2018-06-23 15:14:00

Kanisa la Korea katika jitihada za kutetea maisha ya binadamu tangu kutungwa!


Hivi karibuni, kumefanyika maandamano makubwa kwa roho ya wakatoliki nchini Korea katika mji wa Seoul kwa ajili ya utetezi wa maisha ambapo wanasema kuwa hakuna kuruhusu sheria ya utoaji mimba, wakionesha juhudi kubwa ya utetezi wa maisha ya binadamu yanayozaliwa. Chanzo hawali yote ni mara baada ya Mahakama kuu ya nchi ya Korea ya Kusini kutangaza kutoa maoni juu ya maamuzi ya sheria iliyokuwa ya sasa inayozuia utoaji wa mimba. Maandamano hayo mara baada ya kufikia katika Kanisa Kuu la Seuol waandamanaji wote walisikiliza hotuba iliyotolewa na Kardinali Andrew Yeom Soo-jung, wa Jimbo Kuu la Seoul ambaye aliwataka kupokea mwaliko na kutetea daima uhai wa maisha ya binadamu na hasa kwa wale wanaojionesha wadhaifu na kuhitaji msaada. 

Kardinali amesisitiza kuwa, maisha ambayo yanafikiriwa madhaifu na yasiyo na maana, ndiyo yenye uwezo na nguvu kubwa, kwa maana hiyo wote ni wote wanahusika na vikwazo na hali haisi ya kijamii ambayo inasukuma wanawake wangi kujikuta wanafanya maamuzi kinyume na sheria hasa tendo la  kukubali kutoa mimba. Hata hivyo  kardinali Soo-jung, amesisitiza kuwa, utoaji mimba siyo jambo  bora, hata katika  suala la uchaguzi,badala yake ni lazima  kujikita katika kujenga utamaduni ambao unafundisha, kuheshimu na kupenda maisha kwa pamoja. Maandamano kwa ajili ya maisha, yameandaliwa na shirikisho la makundi ya asasi mbalimbali  ambayo yanahamasisha  uhai wa maisha katika utamaduni wa dhati wa maisha  na kusisitiza kuwa  maisha matakatifu yanayozaliwa lazima yabidishe wengi katika  kuwasaidia wanawake wote na familia zenye kuwa na matatizo. 

Hii ni kazi ngumu hasa kukabiliana na mivutano ya baadhi ya mashirika mengine ya kijamii ambayo yanatoa msukumo wa kutengua hata sheria ya utoaji mimba na kugusa dhamiri na hisia za kujitegemea kwa mwanamke. Vilevile utoaji wa mimba kwa upande wa wakatoliki ni suala lisilo kuwa na haki, kukosa kuheshimu maisha na haki za maisha ya wanawake. Baadhi ya mataifa kama Marekani, Ulaya, na kwingineko yamekuwa  na mapendekezo mpya kuhusu sheria inayo taka kuruhusu utoaji mimba, ambayo kwa bahati mbaya wanapata washabiki wake katika  nchi nyingi kwa mfano wa hivi karibuni nchini Ireland.

Hata hivyo watetezi hao ni baadhi ya asasi maarufu za kiraia zinazokuwapo katika nchi kwa upande mmoja ambazo zinaingia katika mzozo na asasi nyingine zenye asili ya ukristo zikipinga vikali mapendekezo ya kuuakiumbe awe hajatungwa, ametungwa na kuazaliwa. Siku ziliopita tumeona nchini nchini Ireland na juhudi za Kanisa la Ireland walizofanya hadi kufikia kilele, japokuwa kwa kushindwa kupata kura zinazostahili ili kutobadilisha muswada wa sheria ya utoaji mimba. Kutokana na hiyo ndipo unaweza kushuhudia utabiri  wa Mtakatifu Paulo Mtume wa watu katika barua yake aliyo mwandikia mwanfunzi wake Timoteo kuwa, “  “Kumbuka kwamba, katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati za taabu. Watu watakuwa na ubinafsi, wenye tamaa ya fedha, wenye majivuno, wenye kujiona, wenye kumtukana Mungu, wasiowatii wazazi wao, wasio na shukrani na waovu; watatokea watu wasio na upendo moyoni, wasio na huruma, wachongezi, walafi na wakali; watachukia chochote kilicho chema; watakuwa wahaini, wakaidi na waliojaa kiburi; watapenda anasa kuliko kumpenda Mungu…” (2Tim.3:1-5).

