2018-07-05 14:35:00

Dr. Ruffini ateuliwa kuwa Mwenyekiti Baraza la Kipapa la Mawasiliano


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Dr. Paolo Ruffini kuwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano. Kabla ya uteuzi huu, Dr. Ruffini alikuwa ni Mkurugenzi mkuu wa Kituo cha Televisheni cha Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, (TV 2000). Alizaliwa tarehe 4 Oktoba 1956 huko Palermo, Kusini mwa Italia. Baada ya masomo yake kutoka Chuo kikuu cha “La Sapienza” kilichoko mjini Roma, akatunukiwa Shahada ya uzamivu katika sheria na taratibu za uendeshaji wa kesi mahakamani. Kunako mwaka 1979 akaanza kazi ya uandishi wa habari kitaaluma na Mwaka 1986 akafunga ndoa  na Maria Argenti.

Tangu wakati huo, amefanya kazi zake katika magazeti ya ! Il Mattino di Napoli kati ya mwaka 1979- 1986; Il Messaggero di Roma kati ya Mwaka1986 hadi mwaka 1996. Baadaye akahamia kwenye kitengo cha Radio na kufanya kazi RAI tangu mwaka 1996 hadi mwaka 2002; Idhaa ya Bunge kati ya mwaka 1998 hadi mwaka 2002; Radio I Mwaka 1999 hadi mwaka 2002; In Blue Radio (2014-2018; Katika Televisheni RAI 3 kati ya Mwaka 2002 hadi mwaka 2011. La 7 kati ya Mwaka 2011 hadi mwaka 2014. Kituo cha Televisheni cha TV2000 kuanzia mwaka 2014-2018. Ni kiongozi aliyebobea katika masuala ya uandishi wa habari kitaaluma na ameshiriki katika mikutano na makongamano mbali mbali mintarafu mawasiliano ya jamii hasa kuhusiana na: Kanuni maadili za mawasiliano, dhamana na wajibu wa Wakristo katika ulimwengu wa mawasiliano ya jamii pamoja na njia mpya za mawasiliano ya jamii.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Vatican News!

 








All the contents on this site are copyrighted ©.