Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi

AMECEA: Kanisa Barani Afrika liendelee kujikita katika misingi ya haki, amani na maridhiano kati ya watu.

AMECEA: Kanisa Barani Afrika liendelee kujikita katika mchakato wa haki, amani na maridhiano kati ya watu ili kuchochea maendeleo endelevu yanayogusa mahitaji ya mtu mzima: kiroho na kimwili.

Yanayoendelea kujiri kwenye mkutano wa 19 wa AMECEA, 2018, Addis Ababa

20/07/2018 15:21

Baba wa AMECEA katika mkutano wao wa 19 wanaendelea kukazia umuhimu wa Kanisa kujikita katika mchakato wa haki, amani na upatanisho ndani na nje ya Bara la Afrika, ili kukuza na kudumisha: utu, heshima na haki msingi za binadamu na kama kielelezo makini cha mshikamano wa watu wa Mungu!

Ufukara wa Kiinjili uwawezeshe Wakristo kutangaza na kushuhudia Injili kwa watu wa Mataifa.

Ufukara wa kiinjili uwawezeshe wakristo kutangaza na kushuhudia Injili ya Kristo kwa watu wa Mataifa!

Ufukara wa Kiinjili uwawajibishe kutangaza na kushuhudia Injili!

13/07/2018 07:11

Yesu Kristo aliyeteswa, akafa na kufufuka kwa wafu ndicho kiini cha Habari Njema ya Wokovu inayopaswa kutangazwa na kushuhudiwa katika uhalisia wa maisha ya Wakristo! Kumbe, ufukara wa Kiinjili ni nyenzo msingi katika mchakato wa kumwilisha Injili ya upendo kwa maskini na wahitaji zaidi!

Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi ateuliwa kuwa Askofu mkuu mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo kuu la Dar es Salaam.

Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi ameteuliwa kuwa Askofu mkuu mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo kuu la Dar es Salaam.

Askofu mkuu Ruwaichi ateuliwa kuwa Askofu mwandamizi mrithi, Dar!

21/06/2018 12:01

Baba Mtakatifu Francisko ameteua Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi kuwa Askofu mkuu mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo kuu la Dar es Saalam, Tanzania. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Ruwaichi alikuwa ni Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Mwanza! Hii ndiyo Breaking News!

Viongozi wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania wanatambua changamoto, fursa na matatizo katika malezi na majiundo ya kipadre: Yanashughulikiwa!

Viongozi wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania wanatambua matatizo, changamoto na fursa za malezi ya wuto wa kipadre, na kwamba, wameanza kuzivalia njuga ili kuandaa mwongozo wa malezi ya kipadre kitaifa.

Changamoto za malezi na majiundo ya kikasisi nchini Tanzania!

23/04/2018 14:51

Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 150 ya Uinjilishaji Tanzania Bara sanjari na Mwaka wa Padre Tanzania ulioadhimishwa mwaka 2017 kama kumbu kumbu ya Jubilei ya Miaka 100 tangu Mapadre wa kwanza wazalendo kuwekwa wakfu. Hii ni nafasi ya kutafakari kuhusu; wito, utume na maisha ya kipadre!

Watanzania wanapaswa kujenga na kudumisha: Hekima, Umoja na Amani nguzo za taifa!

Watanzania wanapaswa kujenga na kudumisha: Hekima, Umoja na Amani nguzo za taifa.

Yaliyojiri Askofu mkuu Isaac Amani Massawe aliposimikwa Arusha

14/04/2018 16:50

Maadhimisho ya Ibada ya Masifu ya Jioni, Jumapili ya Huruma ya Mungu na hatimaye, Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kumsimika Askofu Mkuu Isaac Amani Massawe wa Jimbo kuu la Arusha yalisheheni utajiri wa busara na hekima zilizotolewa na wahusika mbali mbali katika tukio hili la kihistoria!

Askofu mkuu Josaphat Louis Lebulu kwa miaka 49 amelitumikia Kanisa kama Padre na miaka 39 kama Askofu, Jimbo la Same na Jimbo kuu la Arusha.

Askofu mkuu Josaphat Louis Lebulu amelitumikia Kanisa kama Padre kwa miaka 49 na kama Askofu takribani miaka 49 huko Jimbo Katoliki la Same na hatimaye, Jimbo kuu Katoliki la Arusha, Tanzania.

Shukrani sana Askofu mkuu Lebulu! Shikamaneni na Askofu mkuu Amani

06/04/2018 09:16

Askofu mkuu mstaafu Josaphat Louis Lebulu wa Jimbo kuu Katoliki Arusha, Tanzania amelitumikia Kanisa kama padre kwa miaka 49 na katika dhamana ya Askofu kwa takribani miaka 39. Amekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Same na hatimaye, Jimbo kuu Katoliki la Arusha! Sasa anang'atuka ili akasali zaidi! 

Kanisa Katoliki Tanzania linaadhimisha Pasaka ya 150 tangu wainjilishwe! Matendo makuu ya Mungu!

Kanisa Katoliki Tanzania linaadhimisha Pasaka ya 150 tangu wainjilishwe!

Askofu mkuu Ruwaichi: Ujumbe wa Pasaka na Miaka 150 ya Ukatoliki

31/03/2018 12:02

Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi wa Jimbo Kuu la Mwanza katika uujumbe wake wa Pasaka kwa mwaka 2018 anamwomba Mwenyezi Mungu awapatie Wakristo wote nchini Tanzania nguvu, uthubutu na furaha ya kumshangilia Kristo Mfufuka bila woga, kigugumizi na wala bila ubaridi wowote ule!

Askofu mkuu Ruwaichi: Alhamisi Kuu ni Siku ya: Shukrani, Kuchunguza ahadi za Kipadre katika unyofu na ukweli na kuombea, kukuza na kudumisha miito.

Askofu mkuu Ruwaichi: Alhamisi kuu ni Siku ya: shukrani kwa zawadi ya wito wa kipadre; ni muda wa kuchunguza dhamiri kuhusu ahadi za kipadre katika ukweli na unyenyekevu; ni siku ya kuombea, kukuza na kudumisha miito!

Askofu mkuu Ruwaichi: Alhamisi Kuu: Shukrani, uaminifu na miito!

29/03/2018 13:55

Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi wa Jimbo Kuu la Mwanza, Tanzania anasema, Alhamisi kuu ni muda muafaka kwa Mapadre kumshukuru Mungu kwa zawadi, wito na maisha ya kipadre; ni wakati wa kutafakari katika ukweli na unyofu ahadi zao za kipadre na mwisho kuombea, kukuza na kudumisha miito.