2018-06-28 17:35:00

Maaskofu wakuu 29 kupewa Pallio Tatakatifu, 29 Juni 2018


Katika maadhimisho ya Sherehe ya Watakatifu Petro na Paulo miamba wa imani, Ijumaa, tarehe 29 Juni 2018, Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kuongoza Ibada ya Misa takatifu na kutoa Pallio Takatifu kwa Maaskofu wakuu 29 walioteuliwa katika kipindi cha mwaka 2017-2018, kama alama ya umoja kati ya Makanisa Mahalia na Khalifa wa Mtakatifu Petro. Pallio Takatifu ni alama ya Kristo Mchungaji mwema na kwamba, manyoya ya Palio Takatifu yalibarikiwa na Baba Mtakatifu Francisko wakati wa kumbu kumbu ya Mtakatifu Agnes, inayoadhimishwa na Kanisa kila mwaka ifikapo tarehe 21 Januari.

Maaskofu wakuu kutoka Barani Afrika wanaopewa Palio Takatifu ni pamoja na: Askofu mkuu Isaack Amani Massawe wa Jimbo kuu la Arusha, Tanzania. Askofu mkuu Alick Banda wa Jimbo kuu la Lusaka, Zambia. Askofu mkuu Gervais Banshimiyubusa wa Jimbo kuu la Bujumbura, Burundi pamoja na Askofu mkuu Gabriel Charles Palmer-Buckle wa Jimbo kuu la Cape Coast, Ghana.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Vatican News!

 








All the contents on this site are copyrighted ©.