Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baraza la Kipapa Ibada na Nidhamu ya Sakramenti

Papa Francisko: Kanisa ni Mama na Mchumba mwaminifu wa Kristo Yesu!

Papa Francisko: Kanisa ni Mama na Mchumba mwaminifu wa Kristo Yesu!

Papa Francisko: Kanisa ni Mama na Mchumba mwaminifu wa Kristo!

21/05/2018 14:58

Kanisa kwa mara ya kwanza tarehe 21 Mei 2018, limeadhimisha Siku kuu ya Bikira Maria Mama wa Kanisa tangu iliporidhiwa na Baba Mtakatifu Francisko ambaye katika mahubiri yake amekazia kwa namna ya pekee kabisa dhana ya Kanisa kama Mama na Mchumba mwaminifu wa Kristo Yesu!

Sherehe ya Bikira Maria Mama wa Kanisa inaanza kuadhimishwa rasmi mwaka 2018 kwa Kanisa zima, Jumatatu baada ya Sherehe za Pentekoste.

Sherehe ya Bikira Maria Mama wa Kanisa inaanza kuadhimishwa rasmi kwa Kanisa zima, Jumatatu mara baada ya Sherehe za Pentekoste kwa mwaka 2018.

Sherehe ya Bikira Maria Mama wa Kanisa kuanza kuadhimishwa mwaka 2018

04/04/2018 07:50

Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa linafafanua kwamba, maadhimisho ya Sherehe ya Bikira Maria Mama wa Kanisa iliyoridhiwa na Baba Mtakatifu Francisko yanaanza rasmi mwaka 2018 na kwamba, hata kama kuna kumbu kumbu za hiyari, kipaumbele cha kwanza kiwe kwa B.Maria.

Tamko: Siku kuu ya Bikira Maria Mama wa Kanisa kuadhimishwa Jumatatu baada ya Sherehe ya Pentekoste.

Tamko: Siku kuu ya Bikira Maria Mama wa Kanisa kuadhimishwa kuanzia sasa Jumatatu baada ya Sherehe ya Pentekoste kwa kutambua dhima ya Bikira Maria katika kazi ya ukombozi.

TAMKO: Kuhusu Siku kuu ya Bikira Maria Mama wa Kanisa

05/03/2018 06:41

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia kwamba, kuanzia sasa Siku kuu ya Bikira Maria Mama wa Kanisa itakuwa inaadhimishwa na Kanisa zima, Jumatatu mara baada ya Sherehe ya Pentekoste kwa kutambua dhima na mchango wa Bikira Maria Mama wa Mungu katika historia nzima ya ukombozi.

Papa Francisko anapania kuendeleza mchakato wa mabadiliko ya Liturujia kadiri ya Mataguso mkuu wa Pili wa Vatican.

Papa Francisko anapania kuendelea mchakato wa mageuzi yaliyoanzishwa na Mababa wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican kwa kukazia umuhimu wa Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa.

Papa Francisko na mwendelezo wa mchakato wa mabadiliko ya Kiliturujia

13/09/2017 11:18

Mababa wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican walikazia umuhimu wa Liturujia katika maisha ya Kanisa! Wakaweka Kanuni za jumla za marekebisho na ukuzaji wa Liturujia Takatifu ambayo ni njia ya Mungu kutukuzwa na mwanadamu kutakatifuzwa kwa njia ya Kristo Yesu, Kuhani mkuu wa Agano Jipya!

Baraza la Kipapa la Ibada, Nidhamu na Sakramenti za Kanisa linayo dhamana ya kutambua na kuthibitisha vitabu vya Liturujia ya Kanisa.

Baraza la Kipapa la Ibada, Nidhamu na Sakramenti za Kanisa linayo dhamana ya kutambua na kuthibitisha tafsiri ya vitabu vinavyotumika kwa Liturujia ya Kanisa.

Tafsiri ya vitabu vya Liturujia ya Kanisa lazima vithibitishwe kwanza

13/09/2017 10:50

Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa limepewa dhamana na Mama Kanisa ya kutambua "recognitio" na kuthibitisha "Confirimatio" tafsiri ya vitabu vyote vinavyotumika katika maadhimisho ya Liturujia ya Kanisa baada ya kufanyiwa kazi na Mabaraza ya Maaskofu na Maaskofu mahalia!

Watengenezaji wa hostia na divai inayotumika kwenye liturujia ya Kanisa wawe waaminifu na wadilifu kwa kuzingatia ubora unaotakiwa.

Watengenezaji wa hostia na divai inayotumika kwa ajili ya maadhimisho ya Fumbo la Ekaristi takatifu wanapaswa kuwa waaminifu na waadili ili kuzingatia ubora unaotakiwa na Mama Kanisa kwa ajili ya maadhimisho haya.

Angalisho juu ya utengenezaji wa hostia na divai kwa ajili ya Ibada!

10/07/2017 10:35

Kutokana na kukua kwa biashara na soko huria katika masuala mbali mbali, Baraza la Kipapa la Nidhamu na Sakramenti za Kanisa limewaandikia Maaskofu barua ya kuwa makini zaidi na hostia pamoja na divai inayotumika kwa ajili ya maadhimisho ya Fumbo la Ekaristi Takatifu ili ziwe na ubora unaotakiwa!