Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Habari \ Habari za Kimataifa

WHO:Kucheza michezo ya kompyuta kupindukia ni dalili za ugonjwa wa akili

Shirika la Afya Duniani limethibisha kuwa kucheza michezo ya kompyuta kupindukia inawezekana kuwa dalili za ugonjwa wa akili - ANSA

19/06/2018 14:38

Kucheza kupindukia katika michezo ya kompyuta na mingine ya kielektroniki inaweza kuwa ni dalili za ugonjwa wa akili. Hilo ni tatizo la afya ya akili ambalo ni kati ya miongoni mwa magonjwa yaliyo tolewa tarehe 18 Juni 2018 na shirika la afya ulimwenguni, (WHO) kwenye ainisho la kimataifa la magonjwa, ICD toleo la 11. Inaitwa gaming disorder, ambapo kwa mujibu wa ufafanuzi wa Shirika la Afya duniani WHO, wanathibitisha kuwa hii ni baada kuwa na  mfululizo wa tabia  inayozidi kuwakumba  watu katika matakwa ya  maisha ya yao. ICD (International Classification of Diseases) ni msingi wa kimataifa wa kubaini magonjwa na mienendo ya kiafya, ambapo imeweza kujumuisha mkusanyiko wa kanuni takribani 55,000 kuhusu majeraha, magonjwa na sababu za vifo, kanuni ambazo huwezesha wataalamu wa afya kubadilishana taarifa kuhusu masuala hayo kote ulimwenguni.

Akizungumzia hatua hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni WHO Bwana Tedros Ghebreyesus amesema, kuongezwa kwa mienendo hiyo ni muhimu sana kwa kuwa inawawezesha kutambua kwa kina kile kinachosababisha watu kuugua na kufariki dunia,pia kuchukua hatua kuokoa maisha. Kwa mantiki hiyo sasa kucheza michezo ya kompyuta kupindukia halikadhalika ulundikaji wa vitu bila matumizi hiyo imejumuishwa katika orodha hiyo kuwa ni ugonjwa wa akili.

Naye Datari Shekhar Saxena, Mkurugenzi wa Idara ya afya ya akili na matumizi ya madawa ya kulevya kwa upande wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ametoa ufafanuzi kwa kina na kwamba   ni utafiti wao umejumuisha kuwa michezo ya kielektroniki kupita kiasi ni kama ugonjwa wa akili. Daktari Saxena anasema, kucha michezo hii sasa imejumuishwa kutokana na ushahidi dhahiri wa kisayansi wa tabia na dalili na kuna umuhimu na mahitaji ya tiba kutoka maeneo mengi duniani. Na ndio maana imeongezwa na bila shaka itasaidia watu kufahamu zaidi kuhusu suala hii na hivyo kusaka na kupata tiba. Hata hivyo  amesisitiza kwamba, kila mtu anayecheza michezo hii kwa kiasi kidogo hawezi kupata shida hii. Kwa maana hiyo ni watu wachache wanaocheza ambao watakidhi vigezo vilivyowekwa vya kuwa na tatizo kutokana na kucheza michezo kwa mujibu wa utafiti wa kimataifa wa kubaini magonjwa na mienendo ya kiafya (ICD-11).

Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

19/06/2018 14:38