Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya, Jimbo kuu la Dodoma

Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya hivi karibuni ametabaruku Kanisa la Parokia ya Mt. Gemma Galgan, Nkuhungu, Jimbo kuu la Dodoma.

Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya wa Jimbo kuu la Dodoma, Tanzania hivi karibuni ametabaruku Kanisa la Parokia ya Mt. Gemma Galgan, Nkuhungu na kutoa Sakramenti ya Kipaimara kwa waamini 310.

Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya atabaruku Kanisa la Parokia ya Nkuhungu

27/01/2018 13:53

Katika maadhimisho ya Sherehe ya Tokeo la Bwana, maarufu kama Epifania, kwa mwaka 2018, Askofu mkuu Beatus Kinyaiya alitabaruku Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Gemma Galgan, Nkuhungu, Jimbo kuu la Dodoma, Tanzania pamoja na kutoka Sakramenti ya Kipaimara kwa Wakristo 310.

Sherehe ya Noeli na Mwaka Mpya 2018 iwe ni fursa ya kukazia misingi ya haki, amani na maridhiano kati ya watu!

Sherehe ya Noeli na Mwaka 2018 iwe ni fursa ya kukazia misingi ya haki, amani na maridhiano kati ya watu wa Mataifa.

Familia ya Mungu nchini Tanzania dumisheni: haki, amani na maridhiano

30/12/2017 14:39

Kipindi cha Noeli na Mwaka Mpya 2018 iwe ni fursa kwa familia ya Mungu kujenga na kudumisha utamaduni wa haki, amani na maridhiano; mambo msingi katika kusimamia haki msingi za binadamu, umoja na mshikamano wa kitaifa, chachu muhimu sana katika mchakato mzima wa maendeleo ya watu!

 

Uzinduzi wa Parokia mpya ya Theresa wa Mtoto Yesu, Jimbo kuu la Dodoma unapania kusogeza huduma za kichungaji kwa waamini.

Uzinduzi wa Parokia mpya ya Theresa wa Mtoto Yesu unalenga kusogeza huduma za kichungaji kwa familia ya Mungu katika eneo hili anasema Askofu mkuu Beatus Kinyaiya.

Parokia ya Theresa wa Mtoto Yesu, Jimbo kuu Dodoma: kitovu cha utume!

11/10/2017 07:38

Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya wa Jimbo kuu la Dodoma, hivi karibuni amezindua Parokia mpya ya Theresa wa Mtoto Yesu inayopaswa kuwa ni kitovu cha maisha na utume wa Kanisa katika maadhimisho ya Sakramenti za Kanisa, Katekesi, Tafakari na Matendo ya huruma: kiroho na kimwili!

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania lina laani vurugu, mauaji na uvunjifu wa amani unaojitokeza nchini humo.

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania lina laani vurugu na mauaji yanayoendelea nchini humo kwani huu si utamaduni wa watanzania!

Tamko la Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania kuhusu vurugu na mauaji

11/09/2017 15:46

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania lina laani kwa nguvu zote matendo yote ya vurugu, mauaji na uvunjifu wa amani. Wanatamani kuona wale wote walio nyuma ya matukio haya ya vurugu, mauaji, utekwaji na utesaji wanatafutwa na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria!

 

Askofu mkuu Beatus Kinyaiya, tarehe 13 Agosti 2017 ametoa Kipaimara kwa waamini 88 na Kubariki nyumba ya Mapadre wa Parokia ya B.M.Mama wa Damu Azizi

Askofu mkuu Beatus Kinyaiya, tarehe 13 Agosti 2017 ametoa Sakramenti ya Kipaimara kwa waamini 88 pamoja na kubariki nyumba ya Mapadre wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Damu Azizi ya Yesu, Jimbo kuu la Dodoma inayosimamiwa na Wamisionari wa Damu Azizi ya Yesu.

Askofu Mkuu Kinyaiya atoa Kipaimara kwa waamini 88 Jimbo kuu Dodoma

23/08/2017 10:58

Sherehe ya Bikira Maria kupalizwa mbinguni mwili na roho sanjari na kilele cha Mwaka wa Padre Tanzania imekuwa ni neema juu ya neema kwa familia ya Mungu Parokia ya Bikira Maria, Mama wa Damu Azizi ya Yesu kuimarishwa kwa Sakramenti ya Kipaimara pamoja na kubariki nyumba ya Mapadre!

Maadhimisho ya Mwaka wa Padre Tanzania: kutambua ukuu na utakatifu wa Daraja Takatifu ya Upadre

Maadhimisho ya Mwaka wa Padre Tanzania: kutambua na kuthamini ukuu wa DarajaTakatifu ya Upadre katika maisha na utume wa Kanisa.

Yaliyojiri kilele cha maadhimisho ya Mwaka wa Padre Tanzania!

16/08/2017 14:00

Maadhimisho ya Mwaka wa Padre nchini Tanzania imekuwa ni nafasi ya kutafakari: maisha, wito, dhamana, ukuu na utakatifu wa Daraja Takatifu ya Upadre katika maisha na utume wa Kanisa ndani na nje ya Tanzania. Kimekuwa ni kipindi cha kuhamasisha miito ya Daraja Takatifu ya Upadre!

Mwaka wa Padre Tanzania unahitimishwa tarehe 15 Agosti 2017: Sherehe ya Bikira Maria Kupalizwa Mbinguni mwili na roho!

Mwaka wa Padre Tanzania unahitimishwa rasmi tarehe 15 Agosti 2017 wakati wa Sherehe ya Bikira Maria Kupalizwa mbinguni.

Kilele cha Mwaka wa Padre Tanzania: Vigogo kutoka Vatican kushiriki

11/08/2017 14:09

Askofu mkuu Protase Rugambwa, Katibu Mwambata wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu ambaye pia ni Rais wa Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa pamoja na Askofu mkuu Marek Solczynski, Balozi wa Vatican nchini Tanzania wanashiriki katika kufunga Mwaka wa Padre nchini Tanzania!