Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

AMECEA

Askofu Charles Kasonde amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa AMECEA na Padre Anthony Makunde kuwa Katibu mkuu wa AMECEA.

Askofu Charles Kasonde amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa AMECEA na Padre Anthony Makunde kuwa Katibu mkuu wa AMECEA kwa kipindi cha miaka minne kuanzia sasa.

Viongozi wapya wa AMECEA: Askofu Charles Kasonde na Padre A. Makunde

24/07/2018 08:29

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu katoliki Afrika Mashariki na Kati, AMECEA limemchagua Askofu Charles Kasonde wa Jimbo Katoliki la Solwezi, Zambia kuwa Mwenyekiti mpya wa AMECEA kwa kipindi cha miaka minne. Katibu mkuu ni Padre Anthony Makunde, kutoka Jimbo Katoliki la Mbeya, Tanzania.

Kanisa Barani Afrika halina budi kujizatiti katika uinjilishaji mpya unaojikita kwenye ushuhuda wenye mvuto na mashiko!

Kanisa Barani Afrika halina budi kuwekeza katika mchakato wa uinjilishaji mpya unaojikita katika ushuhuda wenye mvuto na mashiko ili kuimarisha haki, amani na maridhiano kati ya watu!

AMECEA lindeni: Haki na Amani; Changamkieni Uinjilishaji mpya!

22/07/2018 14:58

Mababa wa AMECEA wametakiwa kuwekeza katika mchakato wa uinjilishaji mpya unaofumbatwa katika ushuhuda wenye mvuto na mashiko, ili kuhakikisha kwamba, kweli Kanisa linaendelea kuwa ni chombo na shuhuda wa misingi ya haki, amani na maridhiano kati ya watu Barani Afrika.

Bara la Afrika halina budi kuwekeza katika mchakato wa maendeleo endelevu na fungamani ya binadamu!

Bara la Afrika halina budi kuwekeza katika mchakato wa maendeleo endelevu na fungamani ya binadamu.

AMECEA: Wekezeni katika mchakato wa maendeleo endelevu na fungamani

22/07/2018 14:32

Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Endelevu na Fungamani ya Binadamu linawataka Mababa wa AMECEA kuhakikisha kwamba, wanawekeza zaidi katika sera na mikakati ya shughuli za kichungaji inayojikita katika huduma ya maendeleo endelevu na fungamani kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya wengi.

AMECEA: Kanisa Barani Afrika liendelee kujikita katika misingi ya haki, amani na maridhiano kati ya watu.

AMECEA: Kanisa Barani Afrika liendelee kujikita katika mchakato wa haki, amani na maridhiano kati ya watu ili kuchochea maendeleo endelevu yanayogusa mahitaji ya mtu mzima: kiroho na kimwili.

Yanayoendelea kujiri kwenye mkutano wa 19 wa AMECEA, 2018, Addis Ababa

20/07/2018 15:21

Baba wa AMECEA katika mkutano wao wa 19 wanaendelea kukazia umuhimu wa Kanisa kujikita katika mchakato wa haki, amani na upatanisho ndani na nje ya Bara la Afrika, ili kukuza na kudumisha: utu, heshima na haki msingi za binadamu na kama kielelezo makini cha mshikamano wa watu wa Mungu!

Askofu mkuu Protase Rugambwa: AMECEA msikubali kutumbukia katika ukabila na udini usiokuwa na mvuto wa mashiko kwa maendeleo ya watu wa Mungu.

Askofu mkuu Protase Rugambwa: Amewataka Mababa wa AMECEA kutokubali kutumbukizwa katika sera za ukabila na udini usiokuwa na mvuto wala mashiko kwa ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu Barani Afrika.

AMECEA: Msikubali ukabila na udini viwapekenyue na kusababisha maafa

17/07/2018 14:00

Askofu mkuu Protase Rugambwa, amewataka Mababa wa AMECEA kujenga na kudumisha umoja, udugu na mshikamano kama dira na mwongozo wa watu wa Mungu Barani Afrika. Usawa na utofauti kati ya watu ni sehemu ya mpango wa Mungu, ili kutajirishana na kushirikishana: karama, fadhila na wema!

Mababa waasisi wa AMECEA walibainisha ajenda saba kama sehemu ya mbinu mkakati wa AMECEA katika sera na mipango ya kichungaji.

Mababa waasisi wa AMECEA walibainisha ajenda saba ambazo zilipaswa kufanyiwa kazi kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya kesho ya Kanisa la Afrika.

Mkutano wa 19 AMECEA: Ajenda 7 za Mababa wa AMECEA, mwaka 1961

16/07/2018 15:09

Mababa wa AMECEA kunako mwaka 1961 waliibua ajenda 7 ambazo zilipaswa kufanyiwa kazi kwa ajili ya "Kesho ya Kanisa la Bara la Afrika": Vyombo vya mawasiliano ya jamii; Mafunzo awali na endelevu ya maisha ya kiroho; Kituo cha uchungaji, Chuo Kikuu; Kujitegemea, Elimu; Haki na Amani.

Askofu mkuu Rugambwa anawataka Mababa wa AMECEA kurejea na kupyaisha Waraka wa Paulo VI "Africae Terrarum"

Askofu mkuu Protase Rugambwa anawataka Mababa wa AMECEA kufanya rejea na kupyaisha Waraka wa Mwenyeheri Paulo VI "Africae Terrarum" yaani "Bara la Afrika".

Askofu mkuu Rugambwa: AMECEA fanyeni rejea kwa Waraka Africae Terrarum

16/07/2018 14:47

Askofu mkuu Protase Rugambwa amewataka Mababa wa AMECEA katika mkutano wao wa 19 kufanya rejea tena kwenye Waraka wa Kitume ulioandikwa na Mwenyeheri Paulo VI "Africae Terrarum" unaobainisha: amana, utajiri, tunu msingi, changamoto na matumaini ya familia ya Mungu Barani Afrika!

Baraza la Kipapa la Mawasiliano litaendelea kushirikiana na AMECEA katika tasnia ya mawasiliano ya jamii.

Baraza la Kipapa la Mawasiliano litaendelea kushirikiana na AMECEA katika tasnia ya mawasiliano, amesema, Dr. Paolo Rufini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano.

Baraza la Kipapa la Mawasiliano kuendelea kushirikiana na AMECEA

16/07/2018 10:01

Dr. Paolo Rufini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano katika ujumbe wake kwa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati, AMECEA, amewahakikishia Mababa wa AMECEA kwamba, Vatican itaendelea kushirikiana na AMECEA katika tasnia ya mawasiliano ya jamii!