2018-06-18 09:02:00

Zipo jitihada za kulinda raia wa Palestina na mazungumzo kati ya Israeli !


Askofu  Mkuu Bernadito Auza Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Baraza Umoja wa Mataifa New York ametoa hotuba yake, katika mkutano Mkuu wa 38  kuhusu dharura maalum za Umoja wa Mataifa. Kwenye kikao kilicho fanyika tarehe 13 Juni 2018. Askofu Mkuu Auza kwa niaba ya Vatican anapaongeza  wajumbe wa mataifa katika jitihada za kulinda raia wa wapalestina dhidi ya vurugu mpya zilizowazunguka na kuhamasisha mazungumzo na mchakato kati ya nchi ya Israeli na Palestina kwenye mchakato wa Amani. Kadhalika amasema Vatican inatoa mwangwi kwa mara nyingine tena wa sauti ya Baba Mtakatifu Francisko, kuhusiana na matukio ya mivutano yanayozidi kuendelea  katika nchi Takatifu na Nchi zote za Mashariki, na hasa kwa uchungu na majeraha ya waathirika  na wote ambao wanateseka.

Aidha amekumbusha kwamba kama wote wanavyo jua   uzoefu wa vita kuu, vurugu kubwa na ghasia hata zile ziazoashiria katika hatua chache za nchi, hatua hizo  zinahitaji mazungumzo na mchakato halisi.  Kwa maana amani ni jambo muhimu kwa ajili ya furaha timilfu ya haki za binadamu wote; na kila binadamu anayo haki ya kufurahia Amani na kuishi kwa amani kwa kipindi kifupi ambacho kinawezekana.

Askofu Mkuu Auza pia amaesema kuwa hivi karibu Vatican imekuwa na fursa ya kutoa neno katika Mkutano wa Nne mjini Geneva unao husu Mkataba waulinzi wa raia katika moyo wa sheria za kimataifa kwa ajili ya binadamu. Protokali za 1977 zilizotolewa kwenye Makubaliano ya Geneva zinaboresha sana ulinzi wa kisheria unaofunika raia na waliojeruhiwa. Kwa njai hiyo ni sharti la kibinadamu kutetea ili kuepuka lengo la kuweka  raia na rasilimali za kiraia kama mbinu ya migogoro, pamoja na siasa na  wanajeshi wa msaada wa kibinadamu.

Kutokana na hiyo Vatican kwa mara nyingine tena inatoa wito  ili kuwa na ujasiri wa kusema hapa migogoro;  ndiyo kwa mazungumzo na hapana kuweka vizingiti; ndiyo kuheshimu makubaliano na hapana kuanzisha vurugu na uadui; ndiyo majadiliano na hapana vitendo vya kutisha; ndiyo  usafi wa dhamiri na hapana kuwa undumila kuwili. Yote haya yanahitaji ujasiri na kuwa na nguvu ya kujikita kwa dhati.

Askofu Mkuu Auza amerudaia kutoa wito wake ya kwamba ni lazima kuwa na  hekima ili kuweza kuzua mivutano mingnie  mipya katika mtazamo wa ulimwengu mahali ambapo tayari imesha onesha madhara mengi ya ukatili mkubwa wa migogoro. Na amethibitisha kuwa hatuna  shaka kwamba Jiji Takatifu la Yerusalemu ni sehemu muhimu  wa dini ,si tu kwa wenyeji wa Nchi Takatifu, bali pia hata kwa dini tatu zinazo mtambua Baba yetu  Ibrahimu ulimwenguni kote. 

Kwa sababu hiyo Askofu Mkuu Auza amesema wakati wa  Mkutano  wa saba wa Kikao kuhusu  Mgogoro wa Kumi wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, uliofanyika tarehe 21 Desemba 2017, alisemama ni wajibu wa Mataifa yote kuheshimu hali ya kihistoria ya Jiji Takatifu, kwa mujibu wa Maazimio ya Umoja wa Mataifa husika, na kwamba ni kwa njia ya hali ya uhakika ya kimataifa tu inaweza kuhifadhi tabia yake ya kipekee na kuwa na uhakika wa mazungumzo na upatanisho wa amani katika kanda hiyo.

Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.