Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Askofu mkuu Michael A. Blume ateuliwa kuwa Balozi wa Hungaria

Askofu mkuu Michael A. Blume ametauliwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Hungaria kabla ya hapo alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Uganda. - AP

05/07/2018 17:04

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Michael A. Blume kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Hungaria. Kabla ya uteuzi huu, alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Uganda. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Michael A. Blume alizaliwa kunako tarehe 30 Mei 1946. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa Daraja Takatifu la Upadre hapo tarehe 23 Desemba 1972. Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto wa XVI akamteuwa  kuwa Askofu mkuu hapo tarehe 24 agosti 2005 na kuwekwa wakfu hapo tarehe 30 Septemba 2005. Tangu wakati huo amekuwa ni Balozi wa Vatican nchini Benin na Togo. Baadaye akateuliwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Uganda.

 

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Vatican News!

05/07/2018 17:04