2018-06-19 15:05:00

Kila tarehe 15 Juni ni Siku Kimataifa ya kupinga manyanyaso kwa wazee!


Kila tarehe 15  Juni ya kila mwaka  ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu ukatili na manyanyaso wanaofanyiwa wazee. Kwa maana hiyo ni njia ya kutaka kuhamasisha uelewa wa manyanyaso na ukatili dhidi ya wazee ili usitishwe. Baraza kuu la Umoja wa Mataifa lilitenga siku ya tarehe 15 mwezi Juni kila mwaka ili kupaza sauti za kupinga manyanyaso yanayo wakumba wazee kwa kila hali, ambapo tangu mwaka 2006 imekuwapo maadhimisho hayo kwa lengo   na mwamko hasa wa ngazi ya juu kuihamasisha jamii ili ijikite katika utetezi wa wazee, licha ya suala hili  daima kuonekana kwa kina katika utume wa Kanisa!

Katika kilele hicho, Bwana Giancarlo Penza mhusika kwa huduma ya wazee katika jumuiya ya Mtakatifu Egidio amesisisitza kuwa, mbele ya kuongezeka kwa maisha, changamoto iliyopo ni ile ya kutoa umuhimu na thamani ya wazee katika jamii. Katika takwimu za Shirika la Afya Duniani WHO walionesha kuwa karibu asilimia 16 ya watu wenye umri zaidi ya miaka 60 wamepata manyanyaso ya kisaikolojia ( 11,6%), kiuchumi (6,8%9, kutokuwajali na (4,2%9, kimwili (2,6%). Mzee mmoja kati ya sita ni waathirika wa manyanyaso kwa mujibu wa utafiti uliofanyika kwa kanda 52 katika nchi 28 duniani. Shirika la Afya duniani (WHO) wanathibitisha kuwa kwa upande wa Ulaya tu ni karibu watu 10,000 kila siku ni wazee waathirika kwa manyanyaso,ambapo kila mwaka wazee 8,000 wanakufa kutokana na matokeo mabaya ya manyanyaso hayo.

Ongezeko la watu wazee, kuishi kwa muda mrefu katoka hali ya kutumia madawa na zaidi kupungua kwa nafasi zaidi ukosefu wa nguvu za upendo kutoka kwa ndugu na jamaa wa wazee, kuongezeka kwa kipeo kiuchumi katika nchi za Ulaya, hizi ni baadhi ya mantiki ambazo zimezidi kuongeza udhaifu zaidi kwa wazee. Kwa njia hiyo Bwana Giancarlo Penza amesisitiza kuwa, inahitajika kujenga ile  aina ya maisha ya kiraiki katika miji na miji mikubwa , kiasia kwamba utarifiki unaweza kisinidikizwa wadhaifu na wale ambao wamebaguliwa na kuwa pembezoni mwa jamii ili kuwapokea.

Aidha  Jumuiya ya Mtakatifu Egidio imetoa wito kwa kufanya kampeni yenye jin “kuongenza mtandao wa mahusiano kijamii; kuhamasisha mitindo mipya ya dharura kama mpango” “ Wazee hoyee”. Anayepambania kila siku  kwa ajili ya kijamii na kusaidia udhaifu wa moyo katika matendo yake binafsi, anayelinda haki za wazee kwa namna ya pekee uhuru wa namna gani na wapi mahali pa kuishi maisha yake, ndiyo mantiki msingi na katika  kutenda ili kuweza kuhamasisha urafiki kati ya kizazi, amehitimisha Bwana Giancarlo Penza Mhusika wa wazee katika Jumuiya ya Mtakatifu Egidio Roma.

Hata hivyo, Baba Mtakatifu Francisko, mara nyingi na katika fursa nyingi amekuwa akisisitiza na kusema, kudharau  na kuwabagua wazee ni dhambi,  na a kuonesha utajiri mkubwa walio nao babu na wazee  katika ulimwengu huu  ulio hukumiwa kwa wale wanatafuta kuwabagua na kuwaona kama vizingiti. Baba Mtakatifu anasema kwamba katika jamii ya ustaarabu ambayo haina  nafasi ya wazee na kuwabagua kwasababu wanaleta matatizo, ni jamii yenye  vurusi vya kifo. ( Katekesi ya Papa tarehe 4 Machi 2015). Vilevile Baba Mtakatifu katika ziara ya hivi karibuni huko San Giovan Rotondo  nchini Italia mnamo tarehe 17 Machi 2018, alitaka wazeee wapewe Tuzo ya Nobel ya uzee ambapo kwa dhati amethibitisha ni kumbu kumbu ya ubinadamu.

Katika kilelele hiki, Umoja wa Mataifa kupitia idara yake ya masuala ya kiuchumi na kijamii, UNDESA inasema kuwa dhuluma dhidi ya wazee huathiri haki za kiafya na za kibinadamu  kwa  mamilioni ya wazee, kwa maana hiyo, suala hili ni lazima lipatiwe nafasi kimataifa. Katika kilele cha maadhimisho hayo, UNDESA inatoa sababu ya ya kuendeleza maadhimisho hata kwani mataifa yote  yanatarajiwa kuona ongezeko la wazee kati ya mwaka wa 2015 na 2030 na kasi ya ongezeko itakuwa kubwa zaidi katika nchi zinazoendelea. Kwa hiyo hofu ni kwamba kwa kuwa idadi inaongezeka, vivyo hivyo kadili ya ongezeko hili ndiyo pia idadi ya wazee wanaokumbwa na madhila na ukatili.

Dhuluma dhidi ya wazee imekuwa ni moja ya tukio kubwa ambayo yanawadhalilisha wazee walio wengi, ikiwa ni katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea. Suala hili linaweza kuwa kama kutochukua hatua yoyote kumhusu mzee na hivyo kuleta kutoaminiana na ukosefu wa uaminifu huo humletea mzee maumivu au msongo wa mawazo. UNDESA inaongeza kusema kuwa dhuluma inaweza kuwa ya kisaikolojia, kimawazo au kimwili na wakati mwingine inaweza kuwa ya kingono au kifedha bila kusahau kumpuuza tu mzee kwa makusudi. Idara hiyo inathibitisha katika baadhi ya nchi hupuuzwa na kwenda mbali zaidi na kutowajali wazee. 

Ukatili kwa wazee hufanyika katika nchizote ziwe zinazotaka kuinuka kiuchumi na zile ambazo tayari imeendelea na tena zaidi wazee wanaonekana mzigo. Katika jamii fulani hususan barani Afrika mjane mzee wakati mwingine hulazimishwa kuolewa kwa nguvu na mtu mwingine na katika baadhi ya makabila wazee hutengwa na kushtumiwa kuwa wachawi. Umoja wa Mataifa wameonesha wazi jinsi gani jamii nyingi zimekuwa kimya juu ya dhuluma kwa wazee na katu suala hilo lilikuwa halizungumzwi hadharani hadi siku za karibuni. Ndio maana  baraza kuu la Umoja wa Mataifa, kupitia azimio nambari 66/127, likatenga siku hii ya 15 Juni kuwa siku ya kuhamasisha ulimwengu dhidi ya dhuluma kwa wazee.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.