Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Askofu Philip Anyolo

Askofu Cornelius Korir wa Jimbo la Eldoret nchini Kenya ameaga dunia tarehe 29 Oktoba  na mazishi yake yatafanyika tarehe 11 Novemba 2017

Askofu Cornelius Korir wa Jimbo la Eldoret nchini Kenya ameaga dunia tarehe 29 Oktoba na mazishi yake yatafanyika tarehe 11 Novemba 2017

Askofu Cornelius Korir wa Jimbo la Eldoret-Kenya ameaga dunia!

08/11/2017 10:30

Maaskofu Katoliki nchini Kenya wanaomboleza kifo cha marehemu Askofu Cornelius Arap Korir kilichotokea usiku wa tarehe 29 Oktoba 2017 nyumbani kwake huko Eldoret.Amethibitisha kifo hicho cha ghafla Mwenyekiti wa (KCCB ) Askofu Philip Anyolo mazishi yake ni tarehe 11Nov 2017

 

 

Maaskofu Katoliki Kenya: Jengeni utamaduni wa kuheshimu utawala wa sheria!

Maaskofu Katoliki Kenya: Jengeni utamaduni wa kutekeleza kwa dhati na kwa hiyari utawala was sheria.

Familia ya Mungu nchini Kenya jengeni utamaduni wa utawala wa sheria

07/09/2017 16:33

Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya linawaalika wadau mbali mbali nchini Kenya kuhakikisha kwamba, wanatekeleza uamuzi wa Mahakama kuu ili kufanikisha uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 17 Oktoba 2017! Wazingatie sheria, kanuni na taratibu ili uchaguzi mkuu uwe ni huru na wa haki.

Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya linawataka wanasiasa kuganga na kutibu magonjwa ya utengano na mipasuko ya kisiasa na kkijamii.

Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya linawataka wananchi wa Kenya kuganga na kuponya madonda ya athari za uchaguzi mkuu maka 2017.

Uchaguzi Mkuu Nchini Kenya: Ponyeni makovu ya utengano, jengeni umoja

16/08/2017 14:20

Mchakato mzima wa uchaguzi mkuu nchini Kenya umesababisha mpasuko mkubwa miongoni mwa familia ya Mungu nchini Kenya kwa misingi ya ushabiki wa kisiasa, ukabila na umajimbo; mambo ambayo hayana tija wala mashiko kwa ustawi na maendeleo ya wananchi wengi wa Kenya.

 

Maaskofu Katoliki Kenya wasema, wananchi wanakabiliwa na maafa ya njaa kutokana na ukame wa kutisha!

Maaskofu Katoliki Kenya wasema, wananchi wanakabiliwa na baa la njaa kutokana na ukame wa kutisha, kumbe, kuna haja kwa Serikali kutangaza kwamba, Kenya inakabiliwa na maafa ya njaa ili iweze kupatiwa msaada na Jumuiya ya Kimataifa.

Maaskofu Kenya: Watu wanakufa kwa baa la njaa!

09/02/2017 13:24

Taarifa kutoka majimbo mbali mbali ya Kanisa Katoliki nchini Kenya inaonesha kwamba, kuna idadi kubwa ya familia ya Mungu nchini Kenya inayoteseka kwa baa la njaa kutokana na ukame wa kutisha, mwaliko kwa Kenya kutangaza Kenya kuwa inakabiliwa na maafa ya njaa ili iweze kupata msaada!

Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya linawaomba wafanyakazi sekta ya afya kusitisha mgomo ili kuokoa maisha ya wananchi!

Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya linawaomba wafanyakazi katika sekta ya afya kusitisha mgomo wao ili kuokoa maisha ya wagonjwa hasa vijijini.

Sitisheni mgomo, wananchi wanakufa kwa magonjwa!

19/01/2017 15:51

Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya kwa mara nyingine tena limewaomba wafanyakazi katika sekta ya afya kusitisha mgomo wao ili kuokoa maisha ya wananchi hasa wagonjwa maskini vijijini! Wanaiomba Serikali kufanya majadiliano ili kumaliza mgogoro huu ambao unahatarisha maisha ya wagonjwa!

Baraza la Maaskofu Kenya linasema, Serikali na vyama vya upinzani wanaweza bado kuanzisha mchakato wa majadiliano ili kufanikisha uchaguzi mkuu 2017.

Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya linasema, bado kuna nafasi kwa Serikali na vyama vya upinzani kufanya majadiliano katika ukweli na uwazi ilikufanikisha mchakato wa uchaguzi mkuu nchini Kenya kwa mwaka 2017.

Maaskofu Kenya wasema: Serikali na wapinzani wajadiliane!

12/01/2017 14:53

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya hivi karibuni ametia mkwaju kwenye muswada wa Mabadiliko ya Sheria za Uchaguzi ya Mwaka 2016 na kuwa sasa Sheria itakayotumika kwa ajili ya mchakato wa uchaguzi mkuu nchini Kenya kwa mwaka 2017, ingawa sheria hii inapingwa na vyama vya upinzani!

 

Ajali mbaya ya barabarani yasababisha watu zaidi ya 30 kupoteza maisha huko Naivasha, nchini Kenya.

Ajali mbaya ya barabarani yasabababisha zaidi ya watu 30 kupoteza maisha yao huko Naivasha, Kenya.

Watu zaidi ya 30 wamefariki kwa ajali ya barabarani Naivasha, Kenya

14/12/2016 08:44

Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya linatuma salam za rambi rambi kwa watu wote walioguswa na msiba mzito wa ajali barabarani huko Naivasha ambayo imepelekea watu zaidi ya 30 kupoteza maisha yao pamoja na uharibifu mkubwa wa magari na miundo mbinu ya barabara! Watu wawe makini zaidi!

 

Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya limetuma salama za rambi rambi na mshikamano kwa Familia ya Mungu nchini humo.

Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya limetuma salam za rambi rambi kwa familia ya Mungu nchini Kenya kutokana na mauaji ya kinyama yaliyofanyika nchini Somalia.

Maaskofu Katoliki Kenya watuma salam za rambi rambi kwa familia ya Mungu Kenya

20/01/2016 17:17

Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya limesikitishwa sana na mauaji ya askari waliokuwa nchini Somalia ili kulinda usalama wa raia na mali zao. Maaskofu wametuma salam za rambi rambi na mshikamano kwa famili zote zilizoguswa na kutikiswa na mauaji hayo ya kigaidi.