Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baa la njaa

Bara la Afrika halina budi kuwekeza katika mchakato wa maendeleo endelevu na fungamani ya binadamu!

Bara la Afrika halina budi kuwekeza katika mchakato wa maendeleo endelevu na fungamani ya binadamu.

AMECEA: Wekezeni katika mchakato wa maendeleo endelevu na fungamani

22/07/2018 14:32

Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Endelevu na Fungamani ya Binadamu linawataka Mababa wa AMECEA kuhakikisha kwamba, wanawekeza zaidi katika sera na mikakati ya shughuli za kichungaji inayojikita katika huduma ya maendeleo endelevu na fungamani kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya wengi.

Nchi za ukanda wa Sahel ni Burkina Faso, Chad, Mali, Mauritania, Niger na Senegal zinakabiliwa na uhaba wa chakula kiasi cha kutisha

Nchi za ukanda wa Sahel ni Burkina Faso, Chad, Mali, Mauritania, Niger na Senegal zinakabiliwa na uhaba wa chakula kiasi cha kutisha

Njaa kubwa inakumba watu wa Afrika hasa katika kanda yote ya Sahel !

19/06/2018 14:23

Hali ya chakula eneo la Sahel inasikitisha kwa mujibu wa ombi lililotolewa mjini New York Marekani na mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu (OCHA),Bwana Mark Lowcock wakati akitoa maelezo kuhusu hali ya kibinadamu ilivyo kwa sasa katika eneo hilo. 

 

UNICEF: Vita, vurugu na kinzani za kijamii vimekuwa ni vyanzo vikuu vya maafa na majanga yanayowapata watoto sehemu mbali mbali za dunia.

UNICEF: Vita, vurugu na kinzani za kijamii ni vyanzo vikuu vya maafa na majanga yanayowapata watoto wengi duniani kiasi cha kurudisha nyuma maendeleo ya elimu, afya na ustawi wa wananchi wengi.

UNICEF: Vita ni chanzo kikuu cha maafa na majanga kwa watoto duniani

05/06/2018 11:55

UNICEF inasema vita sehemu mbali mbali za dunia imesababisha watoto wengi kushindwa kuendelea na masomo yao hali ambayo inasababisha kuongezeka kwa baa la ujinga na umaskini duniani; vita imeharibu miundo mbinu ya huduma ya afya kiasi kwamba, idadi ya watoto wanaofariki dunia inaongezeka!

Baraza la Maaskofu Katoliki Burkina Faso-Niger limekutana na Baba Mtakatifu Francisko pamoja na waandamizi wake wakati wa Hija ya Kitume mjini Vatican

Baraza la Maaskofu Katoliki Burkina Faso-Niger limekutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko pamoja na waandamizi wake wakati wa Hija yao ya Kitume mjini Vatican.

Changamoto za maisha na utume wa Kanisa Katoliki Burkina Faso-Niger

30/05/2018 09:41

Baraza la Maaskofu Katoliki Burkina Faso-Niger linasema, kati ya changamoto kubwa katika maisha na utume wa Kanisa katika nchi hizi ni majadiliano ya kidini na kiekumene; wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji; balaa la njaa, utapiamlo, umaskini na ujinga na utunzaji bora wa mazingira!

Baraza la Maaskofu Katoliki Congo Brazzaville linasema, kwa sasa hali ni tete sana nchini mwao kutokana na kinzani za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Baraza la Maaskofu Katoliki Congo Brazzaville linasema, hali ni tete sana nchini mwao kutokana na kinzani za kiuchumi, kisiasa na kijamii ambazo zimewatumbukiza wananchi wengi katika ombwe na hali ngumu ya maisha.

Maaskofu Katoliki Congo Brazzaville wasema, hali ni tete sana!

16/05/2018 10:49

Baraza la Maaskofu Katoliki Congo Brazzaville baada ya kukaa, kutafakari na kuchambua hali halisi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii nchini mwao wanadiriki kusema kwamba, kwa sasa hali ni tete sana kutokana na kukithiri kwa rushwa na ufisadi, hali ngumu ya maisha na kinzani zisizona tija!

Papa Francisko katika Ujumbe wake wa Pasaka kwa Mwaka 2018: Amani, Majadiliano, Upatanisho, Faraja, Matumaini, Utu na Heshima ya binadamu.

Papa Francisko katika Ujumbe wake wa Pasaka kwa Mwaka 2018: Urbi et Orbi anakazia: Amani, Haki, Majadiliano, Upatanisho, Faraja, Utu na Heshima ya binadamu.

Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa Pasaka 2018: "Urbi et Orbi"

01/04/2018 12:30

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake wa Pasaka kwa mwaka 2018 anawaombea watu waliokata tamaa matumaini; amani kwa wale wanaoogelea katika vita, kinzani na mipasuko ya kijamii; upatanisho, majadiliano, faraja kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi duniani!

Nchini Venezuela,watu wanashindwa kujikimu kupata hata mlo wa siku kutokana na hali mbaya ya kijamii,kisiasa na kiuchumi

Nchini Venezuela,watu wanashindwa kujikimu kupata hata mlo wa siku kutokana na hali mbaya ya kijamii,kisiasa na kiuchumi

Maaskofu Venezuela:Nchi imegeuka kuwa ngeni hata kwa raia wote!

22/03/2018 15:14

Tarehe 19 Machi ilikuwa ni sikukuu ya Mtakatifu Yosefu na hivyo Baraza la Maskofu wa Venezuela katika fursa hiyo wametuma ujumbe kwa watu wa Mungu na wenye mapenzi mema, zaidi wanakumbusha viongozi wote wa kisiasa,kijamii na kiuchumi kuwatendea wema watu wao, kwa mfano wa Yesu

 

Utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote ni wajibu wa familia ya Mungu kimaadili.

Utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote ni wajibu wa kimaadili wa familia yote ya Mungu.

WCC: Utunzaji bora wa mazingira ni wajibu wa wote kimaadili!

07/03/2018 14:30

Familia ya Mungu Barani Afrika inakabiliwa kwa kiasi kikubwa na athari za mabadiliko ya tabianchi yanayoendelea kusababisha mamilioni ya watu kutumbukia katika baa la umaskini, magonjwa, njaa, vita na kinzani za kijamii! Utunzaji bora wa mazingira ni wajibu wa kimaadili kwa watu wote!