2018-06-26 16:00:00

Kanisa katoliki katika kutekeleza malengo endelevu ya SDGs ya ajenda 2030


Askofu Mkuu Ivan Jurkovic, mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika ofisi za Umoja wa Mataifa ametoa hotuba yake tarehe 25 Juni 2018 katika kikao cha 38 kitengo cha  haki za Binadamu huko mjini  Geneva nchini Uswiss. Kikao hicho kilikuwa na mada ya haki ya mafunzo , ambapo amekumbusha juhudi za Kanisa Katoliki mbele  mashule 200,000 na zaidi ya elfu mbili za vyuo vikuu.

Katika hotuba hiyo amesisitiza kwamba  wazazi lazima wawe na uwezekano wa kuchagua shule ambayo inazingatia vema thamani zao, kwa maana hiyo wazazi wanayo haki msingi ya kuwaelimisha watoto wao. Katika dunia ambayo umegubikwa na kumezwa na utandawazi, Askofu Mkuu anasema elimu inahitaji matendo ya yati hasa kujikita katika  mazungumzo ambayo yanaunda makutano , kusifu tofauti za tamaduni na dini. Lakini lengo hilo muhimu haliwezekani kamwe kumalizia  kwa njia ya ukoloni wa itikadi zinazo sambaza mawazo potofu, katika  asili ya jamii, na maisha ya binadamu, ambayo kila wakati yanazi kukutana na hekima ya watu na dini zao.

Kutokana na mantiki hiyo, ndipo Askofu Mkuu Ivan Jurkovič anasisitiza juu ya uwajibika wa wazazi hasa katika utambuzi wa  haki na msingi walizo nazo wazazi na zaidi wa kuelimisha watoto wao na ili kuweza kutamba msingi na maana ambayo ni uwezekano kwa ajili ya familia katika kuchagua shule na kutafakari vema  thamani zao msingi na kuziheshimu hawali ya yote wao wenyewe. Uhuru huo ndiyo hatua nyeti zaidi ya kuweza kuwa na  mafunzo yaendelee katika nafasi ya kina na mandeleo kamili ndani ya jamii.

Kila binadamu ana haki ya kupata elimu, kwa maana elimu ina lengo la kumfundisha mtu aweze kuona mwisho wake kwa ajili ya wema wa jamii mahali ambamo yeye anaishi; elimu ndio mwangaza na taa pekee inayomuangazia mwanadamu katika maisha,  na elimu ndio jukumu na a sababu ya msingi ya mtu kuweza kupata hadhi na kujua vema haki msingi anazopaswa kuwa nazo .

Hata hivyo, kulingana na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs),ya ajenda 2030 mipango mbalimbali inatekelezwa ili kuwawezesha kila mtu hasa katika kuomba serikali za nchi  ziweze kutoa mchango unaostahili ili watu wote waweze kuwa na fursa ya kudumu na kukwamua.  Ajenda ya Elimu ya SDGs 2030 inahimiza Serikali nyingi ziweze kupiga hatua kubwa katika kutimiza malengo ya kitaifa na mataif,a  ndani ya muktadha wa malengo ya dunia nzima ambapo bila juhudi za pamoja ni vigumu kufikia, kwa maana hiyo Askofu Mkuu Ivan Jurkovic amewataka Jumuiya ya kimataifa kusaidia juhudi za nchi hizo kwa maana katika mapambano dhidi ya kuondokana na umaskini na ujinga ili kupata maendeleo.

Shughuhuli makini ya elimu kwa upande wa Kanisa Katoliki inaendelea kutoa mchango wake kwa njia ya mitanado mingi ambapo kwa saa ni zaidi ya mashule 200,000 na zaidi ya vyuo vikuuu elfu moja.  Hiyo ina maana ya kwamba kusaidia hali ya mafunzo, inahakikishia vijana na wazalendo wa kesho kushiriki kikamilifu utajiri wa urithi wa utamaduni  katika jamii yao na kujiandaa katika mazungumzo na watu wote katika ulimwengi ambao unazidi kuchanganyikana na  ili  kuwa wakala wa amani na maendeleo kamili ya binadamu.

Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.