Katika mantiki hiyo na picha ya hali halisi ya  karibu wa dunia nzima kwa ujumla kwenye masuala mengi ya kijamii, je hayo yasemwayo na Maandiko Matakatifu hayapo hizi nyakati zetu. Katika dunia hii watu wamekuwa na ubinafsi na tamaa ya fedh; watu wanao jijali wao na fedha kuliko maisha ya binadamu, kumuuza kama mnyama na kunyanyasa; wenye kumtukana Mungu na kuutoa uhai wa binadamu wakitaja jina lake; wasio na shukrani na waovu kumtendea vibaya mtu jirani na ndugu, manyanyaso kwa watoto, wanawake na wazee. Wapo watu wengi wasio kuwa na upendo, wenye mioyo migumu kama mawe na kuwatendea ukatili wenzao kila sehemu, iwe kuwakwaza kwa maneno, mifano na matendo, kama vile ukosefu wa kumkaribisha mwenzako, kumpkea mgeni, kumsema vibaya na kumfanyia ukatili wa kichichini.

Watu wangapi wasio na huruma hata kati ya familia, jamii kazini na sehemu nyingine nyingi, wengi wenye kuchukia chochote kilicho chema cha jirani hata ndugu mke au mtoto au mkwe na wengine wengi  wanaopenda anasa kuliko kumpenda Mungu. Yatosha kutazama katika luninga au kusikiliza katika radio utaona au  kusikiliza majadiliano ambayo yanahusu anasa, bila uwepo wa hali ya  hewa ya Mungu. Hayo yote na mengine yamempelekea mwanadamu kufika hatua ya kutojali uhai wa  mtu, kwa maana utafikiri umbu katika tumbo la mwili wa binadamu ni uchafu, hiki ni kilio hata cha Mungu ambaye ameumba binadamu kwa mfano na sura yake lakini, binadamu amesahau kabisa hata hasira aliyokuwa  nayo juu ya dhambi  ya Sodoma na Gomora, na maombi ya mtetezi mkuu baba wa Imani Ibrahimu

Historia ya Sodoma na Gomora:

“Bwana akasema, kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana, basi, nitashuka sasa nione kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia; na kama sivyo, nitajua. Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za Bwana. Ibrahimu akakaribia, akasema, Je! Utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu? Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, wala hutauacha mji kwa ajili ya hao hamsini wenye haki waliomo? Hasha usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha; Mhukumu ulimwengu wote asitende haki? Bwana akasema, Nikiona katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, nitapaacha mahali pote kwa ajili yao. Ibrahimu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu. Huenda wakapunguka watano katika wale hamsini wenye haki, je! Utaharibu mji wote kwa kupungua watano? Akasema, Sitauharibu, nikiona humo arobaini na watano. Akazidi tena kusema naye, akinena, Huenda wakaonekana humo arobaini? Akasema, Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini. Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema, Huenda wakaonekana huko thelathini? Akasema, Sitafanya, nikiona humo thelathini.

Akasema, Tazama, nimeshika kusema na Bwana, huenda wakaonekana huko ishirini? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini. Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu, Huenda wakaonekana huko kumi? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi. Basi Bwana alipokwisha kuzungumza na Ibrahimu, akaenda zake; Ibrahimu naye akarudi mahali pake.  Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi. Akasema, Bwana zangu, karibuni nawasihi mwingie nyumbani mwa mtumwa wenu, mkalale, mkanawe miguu yenu, hata asubuhi mwondoke na mapema mkaende zenu. Wakasema, Sivyo, lakini tutakaa uwanjani usiku kucha. Akawasihi sana, nao wakaja, wakaingia nyumbani mwake.

