Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Askofu mkuu Paul Richard Gallagher

Vatican: Jumuiya ya Kimataifa haina budi kujielekeza zaidi katika utamaduni wa amani sanjari na maboresho ya maisha ya watu kwa kukazia maendeleo!

Vatican: Jumuiya ya Kimataifa haina budi kujikita katika utamaduni wa amani na maboresho ya maisha ya watu kwa kuzingatia kanuni msingi za maendeleo endelevu ya binadamu!

Vatican: Jumuiya ya Kimataifa ijielekeze katika amani na maisha bora

26/09/2017 10:27

Askofu mkuu Paul Richard Gallagher anasema, Jumuiya ya Kimataifa haina budi kujielekeza zaidi katika mchakato wa ujenzi wa utamaduni wa amani duniani sanjari na marekebisho ya maisha ya watu kwa kujikita katika utu, heshima, ustawi na maendeleo ya wengi; kwa kuzingatia haki msingi za binadamu!

 

Jumuiya ya Kimataifa ina wajibu na dhamana ya kulinda na kudumisha uhuru wa kuabudu na kidini duniani.

Jumuiya ya Kimataifa ina dhamana na wajibu wa kukuza na kudumisha uhuru wa kidini na kuabudu.

Jumuiya ya Kimataifa ina dhamana ya kulinda uhuru wa kuabudu!

25/09/2017 09:56

Vitendo vya kigaidi, mauaji ya kimbari, utekaji nyara na unyanyasaji wa watu kijinsia; uporaji na uharibifu wa nyumba za ibada na makazi ya watawa na wakleri; taasisi za elimu na afya zinazomilikiwa na Makanisa ni kati ya mambo yanayochefua uhuru wa kidini na kuabudu duniani!

Ili amani ya kweli iweze kupatikana nchini Siria, haki msingi, utu na heshima ya binadamu vinapaswa kusingatiwa.

Ili amani ya kweli iweze kupatikana nchini Siria kuna haja ya kudumisha haki msingi za binadamu, uhuru wa kuabudu, utawala wa sheria, utu na heshima ya binadamu.

Zingatieni haki msingi, utu na heshima ya binadamu ili kupata amani

23/09/2017 16:43

Askofu mkuu Paul R. Gallagher anasema ili amani ya kweli iweze kupatikana nchini Siria kuna haja ya kujikita katika kudumisha haki msingi za binadamu, uhuru wa kuabudu, utu na heshima ya binadamu na kwamba, mambo yote haya yanapaswa kupatiwa ufumbuzi kwa njia ya majadiliano katika ukweli.

Vatican yatia sahihi kwenye Mkataba wa Kimataifa unaopiga rufuku silaha za kinyuklia duniani!

Vatican yatia sahihi kwenye Mkataba wa Kimataifa unaopiga rufuku kisheria silaha za kinyuklia.

Vatican yatia sahihi Mkataba wa Kimataifa dhidi ya Silaha za Nyuklia

22/09/2017 15:40

Askofu mkuu Paul Richard Gallagher anasema, Vatican imeamua kutia sahihi kwenye Mkataba wa Kimataifa unaopiga rufuku silaha za kinyuklia unapania kukuza utamaduni wa kulinda na kudumisha amani, mshikamano na maridhiano kati ya watu wa Mataifa sanjari na maendeleo endelevu ya binadamu!

Vita, ghasia, machafuko na mipasuko ya kijamii inaendelea kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao.

Vita, ghasia, machafuko na mipasuko ya kisiasa inaendelea kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao.

Vatican yasikitishwa sana na machafuko ya kisiasa huko Afrika ya Kati

21/09/2017 16:42

Vita, ghasia, machafuko na mipasuko ya kijamii, kisiasa na kidini ni kati ya mambo yanayoendelea kuchangia kuibuka kwa wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji katika Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati. Kuna watu wanaendelea kuwawa, wengine wengi hawana makazi ya kudumu!

Biashara ya binadamu, utumwa mamboleo na mifumo yake yote ni udhalilishaji wa utu na heshima ya binadamu!

Biashara ya binadamu na utumwa mamboleo ni udhalilishaji wa utu na heshima ya binadamu.

Utumwa mamboleo ni kashfa dhidi ya utu na heshima ya binadamu!

21/09/2017 16:01

Baba Mtakatifu Francisko katika maisha na utume wake kama Khalifa wa Mataifa Petro anaendelea kutoa kipaumbele cha pekee katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya binadamu, utumwa mamboleo na mifumo yake yote kwani inadhalilisha: haki msingi, utu na heshima ya binadamu!

Amani na usalama wa Jumuiya ya Kimataifa, wakimbizi na wahamiaji na hatima ya Wakristo Mashariki ya Kati ni changamoto za kimataifa!

Amani na usalama wa Jumuiya ya Kimataifa; wakimbizi na wahamiaji pamoja na hatima ya Wakristo huko Mashariki ya Kati ni kati ya changamoto za Jumuiya ya Kimataifa.

Askofu mkuu Gallagher: Changamoto za Jumuiya ya Kimataifa: Usalama!

18/09/2017 09:21

Askofu mkuu Paul Richard Gallagher anasema, Jumuiya ya Kimataifa kwa sasa inakabiliwa na wasi wasi mkubwa wa kutoweka kwa amani kutokana na vitisho vya kijeshi na majaribio ya makombora ya masafa marefu linalofanywa na Korea ya Kaskazini; wakimbizi na hatima ya Wakristo huko Mashariki ya Kati

Akiwa nchini Iran Askofu Mkuu P. Gallager, alipata mlo wa mchana na Waziri wa Biashara ya nchi za nje Bw. Zarif

Asubuhi ya tarehe 6 Askofu Mkuu Gallager na wengine walikutana na Waziri wa Biashara ya nchi za nje Zarif na baadaye kupata chakula cha mchana na waziri,

Ziara ya Ask. Mkuu Paul R. Gallagher katika nchi ya Iran 5-9 Sept

11/09/2017 15:26

Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican,alianza ziara katika nchi ya Iran kuanzia tarehe 5-9 Septemba. Askofu Mkuu aliwasiri mjini Teharan 5 Septemba akisindikizwa na Monsinyo I. Paul Strejac,mshauri wa Ubalozi katika kitengo cha Mahusiano ya nchi za nje