Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko nchini Chile 2018

Papa Francisko akiwa njiani kurejea mjini Vatican ametuma salam na matashi mema kwa viongozi wakuu wa nchi na serikali alimopitia.

Papa Francisko akiwa njiani kurejea mjini Vatican baada ya kuhitimisha hija yake ya kitume huko Amerika ya kusini, Jumatatu tarehe 22 Januari 2018 amewatumia wakuu wa serikali na nchi salam na matashi mema.

Papa Francisko atuma salam na matashi mema kwa wakuu wa nchi

23/01/2018 13:54

Baba Mtakatifu Francisko akiwa njiani kurejea tena mjini Vatican mara baada ya kuhitimisha hija yake ya kitume, amewatumua ujumbe wa amani na matashi mema wakuu mbali mbali wa nchi ambamo amepitia wakati akirejea kutoka huko Amerika ya Kusini ambako ameshuhudia imani katika matendo!

Papa Francisko amewasili tayari nchini Perù kwa ajili ya hija yake ya kitume inayoongozwa na kauli mbiu "Umoja wa Matumaini"

Papa Francisko amewasili tayari mjini Lima, nchini Perù tayari kuanza hija yake ya kitume inayoongozwa na kauli mbiu "Umoja wa matumaini".

Papa Francisko tayari "ametinga timu" nchini Perù kwa kishindo!

19/01/2018 15:16

Baba Mtakatifu Francisko amewasili nchini Perù, Alhamisi tarehe 18 Januari 2018 tayari kuanza hija yake ya kitume inayoongozwa na kauli mbiu "Umoja wa Matumaini". Akiwa njiani kuelekea Jimbo kuu la Lima, Perù, ameishukuru familia ya Mungu nchini Chile kwa mapokezi makubwa waliyompatia!

Papa Francisko anawashukuru wadau mbali mbali waliojisadaka usiku na mchana ili kufanikisha hija yake ya kitume nchini Chile.

Papa Francisko anawashukuru wadau mbali mbali waliojisadaka usiku na mchana ili kuhakikisha kwamba, anafanikisha hija yake ya kitume nchini Chile kuanzia tarehe 15 hadi tarehe 18 Januari 2018.

Papa Francisko anawashukuru wote waliojisadaka kwa ajili ya hija yake

18/01/2018 15:42

Baba Mtakatifu Francisko anawashukuru viongozi wa Kanisa na Serikali pamoja na umati mkubwa wa watu wa Mungu waliojisadaka usiku na mchana ili kuhakikisha kwamba, hija yake ya kitume inafanikiwa huko nchini Chile kwa kujenga utamaduni wa watu kukutana na kuadhimisha Mafumbo ya Kanisa.

Papa Francisko asema, vijana ni chachu ya mageuzi ya kijamii, upyaisho wa Kanisa na kiini cha maisha na utume wa Kanisa.

Papa Francisko anasema vijana ni chachu ya mageuzi na upyaisho wa KanisA; Niini cha maisha na utume wa Kanisa.

Vijana ni chachu ya mageuzi na kiini cha maisha na utume wa Kanisa!

18/01/2018 08:15

Baba Mtakatifu Francisko anapenda kuwahakikishia vijana kwamba, wao ni sehemu muhimu sana ya mageuzi ya kijamii na chachu inayolipyaisha Kanisa! wao ni kiini cha maisha na utume wa Kanisa, ndiyo maana ameitisha Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana ili Kanisa liweze kujifunza kutoka kwa vijana!

Papa Francisko akutana na waathirika wa nyanyaso za kijinsia Chile!

17/01/2018 15:09

Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake kwa viongozi wa serikali, wanadiplomasia na viongozi wa vyama vya kiraia amekemea vikali na kulaani nyanyaso za kijinsia dhidi ya watoto wadogo zilizofanywa na viongozi wa Kanisa nchini Chile. Amekutana na waathirika wa nyanyaso hizi na kuwafariji!

 

Papa Francisko anawataka Maaskofu kujikita katika malezi ya wakleri, maisha na utume wa waamini walei pamoja na dhan aya Sinodi ili kujenga udugu.

Papa Francisko anawataka Maaskofu kujikita katika malezi ya wakleri wao; wito, maisha na utume wa waamini walei pamoja na kumwilisha dhana ya sinodi kama sehemu ya mchakato wa ujenzi wa udugu na umoja ndani ya Kanisa.

Papa: Maaskofu jikiteni zaidi katika malezi, maisha, utume na sinodi

17/01/2018 12:00

Baba Mtakatifu Francisko anawataka Maaskofu kuhakikisha kwamba, wanajielekeza zaidi katika malezi ya awali na endelevu ya wakleri wao ili kukabiliana na changamoto mamboleo; wakuze na kudumisha wito, maisha na utume wa waamini walei sanjari na kujenga dhana ya sinodi kielelezo cha udugu!

Papa Francisko anawataka wakleri na watawa kuiga mfano wa Mtume Petro kwa kutubu, kuongoka na kutakaswa na Kristo Yesu katika maisha na utume wao!

Papa Francisko anawataka wakleri na watawa kuiga mfano wa Mtume Petro aliyeteleza na kuanguka katika udhaifu wake, akasamehewa dhambi zake na kutakaswa kwa huruma ya Kristo, na hivyo kusonga mbele katika ushuhuda wa huduma kwa watu wa Mungu!

Petro mtume aliyeanguka, akasamehewa na kutakaswa awe mfano wa Kanisa

17/01/2018 11:06

Baba Mtakatifu Francisko anawataka wakleri na watawa kumwangalia Mtakatifu Petro, Mtume aliyeanguka kutokana na udhaifu wake wa kibinadamu kiasi hata cha kumkana Yesu; Petro, aliyesamehewa mapungufu yake na Petro mtume, aliyetakaswa kwa huruma ya Kristo Yesu, awe mfano wa kuigwa!

Baraza la Maaskofu Katoliki Chile linasikitishwa sana na uchomwaji wa Makanisa nchini humo!

Baraza la Maaskofu Katoliki Chile linasikitishwa sana na uchomwaji wa Makanisa nchini humo wakati huu, familia ya Mungu nchini humo inapojiandaa kumkaribisha Papa Francisko.

Maaskofu wasikitishwa na uchomwaji wa Makanisa nchini Chile!

14/01/2018 14:22

Baraza la Maaskofu Katoliki Chile limesikitishwa sana na wimbi la uchomwaji wa Makanisa, vitendo vinavyofanywa na kikundi cha watu wachache nchini humo, ambacho kinapaswa kutambua kwamba, watu wengi wanataka kujenga moyo wa umoja wa kitaifa, uzalendo na majadiliano!