Akawafanyia karamu, akawapikia mikate isiyochachwa nao wakala.  Hata kabla hawajalala, watu wa mji, wenyeji wa Sodoma, wakaizunguka nyumba, vijana kwa wazee, watu wote waliotoka pande zote.  Wakamwita Lutu, wakamwambia, Wa wapi wale watu waliokuja kwako usiku huu? Uwatoe kwetu, tupate kuwajua. Lutu akawatokea mlangoni, akafunga mlango nyuma yake.Akasema, Basi, nawasihi, ndugu zangu, msitende vibaya hivi. Tazama, ninao binti wawili ambao hawajajua mtu mume, nawasihi nitawatolea kwenu mkawafanyie vilivyo vyema machoni penu, ila watu hawa msiwatende neno, kwa kuwa wamekuja chini ya dari yangu.

 Wakasema Ondoka hapa! Kisha wakanena, Mtu huyu mmoja amekuja kwetu kuketi hali ya ugeni; naye kumbe, anataka kuhukumu! Basi tutakutenda wewe vibaya kuliko hawa. Wakamsonga sana huyo mtu, huyo Lutu, wakakaribia wauvunje mlango. Lakini wale watu wakanyosha mikono yao, wakamwingiza Lutu kwao nyumbani, wakaufunga mlango. Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta mlango. Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je! Unaye mtu hapa zaidi? Mkwe, wanao, na binti zako, na wo wote ulio nao katika mji, uwatoe katika mahali hapa; maana tutapaharibu sisi mahali hapa, kwa kuwa kilio chake kimezidi mbele za Bwana; naye Bwana ametupeleka tupaharibu.

Lutu akatoka akasema na wakweze, waliowaposa binti zake, akasema, Ondokeni mtoke katika mahali hapa kwa sababu Bwana atauharibu mji huu. Lakini akawa kama achezaye machoni pa wakweze.  Hata alfajiri ndipo malaika wakamhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, usipotee katika maovu ya mji huu. Akakawia-kawia; nao wale watu wakamshika mkono, na mkono wa mkewe, na mkono wa binti zake wawili, kwa jinsi Bwana alivyomhurumia, wakamtoa wakamweka nje ya mji. Ikawa walipomtoa nje, mmoja alisema, Jiponye nafsi yako usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea. Lutu akawaambia, Sivyo, bwana wangu!

Tazama, mtumwa wako ameona kibali machoni pako, nawe umezidisha rehema zako ulizonifanyia kwa kuponya nafsi yangu, nami siwezi kukimbilia mlimani nisipatwe na yale mabaya, nikafa.  Basi mji huu u karibu, niukimbilie, nao ni mdogo, nijiponye sasa huko, sio mdogo huu? Na nafsi yangu itaishi.  Akamwambia, Tazama, nimekukubali hata kwa neno hili, kwamba sitauangamiza mji huo uliounena. Hima, ujiponye huko, maana siwezi kufanya neno lo lote, hata uingiapo humo. Kwa hiyo jina la mji ule likaitwa Soari. 

Jua lilikuwa limechomoza juu ya nchi Lutu alipoingia Soari. Ndipo Bwana akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto toka mbinguni kwa Bwana. Akaangusha miji hiyo na Bonde lote, na wote waliokaa katika miji hiyo, na yote yaliyomea katika nchi ile. Lakini mkewe Lutu akatazama nyuma yake, akawa nguzo ya chumvi. Ibrahimu akatoka asubuhi kwenda mahali aliposimama mbele za Bwana,naye akatazama upande wa Sodoma na Gomora na nchi yote ya hilo Bonde, akaona, na tazama, moshi wa nchi ukapanda, kama moshi wa tanuru. Ikawa Mungu alipoiharibu miji ya Bondeni, Mungu akamkumbuka Ibrahimu, akamtoa Lutu katika maangamizi alipoiangamiza miji hiyo aliyokaa Lutu. (Mwanzo 18:16-33, 19:1-29)

Na Sr Angela Rwezaula 

Vatican News!

 

 

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.