2018-06-25 16:55:00

Papa Francisko: utofauti ni msingi wa maisha ya binadamu!


“Ninayo furaha ya kuwasalimia wote kuanzia kwa Mwenyekiti Askofu Mkuu Vincenzo Paglia na kumshukuru kuwakilishwa kwake Mkutano Mkuu ambao unahusu  mada ya maisha ya binadamu na ambayo  itawekwa katika mantiki ya ulimwangu mzima, mahali tunapoishi. Aidha leo hii ninataka kumsalimia Kardinali Segreccia mwenye umri wa mika 90 lakini bado anayo shauku, kijana katika mapambano kwa ajili ya kutetea na kudumisha Injili ya maisha. Asante sana kwa kile ulichofanya katika kambi hiyo na kile unachoendelea kufanya asante”.

Ni utangulizi wa hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 25 Juni 2018, alipokutana na wajumbe Braza la Kipapa kwa ajili ya maisha wakiongozwa na Askofu  Mkuu Vincenzo Paglia Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya maisha na Kansela wa Taasisi ya Kipapa Yohane Pauli II. Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake anasema, hekima inapaswa kufuatana na tabia zetu mbele ya ekolojia ya binadamu na kutoa ushauri wa kufikia ubora wa maadili na tasaufi ya maisha katika hatua zake zote. Yapo maisha ya binadamu anayezaliwa  katika maisha, kwenye muda wa kuchukua mimba, maisha kuzaliwa, maisha ya utoto, maisha ya ujana, maisha ya utu uzima, maisha ya uzee na uchakavu, hatimaye yapo maisha ya milele.

Kadhalika yapo maisha ambayo ni ya familia na jumuiya, maisha ambayo ni ya wito na kutumaini. Na kama jinsi ilivyo maisha  ya binadamu mdhaifu na mgonjwa, maisha yaliyo na majeraha, kusononeka, kuchanganyikiwa, kukataliwa na kubaguliwa. Yote hayo ni maisha ya binadamu. Ni maisha ya binadamu ambaye anaishi katika ardhi iliyo umbwa na Mungu na kushirikishana na nyumba ya pamoja na viumbe wengine wanaoishi. Kwa hakika Baba Mtakatifu anathibitisha,  katika kutika maabara ya biolojia wanajifunza maisha na zana, zinazoruhusu  kufanya utafiti wa mantiki ya fisikia, kemia na ufundi. Ni mafunzo muhimu na dharura, lakini ambayo lazima kushirikishama   matarajio makubwa na kizazi zaidi na ambayo yanatakiwa umakini katika maisha ya dhati ya binadamu anayekuja katika uwanja huu wa dini kwa njia ya hija ya neno na mawazo ya matokea na Roho.  

Je ni utambuzi gani leo   hii unapatikana katika hekima ya binadamu kwa maisha ya sayansi ya asili? Ni utamaduni gani wa kisiasa ambao unajikita katika kuhamasisha na kulinda maisha ya dhati ya binadamu? Kazi nzima  ya maisha ni kuzaa binadamu mpya, elimu ya ubora wa kitasaufi na ubunifu, kuanzuswa kwa upendo wa familia na jumuia, kutunza ule udhaifu  na uathirika wake, majeraha yake; kama vile kuanzishwa kwa maisha ya watoto wa Mungu katika Kristo Yesu. Baba Mtakatifu Francisko amesema, tunapowakabidhi  watoto kuwa na ukosefu wa mambo muhimu, maskini kuwa na njaa, wanaoteswa katika vita, wazee wanao achwa pekee yao, je hata sisi hatufanyi kazi chafu ya kifo? Je hayo yanatoka wapi, kwa dhati kazi mbaya ya kifo inatokana na dhambi. Ubaya utafuta kila ulaghai kwamba kifo ndiyo mwisho wa kila kitu na sisi tulikuja duniani kwa bahati mbaya na tutaishia bila kitu.

Maono ya ulimwengu kuhusu elimu ya utambuzi wa uhai na juu ya maisha  ambayo kama wajumbe wanawakilisha  kutoa katika kambi maadili kijamii na kibiadamu katika sayari, maono hayo yana nguvu kwenye matajario ya kikristo na kujikita kwa ujasiri kwenye hali hasi ya kazi mbaya kuhusu kifo inayotokana na dhambi.  Elimu hii haitaweza kutenguka kuanzia katika magonjwa na kifo ili kuweza kuamua maana ya maisha na kuelezea thamni ya mtu. Badala yake intatenguka zaidi kwa kina katika uelewa wa hadhi ya binadamu na jinsi Mungu anavyo penda, hadhi ya kila mtu, kwa kila hatua za hali yake ya maisha na kutafuta mitindo  mipya ya upendo pamoja na tiba ambayo inaweza kumsaidia aliye athirika na udhaifu wake.

Hata hivyo Baba Mtakatifu ameonesha mahitaji ya mang’amuzi yanayo takiwa ambayo ni msingi katika maisha ya binadamu: mtu  kuanzia ngazi zote hadi kijamii na umri wa maisha. Hata kama vile hali ngumu na hatua zote au hata hatarishi ambazo ni maalum na zinahitaji hekima ya kimaadili na ujasiri wa uvumilivu kimaadili, kwa mfano: masuala ya  jinsia na kizazi, ugonjwa na uzee, ukosefu na ulemavu, kunyimwa na kutengwa, vurugu na vita. “ Utetezi wa asiye kuwa na hatia ambaye bado hajazaliwa, kwa mfano lazima uwe wazi, na ni lazima kuwa makini kwa sababu  pale ndipo kuna mchezo wa hadhi ya maisha ya binadamu, daima maisha matakatifu na yanayotakiwa upendo wa kila mtu zaidi ya maendeleo yake. Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa, utakatifu ni maisha ya maskini ambaye tayari wamekwisha zaliwa  na ambao wanangaika katika umasikini, na kubaguliwa, utakatifu upo kwa wale waliuzwa kwenye biashara haramu, utakatifu upo katika eutanasia iliyo fichika kwa wagonjwa na wazee ambao hawana tiba na katika kila aina ya utume, kila aina ya aliye baguliwa ( Wosia Gaudete et exsultate, 101).

Katika maandiko ya mafundisho ya kikristo na kikanisa juu ya mada ya maadili ya maisha ya binadamu, yanapewa kupata nafasi kwa mantiki ya elimu ya mtu kamili na siyo kuchangamana  kati ya masuala ya vikwazo vya maadili na vile vya  haki . Uongofu wa sasa ambao  ni kiini cha ekolojia ya binadau kamili, hasa katika ule wa pamoja na ugumu wa hali ya binadamu, ndiyo Baba Mtakatifu anawatakia waweze kuwajibika kwa dhati katika shughuli ya kiakili, raia na kidini kama msaada mkubwa  unaofanyika kwa pamoja na mapendekezo chanya.

Kutambua na kuthamini kwa uaminifu, kujikita katika maisha, hutoa chachu  ya shukrani kwetu sisi na uwajibikaji,kutia moyo wa kujitoa kikamilifu kwa ukarimu na uzoefu wa jumuiya ya kibinadamu. Hekima ya kikristo lazima ifunguke kwa huruma na shauku ya mawazo ya mwelekeo wa binadamu katika maisha ya Mungu ambaye alitoa ahadi ya kufungua maisha zaidi ya kifo, mtazamo usio na mwisho wa upendo wa miili katika mwanga na bila machozi. Hiyo inashangaza zaidi kwa yale yote yanayoonekana na yasiyoonekana ambayo yamejificha katika umbu la muumbaji.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.