Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Askofu mkuu Arthur Roche

Papa Francisko anapania kuendeleza mchakato wa mabadiliko ya Liturujia kadiri ya Mataguso mkuu wa Pili wa Vatican.

Papa Francisko anapania kuendelea mchakato wa mageuzi yaliyoanzishwa na Mababa wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican kwa kukazia umuhimu wa Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa.

Papa Francisko na mwendelezo wa mchakato wa mabadiliko ya Kiliturujia

13/09/2017 11:18

Mababa wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican walikazia umuhimu wa Liturujia katika maisha ya Kanisa! Wakaweka Kanuni za jumla za marekebisho na ukuzaji wa Liturujia Takatifu ambayo ni njia ya Mungu kutukuzwa na mwanadamu kutakatifuzwa kwa njia ya Kristo Yesu, Kuhani mkuu wa Agano Jipya!

Baraza la Kipapa la Ibada, Nidhamu na Sakramenti za Kanisa linayo dhamana ya kutambua na kuthibitisha vitabu vya Liturujia ya Kanisa.

Baraza la Kipapa la Ibada, Nidhamu na Sakramenti za Kanisa linayo dhamana ya kutambua na kuthibitisha tafsiri ya vitabu vinavyotumika kwa Liturujia ya Kanisa.

Tafsiri ya vitabu vya Liturujia ya Kanisa lazima vithibitishwe kwanza

13/09/2017 10:50

Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa limepewa dhamana na Mama Kanisa ya kutambua "recognitio" na kuthibitisha "Confirimatio" tafsiri ya vitabu vyote vinavyotumika katika maadhimisho ya Liturujia ya Kanisa baada ya kufanyiwa kazi na Mabaraza ya Maaskofu na Maaskofu mahalia!

Watengenezaji wa hostia na divai inayotumika kwenye liturujia ya Kanisa wawe waaminifu na wadilifu kwa kuzingatia ubora unaotakiwa.

Watengenezaji wa hostia na divai inayotumika kwa ajili ya maadhimisho ya Fumbo la Ekaristi takatifu wanapaswa kuwa waaminifu na waadili ili kuzingatia ubora unaotakiwa na Mama Kanisa kwa ajili ya maadhimisho haya.

Angalisho juu ya utengenezaji wa hostia na divai kwa ajili ya Ibada!

10/07/2017 10:35

Kutokana na kukua kwa biashara na soko huria katika masuala mbali mbali, Baraza la Kipapa la Nidhamu na Sakramenti za Kanisa limewaandikia Maaskofu barua ya kuwa makini zaidi na hostia pamoja na divai inayotumika kwa ajili ya maadhimisho ya Fumbo la Ekaristi Takatifu ili ziwe na ubora unaotakiwa!

Kwa mara ya kwanza waamini wa Kanisa Anglikani wamesali masifu ya jioni kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican tarehe 13 Machi 2017.

Kwa mara ya kwanza katika historia waamini wa Kanisa Anglikani wamesali Masifu ya jioni kwa heshima ya Mtakatifu Gregory mkuu kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Waanglikani wasali masifu ya jioni kwenye Kanisa kuu la Mt. Petro!

14/03/2017 09:48

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Kanisa Katoliki, waamini wa Kanisa Anglikani, Jumatatu tarehe 13 Machi 2017 wamepata nafasi ya kusali Masifu ya Jioni kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro kama njia ya kumuenzi Mtakatifu Gregory mkuu aliyekita katika Uinjilishaji na Uekumene wa huduma.

Papa Francisko anawahimiza Wakleri kuandaa vyema mahubiri yao kwa kujikita katika Biblia, Masomo ya Kiroho na Mafundisho Jamii ya Kanisa.

Papa Francisko anawahimiza Wakleri kuhakikisha kwamba, wanaandaa mahubiri yao kwa kujikita katika Maandiko Matakatifu, Masomo ya Kiroho na Mafundisho Jamii ya Kanisa.

Mwongozo wa mahubiri makini!

28/12/2016 08:27

Baba Mtakatifu Francisko katika Waraka wake wa Kitume "Furaha ya Injili" anakazia umuhimu wa mahubiri katika liturujia kama chemchemi ya furaha, faraja, amani, utulivu na upyaisho wa maisha ya kiroho na kiutu kwa kuzingatia kwamba Kanisa ni Mama na Mwalimu anayeheshimu ukweli na haki!

Siku kuu ya Mtakatifu Maria Magdalena: Siku ya shukrani kwa wanawake wanaojisadaka kwa ajili ya Kristo na Kanisa lake.

Siku kuu ya Mtakatifu Maria Magdalena ni siku ya shukrani kwa wanawake wanaojisadaka kwa Kristo na Kanisa lake.

Siku kuu ya Mt. Maria Magdalena: Siku ya shukrani kwa wanawake!

22/07/2016 15:25

Kwa mara ya kwanza katika historia Kanisa limeadhimisha Siku kuu ya Mtakatifu Maria Magdalena mtume wa mitume, shuhuda amini wa huruma na upendo wa Mungu katika maisha ya mwanadamu, siku ambayo pia imetumika kuwashukuru wanawake wanaojisadaka kwa ajili ya ushuhuda kwa Kristo.