Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Askofu mkuu Martin Krebs ateuliwa kuwa Balozi mpya wa Vatican Uruguay

Askofu mkuu Martin Krebs ateuliwa na Papa Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Uruguay. - REUTERS

16/06/2018 15:38

Baba Mtakatifu Francisko ameteua Askofu mkuu Martin Krebs kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Uruguay. Kabla ya uteuzi huu Askofu mkuu Martin Krebs alikuwa ni Balozi wa Vatican kwenye Visiwa vya Marshall na Nauru; New Zealand Visiwa vya Cook, Fiji, Kribati, Palau, Samoa, Shirikisho la Micronesia, Tonga, Vanuatu na pia mwakilishi wa kitume kwenye Bahari ya Pacific.

Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Krebs alizaliwa kunako tarehe 2 Novemba 1956 huko Essen, Ujerumani. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 10 Oktoba 1983. Tarehe 8 Septemba 2008, akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu mkuu na Balozi. Tarehe 16 Novemba 2008 akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu katika Ibada iliyoongozwa na Kardinali Tarcisio Bertone, aliyekuwa Katibu mkuu wa Vatican kwa wakati ule.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S

Vatican News!

16/06/2018 15:38