katoliki DRC kwamba, uchaguzi mkuu utaweza kufanyika mwaka 2017.

Ni matumaini ya Baraza la Maaskofu Katoliki kwamba, uchaguzi mkuu utaweza kufanyika nchini humo kwa mwaka 2017.

DRC: Je, kweli uchaguzi utafanyika nchini humo kwa Mwaka 2017?

08/07/2017 16:26

Familia ya Mungu inaendelea kujiuliza ikiwa kweli DRC itaweza kufanya uchaguzi wake mkuu kama ilivyokuwa imepangwa? Hii inatokana na ukweli kwamba, mchakato wa zoezi zima la upigaji kura ulionekana kana kwamba, usimama! Baraza la Maaskofu Katoliki DRC lina matumaini ya kufanyika uchaguzi mkuu!