2018-06-22 13:51:00

Tarehe 24 Juni Siku ya kukumbuka wahamiaji waliokufa njiani kuja Ulaya


Haki na mapokezi ndiyo njia iliyochanganuliwa na Kanisa la Ulaya mbele ya janga la mapambano dhidi ya uhamiaji. Haya yametamkwa na Baraza la Makanisa Ulaya (Cec ) ambayo katika siku hizi wanatoa wito hawali ya yote kwa Jumuiya ya kikristo barani Ulaya ili kukumbuka waathirika ambao tangu mwaka 2000 hadi leo wanakaridiriwa watu 30,000 wamekufa wakiwa njiani kuelekea Ulaya.

Matukio ya hivi karibuni, yanayohusiana na Meli ya kuokoa watu iitwayo Aquarius, ambayo imeleta mgomgoro mkubwa, Baraza la Makanisa (Cec) wanakumbusha kupitia katika  tovuti yao, wakionesha jinsi gani baadhi ya wanasiasa hawatoi kipaumbele cha hali halis ya maisha na ustawi wa watu wangi ambao wanakimbia ghasia, vita na ukosefu wa haki, na kwa njia hiyo kulazimika kukatisha bahari katika hali ya matatizo yasiyo elezea na yenye hatari ya kupoteza maisha. Hali kama hiyo kwa mujibu wa Baraza la Makanisa Ulaya linabainisha kuwa ni kama kufilisika kimaadili na zaidi ya ukosefu wa kujikita katika matendo ya thamani za Ulaya.

Mbele ya tabia hizi wanasisitiza tena Makanisa lazima kuendelea kutetea hali halisi ya wakimbizi na kuwapokea wanye kuhitaji. Zaidi ya hayo wanaongeza, Makanisa ya Ulaya tayari yamesha toa jibu dhidi ya upofu wa kuona upotezaji wa maisha kwa njia ya mshikamano na kusaidia juhudi za kutafuta msaada na kuhakikisha kwamba Baraza la Umoja wa Ulaya kwa namna ya pekee kujikita zaidi  katika  haki, usalama na sheria wakimbizi na wahamiaji na kwa  mantiki hii ndiyo jibu la kutatua hali halisi ya kipeo. Heikki Huttunen, Katika Mkuu wa Cec pamoja na Doris Peschke, Katibu Mkuu mstaafu wa Tume ya Ulaya kwa ajili ya Ulaya (Ccme), wametoa wito kwa makanisa ili kufanya kumbu kumbu ya wale waliopoteza maisha yao wakitafuta usalama na haki.

Katika barua yao Huttunen na Peschke iliyotumwa kwa wenzao ambao wanafanya uchaguzi wa Cec na Ccme wanakumbusha maelekezo yaliyotokea wakati wa makutano mkuu wa hivi karibuni uliofanyika huko Novi Sad nchini Serbia kwamba: “Utetezi wa haki za watu ambao wanalazimika kuacha nyumba zao kwasababu ya vita na kusukumwa kuja katika bara letu kwa matumaini ya kupata maisha mazuri, ni kutulazimisha kujitazama sisi na kutafakati barani Ulaya wakati endelevu, lakini pia  hata uwajibikaji na nafasi ya kuweza kujikita wakati endelevu na mbele dunia”. Na kwa sababu hiyo “kama jumuiya ya Kanisa, wanaongeza kusema, “sisi tumetiwa moyo wa kutumia kila aina ya uwezo tuli nao ili kuwa na mshikamano na umakini wa mada hii”. 

Kwa mtazamo huo, Tume ya Barazama la makanisa Ulaya kwa ajili wakimbizi  (Ccm) imetoa pendekezo kwa ajili ya maadhimisho kwa namna ya pekee tarehe 24 Juni, Jumapili inayofuata baada ya Siku ya Kimataifa ya wakimbizi kufanya  “ kumbu kumbu ya wale waliopoteza maisha yao wakitafuta usalama na haki”.

Na Sr Angela Rwezaula
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.