2018-06-19 07:40:00

Sera na mbinu mkakati wa Kanisa kwa ajili ya wakimbizi na wahamiaji!


Baba Mtakatifu Francisko anasema, sera na mbinu mkakati wa Kanisa Katoliki katika huduma kwa wakimbizi na wahamiaji inajikita katika mambo makuu manne yaani: “Kuwapokea, uwalinda, kuwaendeleza na kuwahusisha wakimbizi na wahamiaji” katika maisha ya jamii inayowapokea na kuwapatia hifadhi na usalama wa maisha! Ni matumaini ya Baba Mtakatifu kwamba, sera na mikakati hii inamwilishwa pia kwenye Makanisa mahalia, ili kuwasaidia watu hawa ambao mara nyingi wanajikuta wakitumbukia katika biashara ya binadamu, utumwa mamboleo na aina mbali mbali ya nyanyaso dhidi ya utu na heshima yao.

Kampeni inayoendeshwa na Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Endelevu ya Binadamu kitengo cha wakimbizi na wahamiaji imepewa tuzo la kimataifa kwa kuwa na mbini mkakati unaotekelezwa katika masuala ya kijamii. Tuzo hii imetolewa katika maadhimisho ya awamu ya kumi na mbili ya Sherehe ya Matangazo ya Kijamii. Video iliyoshinda tuzo hili la kimataifa, imeandaliwa na Kampuni ya “. La Machi Communication for Good Cause”. Tukio hili limdeadhimiswa usiku tarehe 15 Juni 2018, huko Madrid, Hispania.

Ni video inayosisitizia mambo makuu mannee yanayopewa kipaumbele cha pekee na Baba Mtakatifu Francisco yaani: ”Kuwapokea, kuwalinda. Kuwaendeleza na kuwahusisha” Kwa mara ya kwanza video hii ilitengenezwa Desemba 2017. Wajumbe wamejikita zaidi katika maandalizi ya kile kinachoitwa “Global Compact 2018” yaani “Mkataba wa Kimataifa wa Usalama wa Wahamiaji”.

Huu ni Mkataba wa Umoja wa Mataifa unaolenga kuratibu na kuboresha mchakato wa wahamiaji na wakimbizi duniani, ili kulinda na kudumisha haki msingi, utu na heshima ya wahamiaji! Umuhimu wa Jamii kusikiliza na kujibu kilio cha wakimbizi na wahamiaji duniani; kwa kukusanya maoni; kwa kupunguza gharama za kuwahudumia wahamiaji sanjari na kudumisha usalama na maisha bora zaidi. Mkataba wa Kimataifa wa Usalama wa wahamiaji unapania pamoja na mambo mengine kuboresha: ulinzi na usalama; haki msingi za binadamu pamoja na kupatiwa huduma ya msaada wa kisheria pale haki zao zinapovunjwa.

Padre Michael Czerny, Katibu mkuu msaidizi, Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Endelevu ya Binadamu wakati wa kupokea tuzo hii amesema, baba Mtakatifu Francisko anaendelea kutoa changamoto kwa Wakristo pamoja na watu wote wenye mapenzi, kusikiliza na kujibu kilio cha wakimbizi na wahamiaji. Video hii inaonesha mwaliko wa Baba Mtakatifu katika uhalisia wake, Vatican inapenda kuhakikisha kwamba, ujumbe huu unawagusa watu wengi zaidil. Video hii iliyorekodiwa na Vatican Media imekwisha kutafsiriwa katika lugha thelatini duniani.

FR. Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Vatican News.








All the contents on this site are copyrighted ©.