Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

"Furaha ya Upendo" ndani ya Familia

Papa Francisko amebaianisha mambo makuu yanayopaswa kukaziwa katika malezi na makuzi ya vijana wa kizazi kipya Jimbo kuu la Roma.

Papa Francisko amebainisha mambo msingi yanayopaswa kukaziwa katika malezi na makuzi ya vijana wa kizazi kipya Jimbo kuu la Roma.

Papa Francisko abainisha mambo msingi katika malezi ya vijana!

20/06/2017 11:33

Baba Mtakatifu Francisko, amefungua rasmi kongamano la Jimbo kuu la Roma kwa kukazia: umuhimu wa familia jijini Roma; umuhimu wa kujenga na kudumisha mshikamano; kuandamana na vijana; elimu endelevu, jinsi ya kukabiliana na changamoto za vijana na umuhimu wa maisha ya kiroho!

Furaha ya upendo ndani ya ndoa na familia sio nadharia bali  ni uhalisia wa maisha ya kila siku

Furaha ya upendo ndani ya ndoa na familia sio nadharia, bali ni uhalisia wa maisha ya kila siku

Furaha ya ndoa na familia sio nadharia, ni uhalisia wa maisha.

06/06/2017 13:59

Katika Barua ya kichungaji, Baraza la Maaskofu Katoliki Ubelgiji limedadavua Wosia wa Kitume, Amoris laetitia, Furaha ya Upendo ndani ya Familia, katika harakati za kuleta matunda bora na yanayodumu katika kuishi furaha ya upendo ndani ya maisha ya ndoa na furaha.

Papa Francisko amekutana na kuzungmza na rais Donald Trump wa Marekani mjini Vatican tarehe 24 Mei 2017

Papa Francisko amekutana na kuzungumza na Rais Donald Trump wa Marekani tarehe 24 Mei 2017.

Rais Donald Trump akutana uso kwa uso na Papa Francisko!

24/05/2017 14:04

Baba Mtakatifu Francisko amemzawadia Rais Donald Trump wa Marekani Nyaraka zake za kitume: Furaha ya upendo ndani ya familia; Furaha ya Injili na Sifa iwe kwako juu ya utunzaji wa nyumba ya wote pamoja na medali ya tawi la mzeituni, linalomkumbusha dhamana ya amani duniani!

Vijana, Imani na Mang'amuzi ya Miito & Furaha ya upendo ndani ya famili; ni msingi wa Sinodi ya Maaskofu 2018.

Vijana, Imani na Mang'amuzi ya Miito ni msingi wa maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu wa Vijana kwa mwaka 2018, ili kuwasaidia vijana kufanya maamuzi magumu katika maisha yao"!

Kardinali Baldisseri: maadhimisho ya Sinodi kwa jicho la kichina!

18/05/2017 10:27

Wosia wa Kitume wa Baba Mtakatifu Francisko "Furaha ya upendo ndani na familia" na Kauli mbiu ya maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana yaani "Vijana, Imani na Mang'amuzi ya Miito" ni nyenzo msingi katika maandalizi ya maisha na utume wa vijana wa kizazi kipya kwa sasa!

Familia bado ni sehemu ya Habari Njema ya Wokovu kwa walimwengu anasema Papa Francisko!

Familia bado ni sehemu ya Habari Njema ya Wokovu anasema Papa Francisko katika barua yake kwa Maaskofu Katoliki sehemu mbali mbali za dunia kama sehemu ya maandalizi ya Siku ya Tisa ya Familia Duniani, itakayoadhimishwa mwaka 2018 huko Dublin, nchini Ireland.

Iweni mashuhuda na vyombo vya Injili ya familia duniani!

20/04/2017 08:45

Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kuwamasisha waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kutambua kwamba, familia bado ni sehemu muhimu sana ya Habari Njema inayopaswa kutangazwa na kushuhudiwa ulimwenguni kwa kujikita katika tunu msingi za maisha ya kifamilia!

Ilikuwa tarehe 2 Aprili 2005 baada  ya saa tatu na nusu za usiku Mtakatifu Yohane Paulo II akaitwa na Baba Mungu,katika mkesha wa Huruma ya Mungu

Ilikuwa tarehe 2 Aprili 2005 baada ya saa tatu na nusu za usiku Mtakatifu Yohane Paulo II akaitwa na Baba Mungu,wakati anaaga dunia, tayari ulikuwa ni mkesha wa sikukuu ya Huruma ya Mungu .

Kumbukumbu ya Mt. Yohane Paulo II ni hai kwa waamini duniani

03/04/2017 16:15

Mtakatifu Yohane Paulo II ametawala kwa  kipindi kirefu tangu mwaka 1978 hadi 2005.Kufika tarehe 2 Aprili 2017 ni mika 12 imepita lakini kumbukumbu yake leo hii ni hai kwa watu na pia kuwapo uwiano sawa kati ya Baba Mtakatifu Francisko katika shughuli za kichungaji kwa Kanisa ulimwenguni 

 

Papa Francisko anasema familia ni Habari Njema kwa walimwengu!

Papa Francisko anasema familia ni Habari Njema kwa walimwengu.

Familia ni Habari Njema kwa walimwengu!

31/03/2017 09:47

Injili ya familia, furaha ya ulimwengu ndiyo kauli mbiu inayoongoza maadhimisho ya Siku ya IX ya Familia Duniani kwa Mwaka 2018 huko Dublin, nchini Ireland. Baba Mtakatifu Francisko anawahamasisha wanafamilia kufanya tena tafakari ya kina kuhusu wosia wake: Furaha ya upendo ndani ya familia!

Waamini wanahamasishwa kutangaza na kushuhudia Injili ya familia

Waamini wanahamasishwa kutangaza na kushuhudia Injili ya familia hadi miisho ya dunia.

Siku ya Familia Duniani kwa Mwaka 2018, Jimbo Kuu la Dublin, Ireland

30/03/2017 16:26

Baba Mtakatifu anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kusimama kidete kutangaza na kushuhudia Injili ya familia katika maisha na vipaumbele vyao. Wosia wa kitume Furaha ya Upendo ndani ya familia ni dira na mwongozo wa maisha na utume wa Familia kwa wakati huu!