Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Njia ya Msalaba 2017

Mama Kanisa kila mwaka ifikapo tarehe 14 Septemba anaadhimisha Siku kuu ya Kutukuka kwa Msalaba Mtakatifu.

Mama Kanisa kila mwaka ifikapo tarehe 14 Septemba anaadhimisha Siku kuu ya kutukuka kwa Msalaba Mtakatifu, kielelezo cha huruma, upendo, msamaha na hekima ya Mungu kwa binadamu!

Siku kuu ya Kutukuka kwa Msalaba wa Yesu: Utakatifu, huruma na upendo

14/09/2017 07:00

Kila mwaka ifikapo tarehe 14 Septemba, Mama Kanisa anaadhimisha Siku kuu ya kutukuka kwa Msalaba wa Kristo, kielelezo cha mateso, kifo na ufufuko wa Kristo kwa wafu; ufunuo wa utakatifu, ukuu, huruma, upendo na msamaha unaobubujika kutoka katika hekima ya Baba wa milele kwa ajili ya binadamu!

Papa Francisko wakati wa Ibada ya Njia ya Msalaba kuzunguka Magofu ya Colosseo amegusia: kashfa ya mateso, imani na matumaini kwa huruma ya Kristo!

Papa Francisko wakati wa Ibada ya Njia ya Msalaba kuzunguka Magofu ya Colosseo amegusia kashfa ya mateso ya watu sehemu mbali mbali za dunia; imani na matumaini kwa huruma na upendo wa Yesu kwa waja wake!.

Papa Francisko: Njia ya Msalaba katika uhalisia wa maisha ya watu!

15/04/2017 08:32

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya maadhimisho ya Njia ya Msalaba kuzunguka Magofu ya Colosseo mjini Vatican, Ijumaa kuu tarehe 14 Aprili 2017 ametafakari kuhusu kashfa ya mateso na mahangaiko ya binadamu ulimwenguni pamoja na imani na matumaini kwa huruma na upendo wa Kristo Yesu!

Wanawake walikuwapo msalabani japokuwa wasingefanya lolote zaidi ya kutafakari,kupenda,kuteseka na kukaa kimya

Wanawake walikuwapo msalabani japokuwa wasingefanya lolote zaidi ya kutafakari,kupenda,kuteseka na kukaa kimya.

Yesu Msalabani amekabidhi Maria Mama yake kuwa Mama wa Kanisa!

14/04/2017 16:27

Katika matanga ya Ijumaa Kuu,yanayo wakilisha dunia nzima kwa kifo cha msalaba, kwayo muda umesimama na kuacha nafasi ya maisha mapya. Hii ni kutokana na giza nene limetanda na pazia la ekalu kupasuka vipande viwili ikiwa ni kutoa fursa ya kuonesha kile kisicho onekana  kuonekana wazi