Baba Mtakatifu Francisko amepokea taarifa ya uchunguzi wa nyanyaso za kijinsia zilizofanywa na baadhi ya viongozi wa Kanisa nchini Chile na kuonesha masikitiko yake makubwa kutokana na kuzama katika ombwe lililomfanya kushindwa kupembua hali kwa ufasaha na hivyo kusababisha mateso kwa watu
Papa Francisko amemtea na kumtuma Askofu mkuu Charles J. Scicluna wa Jimbo kuu la Malta kwenda Chile kusikiliza na kuchunguza shutuma dhidi ya Askofu Barros wa Jimbo Katoliki la Osorno, Chile, ili hukumu ya haki iweze kutendeka!
Baba Mtakatifu Francisko amemteua na kumtuma Askofu mkuu Charles Scicluna wa Jimbo kuu la Malta kwenda nchini Chile ili kusikiliza shutuma za unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto wadogo zinazomkabili Askofu Juan de la Cruz Barros Madrid, ili zijadiliwe na hukumu inayozingatia haki itolewe.
Baba Mtakatifu Francisko katika mahojiano maalum na waandishi wa habari akiwa anarejea mjini Vatican amezungumzia imani na ushuhuda wa upendo, changamoto na kufafanua kuhusu kashfa ya nyanyaso za kijinsia dhidi ya watoto wadogo nchini Chile.
Ushuhuda wa imani ya familia ya Mungu Amerika ya Kusini, ujasiri, moyo wa toba na wongofu wa ndani na ushuhuda wa nguvu ya Injili kwa wafungwa wanaotaka kuandika kurasa mpya, utunzaji wa mazingira na kashfa ya Karadima, vimepembuliwa na Papa Francisko karika mahojiano na wanahabari.
Mitandao ya kijamii: